Kilimo cha Mpunga kitaalam na masoko yake


M

Memory

Senior Member
Joined
Jun 29, 2011
Messages
108
Points
170
M

Memory

Senior Member
Joined Jun 29, 2011
108 170
Ndugu wana JF,

kilimo_mbarali-jpg.352130


Naomba kama kuna mtaalamu wa kilimo anisaidie ili nifahamu makadirio ya kiasi cha mavuno ya mpunga katika ekari moja katika kilimo cha kisasa ili tujipange kutekereza sera ya kilimo kwanza!

Naomba pia kufahamu sehemu ambazo unaweza ukapata washauri wazuri wa kilimo cha mpunga ambao si tu wanatumia makaratasi bali wana uzoefu na hii kazi kwa vitendo kwa muda sasa.

Asanteni.

Naomba ushauri jinsi ya kuanzisha shamba dogo la kilimo cha mpunga; maelezo yangu ya awali ni kama ifuatavyo

  1. lengo ni kujiongezea kipato
  2. eneo ni eka 2.5
  3. aina ya mbegu : za muda mfupi zinazonukia , kwa ajili ya kuvutia wateja
  4. aina ya kilimo : ningependa kununua pampu ya kutumia petrol/diesel ili niongezee maji wakati pakiwa na upungufu wa mvua; niwe namwagilia ndani ya vijaruba vidogo; naomba pia ushauri kuhusu aina ya pampu
  5. nitaajiri kibarua 1; atafanya kazi za ulinzi na palizi
  6. Ardhi ni ya kununua ( Tshs 50000 kwa eka), maji yapo ndani ya mita 50 na ni ya kudumu
  7. Mtaji nitategemea mkopo kutoka benki nitakaorejesha ndani ya miaka 4
Naomba ushauri wa hali halisi ya kilimo hiki, je bajeti yangu inatakiwa iewje(kiasi gani), je eneo linatosha au halitaweza kulipa gharama za uendeshaji?, nitaweza kubreak even baada ya muda gani

nawasilisha

---------------------------------
Michango ya wadau
---------------------------------
Mkuu Sendoro Mbazi

eka 2.5 ni sawa na hekta 1, hapo unapata vijaruba 25 vya 20 x 20
kulima kila kijaruba sh 3000(makadirio kibarua), jumla 75000
kwa trekta 50,000 x 2.5 = 125,000
kusawazisha/ harrowing 30 x 2.5 = 75000.

Mbegu tafuta kwa wakulima ndio za uhakika zaidi japo madukani ni kati ya 2500 mpaka 3500
ukisambaza mbegu/broadcasting utahitaji kg 20 x 2.5 = 50 x 3000 = 150,000
ukipanda kitaluni kg 3 x 2.5 = 7.5 x 3000 = 22500 (kuna gharama za kuotesha miche)

Palizi 2, (25 x 3000)2 = 150,000.

niishie hapo kwanza..
sijataja gharama za kuvuna kupiga na kuhifadhi na vingine kama nimesahau

NB: kijana mmoja hawezi palilia peke yake kama hujapanda kwa mistari itamgharimu muda mwingi sana
Mkuu Sendoro Mbazi, hongera kwa kuingia kwenye Kilimo cha mpunga mchango wangu ni huu hapa, utanijulisha iwapo utakuwa ni msaada kukidhi haja yako.

Aina za mbegu
Tumia mbegu iliyothibitishwa na wataalamu iitwayo SARO (TXD 306), inazaa sana gunia 32 kwa ekari moja.
Mbegu hii inaradha nzuri na inakubalika kibiashara. Ekari moja hutumia kilo 10 kwa mpunga wa kupandikiza.
Andaa sh 2500 x 2.5 jumla sh 6250 kama itabidi uzifuate mbali ongeza nauli na gharama za safari zote.

Pump
Tumia pump ya inchi 3 sawa na horse power 5 hadi 6. Ninauzoefu na pump ya JD ni ya petrol. Ekari moja petrol ni lita 5 lakini kwa mpunga itabidi uloweshe shamba mara mbili kwa wiki!

