Nimekuwa nafuatilia threads zinazohusu kilimo na kuvutiwa na jinsi mnavyochangia-mfano Elnino na Malila na members wengine. naomba kuuliza kama nitaamua kulima MITIKI (teak wood). Sasa naomba mwenye utaalamu anisaidie kunielewesha yafuatayo:
- Je unapotaka kupanda mitiki je mbegu zinauzwa wapi?
- Je mbegu unazipanda kwenye vimfuko vidogovidogo na udongo wake (i.e kitalu). je mche unapotolewa kwenye kitalu unaupanda moja kwa moja shambani au kuna process nyingine?- i.e. yaani namaanisha hatua (steps) za kutoa kwenye kitalu kwenda shambani
- Je unatakiwa kuweka umbali gani kati ya mtiki/mche mmoja na mwingine kama unataka ikue kwa ajili ya mbao.. na je spacing ni kiasi gani kama unataka ikue na uvune kama milingoti
- Je kwenye ekari moja unaweza kupanda miche mingapi?
- Je KIWASTANI inachukua miaka mingapi mpaka uvune kupata mbao na pili kupata milingoti
- Je kuna paper au website ninayoweza kupata maelezo zaidi?
[h=3]JINSI YA KUKATA MICHE YA MISOJI (MITIKI)[/h]
Kwa kawaida miche ya misoji mara baada ya kutolewa kwenye kitalu huitaji kukatwa, mjasiliamali aliyeko jijini Mwanza aitwae NAYMA aliniomba nimwelekeze kwa picha na mimi bila hiyana nilikwenda shamba na kung,oa mche mmoja na kuukata na kuupiga picha kabla ya kuukata na baada ya kuukata ili kupata kipandikizi
MCHE KABLA YA KUKATWA (angalia mishale kujua sehemu za kukata)
Mche wangu niliukata na kuacha kiasi cha nchi mbili au pingili mbili za vidole kwa sehemu ya juu ya mzizi na kwenye mzizi niliondoa ile sehemu nyembamba ya chini, kwa kawaida hii sehemu ya chini hufa mara baada ya kupandwa kwa sababu sehemu nene/kubwa ya mzizi inayoachwa ndiyo huifadhi maji na chakula cha mmea, nadhani hapa nitakuwa nimemsaidia kama bado nipigie kwenye ile namba niliyokupa
KIPANDIKIZI TAYARI KWA KUPANDWA
Kumbuka wakati wa kupandwa lazima uweke kisahani ili kiweze kukusanya maji kwa ajili ya ukuaji mzuri, kama ni udongo unaotuamisha maji usiweke kisahani bali wekea kama tuta au mwinuko
WEKA KISAHANI KAMA UDONGO HAUTUAMISHI MAJI
WEKA TUTA KAMA UDONGO UNATUAMISHA MAJI