Hao nguruwe pori hawaliwi mkuu?
Chilumbile Nungu cha kumemena. Watakuja wenye dini zao waharibu uzi bure, miye simo.
Hao nguruwe pori hawaliwi mkuu?
Jamani nisaidieni, nimelima mhogo huko kisarawe lakini naona umeingiliwa na ugonjwa wa kuoza. Ukivuna mihogo unakuta kama imepikwa vile. Huu ni ugonjwa gani na una dawa?Fuata kalenda ya mvua za pwani, kuna vuli na masika. Sema siku hizi mvua na zenyewe hazieleweki kama zamani. Vuli ya zamani ilikuwa kt ya sept na nov na kisha masika ni march. Hiki kipindi cha vuli ndio kizuri kuotesha mhogo, kulingana na wenyeji wangu wanavyofanya. Sijui kama kuna kilimo cha umwagiliaji kwa zao la mhogo !!!!!!! Ikibidi tutaanzisha kilimo cha umwagiliaji mhogo, cheze sayansi weeeee.
Chukua mihogo yako iliyoathirika, peleka pale Kibaha idara ya kilimo, watakwambia ni ugonjwa gani, pengine wakakupa na wazo la kubadirisha mbegu au njia nyingine mbadala.Ndugu hata mi imenikuta,nililima maeneo ya madafu mlandizi,heka 5 zote zimeteketea!! natamani tena kurudi kwenye kilimo cha mihogo ila sijapata taarifa za kutosha tena ili nikajaribu kwingine.
Nenda Kibaha regional block, uliza idara ya kilimo, wape sample ya mihogo iliyoathirika, watakupa jibu.Jamani nisaidieni, nimelima mhogo huko kisarawe lakini naona umeingiliwa na ugonjwa wa kuoza. Ukivuna mihogo unakuta kama imepikwa vile. Huu ni ugonjwa gani na una dawa?
<br />
<br />
Ni miezi 7 tu itakuwa tyr kuvunwa mkuu!
Nashukuru kwa ushauri ndugu yangu. Nitafanya hivo.Chukua mihogo yako iliyoathirika, peleka pale Kibaha idara ya kilimo, watakwambia ni ugonjwa gani, pengine wakakupa na wazo la kubadirisha mbegu au njia nyingine mbadala.
Wow nimeupenda sana ushauri wako kwa jamaa mkuu, na Mungu akubarikiMkuu huko sokoni ulikokwenda kutafiti soko uliulizia aina za mihogo zinazopapatikiwa na walaji? Ulishaulizia misimu na bei zake? Huko sokoni uliulizia mambo yanayoangusha bei ya mihogo sokoni? Uliulizia ufungashaji na hifadhi yake? Je uuzaji upi utakulipa kwa kutumia dalali au kuuzia wauzaji moja kwa moja?
Huko shambani nako umeshakutana na wakulima kujua changamoto zinazowakabili kwenye kilimo hiki? mbegu inayofaa? changamoto wanazokutana nazo sokoni? changamoto za shambani? n.k.
Nimekuuliza hivi ili taratibu uanze kutafuta majibu mwenyewe wakati tukisubiri huenda akatokea mzoefu kueleza ulichoomba msaada. Hadi sasa ni kimya na wakati mwingine ndiyo imetoka hivyo! Dondoo ninayokupa ni kwamba usije ukabeba mbegu yako unayoipenda toka kwenu Kigoma au Mbamba bay ukaingia nayo kichwa kichwa kwenda kuipanda Kisarawe at large scale !!! Utakuja lia. Tabia ya mihogo inabadilika kutegemea na aina ya udongo. Muhogo mtamu eneo fulani unaweza kuwa mchungu eneo lingine na vice versa, ndiyo maana kuna wakazi wa mkoa mmoja Tz ukiwatajia kula mihogo wanatetemeka kwamba kwao ni sumu.