Pump 450,000/= mipira inategemea na umbali toka source ya maji, Pipe ya kunyonyea maji kwenye source 1m sh 8000, utahitaji at least mita 4, (32,000/=), pipe ya kupelekea shambani roll moja urefu wa mita 100 kama litatosha mita 1 sh 2000 ( 200,000/=) dumu la lita 20 kuhifadhia mafuta 3,000 dumu dogo la kupelekea mafuta shamba 1500/=, Petrol lita 4 kwa ekari moja x eka 2.5 x 2 kwa wiki x wiki 6 (assume 6 weeks rain, 6 weeks no rain) x bei ya petrol lita moja 2300/=, service ya pump lita moja ya oil inatosha hadi unavuna, tenga pembeni shs 10,000/= kwa service. Usafiri wa kupeleka na kurudisha pump kama huna baiskeli tenga 2000 kila siku ya kumwagilia kwa umbali ndani ya kilometer 5.
Hapa andaa jumla ya shillingi 974,500/=.

Kama ni shamba jipya
Kutengeneza majaruba idadi yake inategemea mtelemko wa shamba - andaa 50,000/= kwa ekari
kusawazisha ndani ya majaruba (hii ni kazi ngumu na kubwa sana kutegemea na slope ya shamba) andaa angalau laki 3 kwa kila ekari moja. Shamba la mpunga sharti liwe level ili kumwagilia kwa urahisi, hii ni very expensive operation, kutengeneza shamba la mpunga ni kama ujenzi wanyumba, ukishatengeneza unabaki ukarabati tu.
Andaa 350,000/= x 2.5 jumla 875,000

Bei ya shamba 50,000 x 2.5 jumla 125,000/=

Gharama zingine za shambani zote kwa ujumla hadi unarudisha mzigo tenga pembeni sh 700,000/= kwa ekari moja kwa hiyo jumla gharama 1,750,000/=

Jumla ghafi 3,730,750/= ongezea 10% tahadhari (373,075/=)

Jumla kuu 4,103,825/=

Ukifuata utaalamu utavuna gunia 32 kwa ekari lakini kwa kuwa na uhakika assume mavuno gunia 25 kwa ekari. Uza bei ikifikia 80,000/= kwa gunia la kilo 100/=
Mapato itakuwa 5,000,000/=
Faida 5,000,000/= kutoa 4,103,825/= inabaki 896,175/=

Mahesabu yanaonesha kuwa utarudisha pesa uliyowekeza na kupata faida
Faida kubwa zaidi ni shamba ambalo utakuwa umeshali-level tayari itakusaidia kuwa na gharama kidogo za umwagiliaji na level inafaida nyingi sana, hutaingia garama hii ya levo miaka ijayo bali ni kufanya usawazishaji mdogo tu.

Nakushauri ukitaka kufanikisha kilimo cha mpunga hakikisha unaweka shamba lako level, yaani ukiweka maji kwa kina cha sm 1 au 2 yasambae jaruba lote kwa kina cha sm1 au 2. Level kweye shamba la mpunga haina mbadala, kutengeneza jaruba na kuweka level ni mambo ya LAZIMA kwenye shamba la mpunga!
Nimewasilisha !!!
Maandalizi sahihi ya shamba ni jambo la msingi katika kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga. shamba lisipoandaliwa vema husababisha mbinu bora zinazoshauriwa kutoonyesha matokeo katika kiwango kinachotarajiwa hasa katika uzalishaji. Kimsingi maandalizi ya shamba yanatakiwa yafanyike kwa usahihi na kwa wakati katika mtiririko unaotakiwa. Zifuatazo ni hatua saba muhimu na za msingi katika kilimo cha mpunga.

1.KUSAFISHA SHAMBA
Safisha shamba mapema kabla ya msimu kuanza. Kusanya na kuangamiza visiki na takataka nyingine zote. Masalia ya mazao yanaweza kutumika kutengeneza mbolea ya mboji. Inapobidi tumia moto kwa uangalifu sana maana moto unaweza kuharibu mazingira, unaua wadudu rafiki, unaharibu udongo na kuteketeza mboji.

2.KULIMA
Kulima husaidia kupunguza kiasi cha magugu, huruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji, hurahisisha mizizi kupenya na kuchanganya masalia ya mazao kwenye ardhi. Wakati wa kulima uangalifu unahitajika ili kuzuia kuharibu usawa wa ardhi. Kina cha kulima kiwe kati ya sentimeta 10 na 15. Ili kurahisisha na kuharakisha kazi ya kulima ni vema kutumia zana/mashine rahisi kama Trekta la mkono na wanyamakazi

3.KUKARABATI/KUJENGA MAJARUBA
Baada ya kulima hakikisha kuwa kingo za jaruba zimekarabatiwa ili kuweza kuhifadhi maji vema. Kama ni shamba jipya, ujenzi wa kingo za jaruba ufanyike kwa kufuata utaalamu unaotolewa. Kingo imara ni muhimu kudhibiti vema maji shambani.

4. KUVURUGA
Weka maji shambani kiasi cha sentimeta 3 hadi 5 juu ya usawa wa ardhi ili kukamilisha vema uvurugaji. Jembe la mkono linatumika lakini ili kurahisisha na kuharakisha kazi hii ni vema kutumia trekta la mkono au wanyamakazi. Unapotumia wanyamakazi au trekta la mkono weka maji shambani si zaidi ya siku moja kabla. Shamba lililovurugwa vema huiwezesha mizizi ya miche kupenya vema ardhini.

5. KUSAWAZISHA SHAMBA
Baada ya kuvuruga ni lazima kuhakikisha kwamba shamba limesawazishwa vema. Shamba lililosawazishwa vema linaruhusu usambaaji mzuri wa maji. Wakati wa kusawazisha kina cha maji kiwe kiasi cha sentimeta 3-5 juu ya usawa wa ardhi Ili kurahisha kazi hii tumia reki ya ubao ili kuvuta udongo kutoka sehemu zilizoinuka kuelekea sehemu zilizo bondeni

6.VYANZO NA ATHARI ZA UPOTEVU WA MAJI YA UMWAGILIAJI
Ili kupata maji ya kutosha inabidi kuhakikisha kwamba upotevu wa maji ya umwagiliaji unapungua kwa kiwango kikubwa na wakulima wanamwagilia maji kwa kiasi kinachohitajika bila kuzidisha kiwango.

Vyanzo vya upotevu wa maji ya umwagiliaji katika skimu za mfano ni pamoja na:
• Maji yanayopotea kwenye mifereji mikuu, ya kati na ile midogo ya kusambaza maji mashambani.
• Maji yanayopotea mashambani wakati wa kumwagilia.

Upotevu wa maji kwenye mifereji mikuu, ya kati na ile ya kusambaza maji unasababishwa na aina ya udongo uliotengeneza kingo za mfereji, uchafu na matengenezo hafifu ya mifereji. Katika baadhi ya skimu upotevu wa maji kwenye mfereji mkuu uliosababishwa na kuvuja maji kwenye tuta la mfereji mkuu na kunywea chini ya ardhi ulikuwa mkubwa kiasi cha kuathiri upatikanaji wa maji kwenye mashamba yaliyoko mbali na banio.Vilevile athari nyingine ilikuwa ni maji mengi kuingia sehemu yasikohitajika na kusababisha tatizo la maji kutuama kwa muda mrefu.Hivyo wakulima wanashauriwa kupunguza upotevu huu wa maji kwenye mfereji kwa kujengea na kusakafia. Upotevu wa maji mashambani wakati wa kumwagilia unasababishwa na kuvuja kwenye tuta linalozunguka jaruba, kunywea chini na kuzidisha kiwango cha maji ya kumwagilia kinachotakiwa. Hii mara nyingi inasababishwa na utengenezaji mbovu wa jaruba. utengenezaji wa majaruba na uimarishaji wa kingo za jaruba umesaidia kupunguza upotevu wa maji kwa kiwango kikubwa na hatimaye kuongeza mavuno na kipato cha mkulima.

7. UPANDIKIZAJI MPUNGA
Ili kupata mavuno mengi na kukifanya kilimo cha mpunga kuwa cha faida ni muhimu wakulima kuzingatia mbinu hii muhimu na kuachana na kilimo cha kiholela kwa kumwaga mbegu moja kwa moja shambani. Aidha kwa wakulima wanaofuata kanuni hii wamepata mafanikio makubwa.

Faida zinazopatikana kwa kupandikiza mpunga
• Mkulima huweza kuchagua miche bora na mizuri ikiwa kitaluni.
• Miche hukua haraka na yenye afya .
• Kiasi kidogo cha mbegu huhitajika.
• Mavuno huwa mengi.

Njia za kupandikiza miche ya mpunga
Zipo njia kuu mbili za kupandikiza miche ya mpunga, nazo ni:
• Kupandikiza kwa mistari
• Kupandikiza bila ya kufuata mistari (Mchaka mchaka).

Aidha kati ya njia hizi mbili, njia ya kupanda kwa mistari ndiyo inayopendekezwa.zaidi. Pamoja na kwamba upandikizaji wa mistari unahitaji nguvu kazi zaidi, njia hii imeonyesha kuwa na mafaniko mengi ikilinganishwa na kupandikiza kiholela. Shamba lililopandwa kwa mistari ni rahisi kupalilia kwa kutumia kipalizi cha kusukuma kwa mkono. Pia ni rahisi kwa mkulima kupanga idadi ya mashina/mimea kwa eneo kwa uchagua nafasi aitakayo itakayompa mazao mengi.

Uandaaji wa miche
Kabla ya kupandikiza miche shambani ni muhimu kufanya maandalizi yafuatayo:
• Inashauriwa kumwagilia miche kwanza ili kupata urahisi wa kungo’a
• Ili kuzuia miche isikatike ovyo, miche ing’olewe kwa kushikwa chini zaidi ya shina
• Epuka kung’oa miche mingi kwa wakati mmoja
• Miche ifungwe kwenye mafungu madogo madogo ili kurahisisha usafirishaji na upandikizaji shambani
• Miche bora tu ndio ichaguliwe. Sifa za miche bora
• Iwe na kimo kinacholingana,
• Iwe na majani mafupi yaliyosimama, yenye mizizi mingi na yenye afya, isiyoshambuliwa na wadudu wala magonjwa,

Jinsi ya kupandikiza miche
• Miche ishikwe kwa vidole vitatu kama inavyoosha kweye picha chini
• Pandikiza kati ya miche 2 -3 kwa kila shina
• Kwa mafanikio zaidi, miche ipandikizwe katika kina cha sentimita 2-3.

Chanzo: Mitiki
 
kasopa

kasopa

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Messages
303
Points
195
kasopa

kasopa

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2010
303 195
Mkuu wewe upo maeneo gani na unashamba au unategemea kukodi mashamba kama unaweza kwenda dakawa kunawanakijiji wanakodisha mashamba na kama utabahatisha kwenye block za iliyokuwa nafco kunawatu hukodisha block zao utapata watala hukohuko
 
Chiwa

Chiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2008
Messages
2,330
Points
2,000
Chiwa

Chiwa

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2008
2,330 2,000
Ni kigumu kinahitaji kujitoa na usimamizi wa kutosha unaweza ukapata gunia 30 kwa eka inategemea unalima wapi unatumia nini na umejitumaje hili ni shamba la watani zangu wapogoro hawa hawtumii mbolea wala planter.
 
M

Memory

Senior Member
Joined
Jun 29, 2011
Messages
108
Points
170
M

Memory

Senior Member
Joined Jun 29, 2011
108 170
Mkuu wewe upo maeneo gani na unashamba au unategemea kukodi mashamba kama unaweza kwenda dakawa kunawanakijiji wanakodisha mashamba na kama utabahatisha kwenye block za iliyokuwa nafco kunawatu hukodisha block zao utapata watala hukohuko
@Kasopa nashukuru sana kwa msaada wako japo bado nategemea kupata estimates of maximum yield katika ekari moja kama kilimo kimefanyika kitaalam ili nifanya maamuzi ya mwisho ya kujua kiasi/ukubwa wa eneo ninalotakiwa kutafuta. Ninafanya utafiti wa kupata maeneo ya kilimo kanda ya Ziwa victoria na Mbeya. Jana kuna mtu amenipatia data za Kilombero hivyo nafikiria pia kufuatilia ikiwa ni pamoja na Dakawa kama ulivyoniambia. Haya ni maandalizi ya kazi ya Mwakani.
 
M

Memory

Senior Member
Joined
Jun 29, 2011
Messages
108
Points
170
M

Memory

Senior Member
Joined Jun 29, 2011
108 170
ni kigumu kinahitaji kujitoa na usimamizi wa kutosha unaweza ukapata gunia 30 kwa eka inategemea unalima wapi unatumia nini na umejitumaje hili ni shamba la watani zangu wapogoro hawa hawtumii mbolea wala planter
Chiwa,
Nashukuru kwa ushauri wako ila naomba ufahamu kuwa hakuna kitu kirahisi hapa Duniani na kadri kitu kinapokuwa kigumu kupatikana ndivyo faida kubwa inavyozidi kupatikana. Dhahabu ni ngumu sana kupatikana na ndiyo maana inalipa zaidi n.k. Tunachotakiwa watanzania ni kufanya kazi kwa bidii zote ili kuongeza vipato vyetu, hii ndiyo siri pekee ya mafanikio. Hata China ya leo imefikiwa baada ya wananchi kujituma katika kazi na biashara na kupata security za mikopo. Kama ungenipatia analysis ya prifit margin katika kilimo cha mpunga ingenisaidia zaidi lakini kama hoja ni kujituma, hilo lisikupe shaka.
 
kasopa

kasopa

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Messages
303
Points
195
kasopa

kasopa

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2010
303 195
Mkuu mimi kwa maono yangu mpunga unalipa sana tu wala usihofu ispokuwa tafuta eneo lenye maji yakutosha yani usitegemee mvua hasakama utapata maeneo ya mkoa wa morgoro ni nzuri zaid kwakuwa huku gharama za undeshaji ni ndogo ukilinganisha na bara na bei pia huku ni nzuri huduma za madawa beipoa na zinapatkana vinginevyo laba uwe na unyeji wahuko nyanza lakini mimi nakushauri utafute shamba sehem za huku hata samani yake ni tofauti na nyanza kila mwaka linapanda marambili mikopo pia inakubalika kiurahisi kama utakim nyaraka zinazo takiwa
Mungu akubariki ufanikiwe ndotoyako mkuu
@Kasopa nashukuru sana kwa msaada wako japo bado nategemea kupata estimates of maximum yield katika ekari moja kama kilimo kimefanyika kitaalam ili nifanya maamuzi ya mwisho ya kujua kiasi/ukubwa wa eneo ninalotakiwa kutafuta. Ninafanya utafiti wa kupata maeneo ya kilimo kanda ya Ziwa victoria na Mbeya. Jana kuna mtu amenipatia data za Kilombero hivyo nafikiria pia kufuatilia ikiwa ni pamoja na Dakawa kama ulivyoniambia. Haya ni maandalizi ya kazi ya Mwakani.
 
Chiwa

Chiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2008
Messages
2,330
Points
2,000
Chiwa

Chiwa

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2008
2,330 2,000
Mwaka jana nililima Ifakara ikala kwangu japo nisiwe mnafki sikuweza kusimamia vizuri na resource hazikutosha sana kwa kifupi kulikuwa na uzembe mwaka huu najipanga tena kulima na nimejaribu kufanya gharama za awali ili nione ina kuwaje kama ninavyo kutumia nadhani kwa mchanganuo huu tutawachokonoa wadau watusaidie zaidi kwani nina plan ya miaka mitatu kwa kila mwaka kuongeza eneo na pia nina mpango wa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kwa kuanzisha umoja wao na kupata bei nzuri zaidi
nashidwa ku attachView attachment ifakara-estmate.xls
 
Chiwa

Chiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2008
Messages
2,330
Points
2,000
Chiwa

Chiwa

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2008
2,330 2,000
Kuna garama za chini za mahitaji hizo huwa zinarudi kwa kila kitu tunawauzia wasaidizi wa shamba kwa mfano umenunua jiko shs 70000 wanfanya kazi inayofanana na hiyo wakati wa kuondoka unawapa jiko japo mimi nimeamua kutoa hizo bidhaa kwa bei nafuu kwa kiasi fulani ili wasiumie sana.
 
kasopa

kasopa

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Messages
303
Points
195
kasopa

kasopa

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2010
303 195
Mkuu mbona kuna mapunguf mengi kwenye mchakato wako napia umepanda gunia tatu 3 katika heka 15 ulitakiwa upande gunia4 napia ni aina gani ya mbegu uliyopanda na unaweza kutujuza ni kiasi gani ulivuna kwa sababu haiwezekani ule hasara kwa heka 15 hata iweje labda mpunga ufe ama hukuzingatia mbegu bora nayo pia ni ngum sana kupiga chini kwa hesabu hata kamaulilima kienyeji basi ungeambulia hata 6m sio ukose kabisa . kwa heka 15 matarajio ya mavuno ni gunia30 kwa heka mbegu bora na matunzo usitegemee mvua utaumia mtalam lazima uwe nae
mwaka jana nililima ifakara ikala kwangu japo nisiwe mnafki sikuweza kusimamia vizuri na resource hazikutosha sana kwa kifupi kulikuwa na uzembe mwaka huu najipanga tena kulima na nimejaribu kufanya gharama za awali ili nione ina kuwaje kama ninavyo kutumia nadhani kwa mchanganuo huu tutawachokonoa wadau watusaidie zaidi kwani nina plan ya miaka mitatu kwa kila mwaka kuongeza eneo na pia nina mpango wa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kwa kuanzisha umoja wao na kupata bei nzuri zaidi
nashidwa ku attachView attachment 35717
 
Chiwa

Chiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2008
Messages
2,330
Points
2,000
Chiwa

Chiwa

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2008
2,330 2,000
Unachosema ni kweli hiyo kwanza ni plan ya mwaka huu bado inamarekebisho sio gharama halisi mwaka jana nililima eka kumi nikapata gunia 22 usiogope ndo ukweli nilitumia kama 2m kwa kilimo chote kuna mambo mengi lakini kubwa ni usimamizi mbovu kwa kumuamini mtu nilivyoenda kwenye mavuno nikakuta aibu yangu lakini mwaka huu sitaki utani mbaya zaidi hata mbegu walinichanganyia kwa wastani kama usimamizi umekwenda vizuri kulingana na mashamba ya majirani umekosa kabisa basi gunia sita kwa heka japo kuna ugojwa wenyeji wanauita kimyanga huo unaweza kula shamba zima.

Nakushauri tafuta fedha ingia utajua vizuri hapa kweye computa hakuna kitu gharama muhimu ndo hizo maelekezo mengine mbele kwa mbele.tuache uwoga.

Hasara inawezekana wako walio panda hekari 100 na kupata gunia mbili acha wali uwe mtamu muhimu ni kufanya na kurekebisha makosa kadri unavyozoea shamba.
 
M

Memory

Senior Member
Joined
Jun 29, 2011
Messages
108
Points
170
M

Memory

Senior Member
Joined Jun 29, 2011
108 170
Mkuu mimi kwa maono yangu mpunga unalipa sana tu wala usihofu ispokuwa tafuta eneo lenye maji yakutosha yani usitegemee mvua hasakama utapata maeneo ya mkoa wa morgoro ni nzuri zaid kwakuwa huku gharama za undeshaji ni ndogo ukilinganisha na bara na bei pia huku ni nzuri huduma za madawa beipoa na zinapatkana vinginevyo laba uwe na unyeji wahuko nyanza lakini mimi nakushauri utafute shamba sehem za huku hata samani yake ni tofauti na nyanza kila mwaka linapanda marambili mikopo pia inakubalika kiurahisi kama utakim nyaraka zinazo takiwa
Mungu akubariki ufanikiwe ndotoyako mkuu
Thanks kwa ushauri
Naomba kama una data za maeneo mhimu kwa kilimo cha mpunga katika mkoa wa Morogoro uwe wa kwanza kunipatia hapa ili niweke plan yangu vizuri kwa ajili ya kuyatembelea nikianza na Dakawa kama ulivyo nitajia hapo awali.
Ahsante!
 
