kwemanga1
JF-Expert Member
- Jan 9, 2014
- 839
- 599
Asante mkuuwaone mohammed entreprises
Asante mkuuwaone mohammed entreprises
Hlw mkuuMimi nilipanda mitiki miche 6000 mwaka 2010 ilikua kama najaribu tu na sina utaalamu sana sasa miti imekua mirefu sana ( kwa kudaria urefu ni zaidi ya jengo la gorofa mbili ) nataka mwenye ujuzi anifahamishe maana nimeambiwa ni muda muafaka kupunguzwa, je hiyo inayopunguzwa naweza pata soko wapi? Maana inayopunguzwa ni zaidi ya miti 2000
Mkuu Contequil,Hlw mkuu
Mkuu kisima iyo bei 250 kwa 3200 pcs, ni mche ambao utaenda pandwa shambani au ni stump inayohitaji kuoteshwa ktk mfuko then ndo iende shamba baadae, na unahisi nikiandaa shamba na mashimo kila kitu upandaje na timu yako inaweza kuwa bei gani, kwa mfano shamba likiwa kilomberoSalama mkuu!
Moro naishi Turiani karibu kabisa na mtibwa teak forest.
Mbegu zipo zakutosha kulingana na shehena ya uhitaji wako.
Bei yangu inavary kulingana na wingi wa miche(stamps) utakazo.
Mathalani kama order yako itafikia miche 3200(ambayo unaweza panda ekari5) ntakuuzia kwa sh250 kila mche na kutakuwa na offer ya miche 300 bure!
Ikiwa order yako ni zaidi ya miche 16000 bei itapungua hadi 200@mche na kutakuwa na nyongeza ya miche 1000.
Utaratibu ni unalipia 50% ya mzigo na 50% nyingine utamalizia on delivery day.
Kama utahitaji huduma ya kupandiwa kitaalam, mimi na team yangu tupo tayari kukuhudumia popote lilipo shamba.
Karibu sana mkuu!
Hiyo ni bei ya stumps mkuu.Mkuu kisima iyo bei 250 kwa 3200 pcs, ni mche ambao utaenda pandwa shambani au ni stump inayohitaji kuoteshwa ktk mfuko then ndo iende shamba baadae, na unahisi nikiandaa shamba na mashimo kila kitu upandaje na timu yako inaweza kuwa bei gani, kwa mfano shamba likiwa kilombero
Mimi natafuta mbao za ujenzi. Ofcourse Kama ningeweza ningetamani nipate mbao za mitiki. Sasa kuna mwenye uzoefu na mbao za mitiki? Kuna Hawa wazungu WA Kilombero Valley Teakwood. Nimetembelea website Yao na kuongea na one of their managers inaonekana focus Yao in export. Anybody anayewajua? Atupie neno hapa. Vile vile Kama kuna mtu anayejua sehemu nyingine wanauza teakwood mbao in large quantity humu humu Tz.
Asanteni in advance.[/QUOTE Unataka mbao size gn npgie 0784616544
stumps ndio nini mkuu?Stumps ndio njia rahisi sana kuliko kununua miche au mbegu.
Stumps kuna jamaa moja anaitwa kisima mtafute humu utampata.
Muagizie akuletee stumps nene na nzuri atakuletea.
Mimi stumps 5000 aliniuzia kwa milioni moja.
Akikuletea hesabu kabla ya kummalizia pesa.
Chukua udongo wenye rutuba au inaweza changanya na mbolea ya ngombe .
Kisha mchanganyo huo changanya na fungicides then pakia kwenye viroba.
Wakati wa kupanda stumps
Stumps huwa ni ndefu zikate kwa chini kidogo.kisha zichomeke kwenye vifuko.
Zichomeke hadi ziwe na usawa sawa na udongo ukiojaza kwenye mfuko.
Hapo ni kumwagia tu ndani ya miezi miwili unapori la miti kwenye kitalu chako.
Jitahidi kuilinda na wadudu kwa kumwagia insectcides.
Soma masage zotestumps ndio nini mkuu?
Wacha ukoraFunqicides ni nn mkuu
Samahani sana mkuu kwa kuchelewa kupata notification ya post hii.Mkuu Kisima msila ndio mti gani huo? Je, unakubali maeneo ya mkoa wa Pwani kama vile Mkuranga? Jibu tafadhali ili niangalie uwezekano wa kuagiza mbegu toka kwako.
Samahani sana mkuu kwa kuchelewa kupata notification ya post hii.
Msila upo kwenye jamii ya msedela au mkangazi, isipokuwa hurefuka zaidi na hujipogolea wenyewe na ni imara zaidi.
Matawi yake huota kwa mpangilio kwa seti maalum kama ilivyo miti ya uzazi wa mpango.
Miti hii mbao zake hutumika kwa kupaulia na pia kama fenicha.
Haubunguliwi na wadudu.
Sifa kuu ya msila ni kwamba inakuwa haraka kuliko carribeae pine, ndani ya miaka7 inakuwa tayari kwa kuvuna.
Inastawi zaidi ukanda wenye mwinuko wa wastani na pawe na joto la wastani.
Kwa ukanda wa pwani miti hii inastawi bila shida yoyote.
Mahala panapo stawi mkangazi au msedelela, hata msila unastawi.
Msila kwa jina jingine huko kanda ya ziwa inajulikana kama "mihumula" tafasiri yake ni "mti tulivu"
Kama utahitaji mbegu za miti hii nicheck
Sawa mkuu.Mkuu nitakucheki ngoja hali ya usalama itengemae kule maana hivi sasa maeneo yale hajulikani nani mkulima nani mhalifu. Niangalie uwezekano wa kupanda miche kadhaa.
Kaina, mawazo yako ni kama yangu.Kila siku naona makala na thread zikizungumzia kilimo cha mitiki na jinsi inavyohitajika sana. Ila sijawahi kuona mtu akitoa kuhusu bei hasa ya mitiki ikishakuwa mikubwa iwe ni kwa mti mmoja mmoja au kwa eka ili kutuhamasisha kulima na pia kutufanya kufanya cost-profit analysis kabla ya kulima. Pia sionagi mtu akieleza ni wapi hasa soko la mitiki lipo au ni kampuni zipi hasa zinanunua mitiki.
Sio kwamba napinga kulima mitiki, ila inakuwa kama hakuna mtu mwenye uhakika hasa wa ni faida kiasi gani (hata kwa makadirio ya wastani, maana bei ni maelewano) mtu anaweza kupata baada yabkuwekeza kwa hiyo miaka 15-20.
Kama yupo mtu wa namna hii naomba atusaidie kutuelewesha zaid. Asante
Hate me at your own risk
Kila siku naona makala na thread zikizungumzia kilimo cha mitiki na jinsi inavyohitajika sana. Ila sijawahi kuona mtu akitoa kuhusu bei hasa ya mitiki ikishakuwa mikubwa iwe ni kwa mti mmoja mmoja au kwa eka ili kutuhamasisha kulima na pia kutufanya kufanya cost-profit analysis kabla ya kulima. Pia sionagi mtu akieleza ni wapi hasa soko la mitiki lipo au ni kampuni zipi hasa zinanunua mitiki.
Sio kwamba napinga kulima mitiki, ila inakuwa kama hakuna mtu mwenye uhakika hasa wa ni faida kiasi gani (hata kwa makadirio ya wastani, maana bei ni maelewano) mtu anaweza kupata baada yabkuwekeza kwa hiyo miaka 15-20.
Kama yupo mtu wa namna hii naomba atusaidie kutuelewesha zaid. Asante
Hate me at your own risk
Kaina, mawazo yako ni kama yangu.
Kuna jamaa yangu amelima mitiki heka 50 na. Nilimuuliza hayo maswali na alishindwa kujibu.
Sipingi kulima mitiki, ila nadhani ulimaji wake umekuwa exagorrated. Ni kama ukuzaji wa sungura. Poleni kusema haya.
Cut point niliyoiona, ni kwamba mitiki inakomaa baada ya miaka 25 na.... Kwa maana hiyo, hii investment sio yako tena, ni ya wanao.
Kwa maana hiyo, kulima mitiki ni excess wakati una mambo mengine ya kufanya. Maana yake hutategemea mitiki kuishi.