KILIMO CHA MITI

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,988
1,175
Habari wana JF.

Naomba wale walio na uzoefu wa kilimo cha Miti wanifungue macho kidogo. Nina heka kadhaa za ardhi katika ukanda wa Pwani ambapo nilijaribu kulima mazao ya kawaida (Nafaka) mwaka huu ambapo niliambulia zero ingawa niliwekeza sana katika ulinzi ambao ulinisaidia tu kuwadhibiti tnguruwe wakati wa usiku kwa kutumia Seng’enge (wire). Wanyama walionisumbua sana ni nyani na jamii yake na ngochiro na jamii yake ambao walikuwa wanaingia shambani muda ambao ilituwia vigumu kuwadhibiti.Eneo hilo lina mapori mengi na ni dhahiri usumbufu wa hawa wanyama unaweza kuendelea kuwepo kwa alau miaka mitano hadi kumi ijayo. Kutokana na niliyoyaeleza hapo juu ninawaza kusafirisha ardhi yote na kupanda miti kwa ajili ya biashara na kuivuna hapo baadaye ILI kuifanya ardhi yangu isibakie idle katika kipindi hiki cha mpito. Nawaomba wajuzi wanisaidie yafuatayo :-

1. Aina ya miti nitayoipanda ambayo hatachakaza ardhi

2. Aina ya miti nitayoipanda ambayo ninaweza kuivuna katika kipindi tajwa hapo juu

3. Tahadhari au mambo ya kuzingatia katika huu mradi.

4. Nitafurahi pia kupokea critics iwapo nimewaza vibaya

5. Lolote lile la kujenga litapokelewa kwa moyo wa unyekevu

Ahsante
 
Kuna search humu ndani kuna taarifa za kutosha kuhusu miti.
Au nenda morogoro kwa wakala wa mbegu za miti kwa msaada zaidi.
 
Mkuu,

issue ya nyani inasumbua hata siku za mwanzo utakapootesha miti. Inabidi ulinde mwanzoni ili hawa binamu zetu wasing`oe miche na kuitupa. Hii ni tahadhari.

Tuje kwenye hoja. Ni wazo zuri, pili umesema vema kuangalia mti ambao hautachakaza ardhi yako kama mlingoti, huu mlingoti usioteshe kama una mpango wa kuja kulima tena hilo shamba.

Sijui ni pwani ya wapi, ila jaribu kuotesha mwarobaini (utavuna haraka kama mbao), mlonge (utavuna kama dawa ukipata soko au chakula cha mifugo), acrocarpus (fast growing, utavuna kama mbao), mianzi (ujenzi na mapambo),mitiki (utavuna kama nguzo na mbao), meria azarachy(fast growing, kwa mbao nyeupe), miembe (matunda na mbao), mikorosho(korosho na mkaa). Mivinje /mitiki ni long term investment.

karibu tena.
 
Habari Mkuu,

Ubarikiwe sana kwa maelezo yako yaliyoshiba. Nashukuru pia kwa ushauri mzuri na tahadhari ulizotupatia. Nina amini kuna wengi zaidi yangu watakaonufaika na maelezo yako.

Karibu mkuu

Back
Top Bottom