Nilishaandika hapa jukwaani JF kuna jamaa yangu alileta za kuleta kachukua mbegu yake maarufu toka kwao huko bara akaipanda Mikese, mihogo ilistawi hakuna mfano kasheshe ni pale alipokwenda mnunuzi shambani ikawa kila shina alilong'oa mhogo ukivunjwa ndani yake kuna kama ringi ya mizizi ekari tatu chali! Mfanya biashara alimpa pole kwamba next time abadili mbegu. Mbegu utakayotumia utaipata huko huko Kisarawe na iwapo utaenda na mbegu yako mpya anza nayo eneo dogo kwanza uione vitu vyake ili usijewafikiria vibaya majirani zako kwamba wamekufanyizia. Mihogo iko hivyo. Wishing you success !!
Nakushauri tu kama unampango wa kulima muhogo we lima tena wakutosha. kuna mradi unaanzishwa huko rufiji unaitwa frederic and jocelyne african starch development ndio umeanza sasa wameshapata ardhi ya kulimia muhogo kwa wingi. pia kitajengwa kiwanda kikubwa sana kwaajili ya kuzalisha starch kwa wingi.Habari wana jamvi natumai mu wazima wa afya,nina mpango wa kuanzisha kilimo cha mihogo k'sarawe na kuleta Dar kwa ajili ya kuuza.Nishafanya utafiti mdogo naweza kupata shamba la kuazima kwa bei nafuu na pia sehemu za kuuzia kwa hapa Dar pia zipo.Je kuna yeyote mwenye uzoefu na shughuli hiyo anisaidie kwa ushauri ili nijue changamoto zake.
Natanguliza shukrani zenu.
Halafu zaidi ya yote Kubota, kuna vyuo vya kilimo vimefanya na vinaendelea kufanya utafit juu ya masuala haya ya kilimo; hivyo basi ni vizuri kuwaona kama mtu anataka kufanya vitu seriously na kwa uhakika. Pia humu JF kuna nyuzi nyingi juu ya kilimoa cha mhogo ni vizuri majid musisi ukazipitia kwa faida ya muda mrefu. Kila la heri.
What about fukayosi mkuu? Mhogo unaota?
Mkuu naanza ujenzi wa kiwanda cha kusindika Rufiji kuanzia Sept na by Jan 2012 nitaanza kununua tani 20 kila siku mihogo aina zote so kama utakuwa na uwezo wa kufikisha tutanunua yote. Michungu na mitamu yote tutachukua kutengezea starch tuna masoko ya nje makubwa na tutanunua bei nzuri tu mkuu.
Maelezo mengi zaidi yapo hapa mkuu
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/39210-project-funding-sources-10.html#post2118391
Mkuu na mimi nina vi ekari vyangu kadhaa huko. Nawaza nilime mihogo mitamu au mananasi? Vipi wewe umefikia hatua yoyote nzuri Kwa sasa?
Asante sana mama Joe,Vipi Kwa upande wa kipato kati ya mihogo na mananasi, ipi inalipa zaidi?Mimi sio mjuzi sana ila mihogo niliilima kidogo haina gharama upate mbegu nzuri kibaha mimi walinipandia ya kawaida ila sikukosa cha kuvuna,. Huitaji ,mbolea. Nanasi wanalima wenzangu kiwangwa muda huu wanapanda hasa hizi mvua inahitaji mbolea kukuzia, palizi etc kwa eka moja gharama yaweza fika laki 8 sina uhakika. Uamuzi ni wako.
Inalipa nanasi lakini pia inahitaji capital kubwa, kitu kingine nilichoona kwa vile ni plantations wanatumia mbolea za viwandani zaidi maana kupata za organic ni ngumu. Hivyo ardhi kwa kilimo hiki inabidi ukibadili mawazo uendelee na mbolea hizi ingawa sina hakika.Asante sana mama Joe,Vipi Kwa upande wa kipato kati ya mihogo na mananasi, ipi inalipa zaidi?
Asante sana mama Joe Kwa hizi info. Ngoja niutafute huo Uzi niusome.Inalipa nanasi lakini pia inahitaji capital kubwa, kitu kingine nilichoona kwa vile ni plantations wanatumia mbolea za viwandani zaidi maana kupata za organic ni ngumu. Hivyo ardhi kwa kilimo hiki inabidi ukibadili mawazo uendelee na mbolea hizi ingawa sina hakika. Kuna uzi humu ulielezea mbegu upandaji na faida kwa eka kwa kilimo cha nanasi hebu google utauona tu. Fukayosi sijaingia ndani ila kama udongo unafanana na wa Kiwangwa utafaa tu.