MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

Habari wadau wenzangu wa Jamii Forum, naomba maoni yenu juu ya kilimo cha zao la mpunga. Napenda pata mawazo yenu juu ya suala zima la kilimo cha mpunga katika kujikwamua kimaisha, nimepata kiasi kidogo cha mkopo nataka peleka katika kilimo ili maisha yaweze songa mbele. Mchango wenu wadau.

Umepanga kulima nini, lini na umefanya mchanganuo vipi?
 
Nataka kulima mpunga mwaka ujao ila maandalizi nafanya mwaka huu nimefanya mchanganuo kuanzia kukodi shamba, maandalizi ya mbegu pia kulima na pesa ya vibalua.
 
Jaribu kuuliza wenyeji kuhusu kukodi,kulima na vibarua eneo husika wanafanyaje ila kwa heka huku wanakodi 75000 kulima 5000 kupanda unalipa kwa siku uhakika wa kupiga 8k had 1M Unakuwepo
 
nimependa wazo lako..kilimo cha mpunga cha lipaa sanaa ila kwa ushaur wangu kama una helaa subir wavunee huwa wanauza bei ndogoo...harafu subiri bei ipande ndio uuze upate faidaaa.....ukilima waweza kuta umekodi umelipa vibaruaa expences nyingiii....harafu ukipata hasara hautatak tena kulima.asante
 
Waadau wa kilimo cha mpunga Dakawa Morogoro, tafadhali naomba ushauri; gharama za shamba kwa ekari ni shilingi ngapi kwa sasa, ekari moja inatoa gunia ngapi , muda wa kupanda hadi kuvuna, muda mzuri wa kupanda ni mwezi gani na changamoto zilizopo kwa sasa.

naomba mrejesho wa mdau wa hii thread nipate picha kamili please.!

Ahsante sana.
 
habari wanajukwaa...kama kichwa kinavyojieleza hapo juu.mimi ni mhitimu wa chuo cha ualimu ngazi ya cheti.kutokana na ajira zetu kutokueleweka ni lini hasa zitatoka nimeamua kutafuta shamba kwa ajiri ya kufanya kilimo cha mpunga.sasa sina utaalamu wa kutosha juu ya kilimo hiki.naomba kama kunamtu mwenye ujuzi anijuze juu ya ipi ni mbegu bora,mbolea za kupandia na kukuzia,madawa ya wadudu na pia kama kunamahitaji mengine.natanguliza shukrani na karibuni kwa michango yenu
 
Habari za asubuhi wadau?
Naomba ushauri, nahitaji niweke mbolea ya maji (booster) kwenye mpunga wangu.
Inatakiwa niweke lita ngapi kwa ekari moja?
Natakiwa niweke mpunga ukiwa na umri gani toka upandwe?
Niweke mara ngapi?
Kila baada ya muda gani?

Asante.
 
mm mwenyew nataka nizame Moro kulima mpunga kwa mdau anaejua bei ya kukodi shamba sas hivi Moro atuambie
 
Hello...
Khabar zenu wapendwa..
Nina shamba la ecre nne lipo bagamoyo.. Maji yake yanafika magotini.. Je linafaa kwa kilimo cha mpunga??.. Na je... Ni mbegu gan nitumie??..
 
Hello...
Khabar zenu wapendwa..
Nina shamba la ecre nne lipo bagamoyo.. Maji yake yanafika magotini.. Je linafaa kwa kilimo cha mpunga??.. Na je... Ni mbegu gan nitumie??..
Unaweza ku control hayo maji?
Yani unaweza kuyaruhusu yatoka na kuyaacha yajae ukihitaji?

Kwa hali hiyo hutaweza kupanda miche au mbegu hadi maji yapungue
 
Hapana... Sijajua hta nitumie njia gan kuyacontrol hayo maji yatokee.. Maana shamba langu lipo bondeni na niyo hukimbilia hapo maji yote..

Unaweza ukanielekeza njia za kucontrol hayo maji..

Me ni mgeni katika kilimo ndo nataka nianze nahitaj sana msaasa wenu
 
Hapana... Sijajua hta nitumie njia gan kuyacontrol hayo maji yatokee.. Maana shamba langu lipo bondeni na niyo hukimbilia hapo maji yote..

Unaweza ukanielekeza njia za kucontrol hayo maji..

Me ni mgeni katika kilimo ndo nataka nianze nahitaj sana msaasa wenu
Inahitaj kuona shamb kwanza ndo mtu apate wazo... Hapo nitakwambia piga mtaro... Weka pampu... Lkn ww ndo unajua jografia ya eneo
 
Hello...
Khabar zenu wapendwa..
Nina shamba la ecre nne lipo bagamoyo.. Maji yake yanafika magotini.. Je linafaa kwa kilimo cha mpunga??.. Na je... Ni mbegu gan nitumie??..
Hapo inabidi ufahamu Hayo maji yanaanza kuingia mwezi gani ili uandae miche yako pindi maji yakianza kuingia ndipo uanze kupandikiza kabla hayajawa mengi zaidi hii itasaidia kwa sababu kuna baadhi ya mbegu za mpunga huwa zinalefuka kufuata level ya maji ila tu yasiwe maji yanayotembea kwa nguvu hivyo mbegu itakayo kufaaa ni "Uhuru"
 
Nahitaj ushaur wenu.. .
Ni shamba la ekari ngap naweza kutoa gunia 100 la mpunga au gunia 90 za mchele??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom