Kilimo cha miwa Kilombero na rushwa ni jipu kwa wakulima

queen of the jungle

JF-Expert Member
Mar 17, 2017
228
429
Habari wapendwa kumekuwa na sintofahamu ya uvunaji miwa Kilombero, bila rushwa hutoi miwa yako na hii ni kutokana na uongozi kutokuwa na usimamizi wa kutosha hasa inapofika kipindi cha uvunaji na nimegundua wanafanya hivyo makusudi ili kuweka mianya ya rushwa kwa wakulima.

Mfano kama viongozi wangeamua kuweka usimamizi kama vile kupanga ratiba za uvunaji zinazoeleweka labda kijiji A wiki yenu ni hii then muwa wote ukavunwa kwa pamoja kuliko hii ya kuchagua mwenye fedha ya kuhonga ndiyo anavuniwa kwanza.

Kitendo cha kuchagua watu wa kuvuniwa kimepelekea baadhi ya wananchi kuamua kuchoma muwa wao ili angalau wakumbukwe kitendo ambacho kimesababisha hasara kubwa kwa wakulima wadogo ambao muwa wo unaungua kwenye ajari lakini hawana hela ya kuhonga ili kuutoa shambani matokeo yake unaozea hapo na inaleta uchungu maana kuna wengine huwa wanakopa kwa ajili ya hicho kilimo.

Kinachosikitisha ni kwamba muheshimiwa Rais anasema sukari ni chache nchini na kuomba kuongeza viwanda wakati kuna miwa mpka sasa haijavunwa na kiwanda na mpka itaharibika au itakuja kupata ajari ya moto na itaishia kutupwa.

Mbali na hivyo kumekuwa na rushwa mno na inaomba peupe na kuanzia ngazi ya chini kabisa kitu ambacho ni unyama kama huna hela wakati wa kuvuna wanakuruka wanaenda kumvunia aliewapa hela. kwa leo naomba niishie hapa
 
Back
Top Bottom