M

Memory

Senior Member
Joined
Jun 29, 2011
Messages
108
Points
170
kasopa

kasopa

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Messages
303
Points
195
kasopa

kasopa

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2010
303 195
Bilashaka mkuu kidogo nipo nje ya eneo nategemea kurudi tareh28 nikifika ntaku pm kama vip twende ukaonane na wenyeji mojkwamoja
Thanks kwa ushauri
Naomba kama una data za maeneo mhimu kwa kilimo cha mpunga katika mkoa wa Morogoro uwe wa kwanza kunipatia hapa ili niweke plan yangu vizuri kwa ajili ya kuyatembelea nikianza na Dakawa kama ulivyo nitajia hapo awali.
Ahsante!
 
Mu-Israeli

Mu-Israeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2012
Messages
2,458
Points
1,250
Mu-Israeli

Mu-Israeli

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2012
2,458 1,250
Hi wana JF,
Kuna njia mpya ya kisasa katika kilimo cha mpunga ambayo huweza kuongeza mavuno kwa 50% hadi 100% bila kutumia madawa au mbolea za kisasa.
Kilimo hiki cha kisasa kinaitwa SRI (System of Rice Intensification).
Kilimo hiki cha kitaalamu tayari kinatumika katika nchi kadhaa.
Katika kilimo hiki mpunga hupandwa kwa nafasi ya cm 25 toka shina hadi shina, na pia kila shina la mpunga hupandikizwa mche (seedling) mmoja au miwili tu.
Kilimo hiki pia hutumia kiasi kidogo sana cha maji maana mimea ya mpunga hautakiwi kukua ikiwa kwenye maji mengi.

Maelezo zaidi yanapatikana kwenye link hii:-

http://sri.ciifad.cornell.edu/

Pia unaweza ku-search kwenye youtube ukapata videos zinazoelezea vizuri zaidi.

Nawakilisha (Siasa ni Kilimo).
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
33,231
Points
2,000
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
33,231 2,000
Safi sana mkuu itatusaidia sana!
 
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,427
Points
2,000
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,427 2,000
Desa la nguvu ili Tz hasa kyela,ifakara,Mangula,mbarali wengi hutumia system ya kumwaga mpunga badala ya kupanda
 
Narubongo

Narubongo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
2,074
Points
1,250
Narubongo

Narubongo

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
2,074 1,250
Mkuu nimejaribu kufuatilia hii kitu nimeona ina tija sana. Nitaenda kuongea na mshauri wangu wa kilimo kuona kama nitaweza kuapply shambani kwangu. Tatizo ni kwamba wataalamu wetu wakilimo wapo outdated sana na vitu kama kama hivi. Wao na internet ni vitu viwili tofauti
 
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
27,734
Points
2,000
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
27,734 2,000
Hi wana JF,
Kuna njia mpya ya kisasa katika kilimo cha mpunga ambayo huweza kuongeza mavuno kwa 50% hadi 100% bila kutumia madawa au mbolea za kisasa.
Kilimo hiki cha kisasa kinaitwa SRI (System of Rice Intensification).
Kilimo hiki cha kitaalamu tayari kinatumika katika nchi kadhaa.
Katika kilimo hiki mpunga hupandwa kwa nafasi ya cm 25 toka shina hadi shina, na pia kila shina la mpunga hupandikizwa mche (seedling) mmoja au miwili tu.
Kilimo hiki pia hutumia kiasi kidogo sana cha maji maana mimea ya mpunga hautakiwi kukua ikiwa kwenye maji mengi.

Maelezo zaidi yanapatikana kwenye link hii:-

The System of Rice Intensification

Pia unaweza ku-search kwenye youtube ukapata videos zinazoelezea vizuri zaidi.

Nawakilisha (Siasa ni Kilimo).
Ngoja nikiprint halafu nikamfundishe bibi kule shinyanga..
thanks for the post buddie..
 

Forum statistics

Threads 1,293,769
Members 497,735
Posts 31,152,863
Top