Kilimo cha Mihogo (Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

Tuwe wakweli ndugu hayo mahesabu uliopiga hapo hayawezekani, mimi nina udhoefu na kilimo cha muhogo, isitoshe mimi mwenyewe nina shamba hukohuko Bungu.

Kusafisha shamba kwasasa ni 50,000 kwa heka, kumbuka shamba ppri lina hatua tatu za kusafisha 1. Kuvunja msitu, 2. Kukusanya mara ya kwanza, kukusanya mara ya pili baada ya kuchoma moto.
3.kungoa visiki alafu na kuchoma moto tena au kutolewa nje ya shamba, mwisho ndio kulima.

jambo jingine ni kuhusu mbegu ya muhogo kweli fungu ni 3000 lakini heka moja inaweza kuchukua mafungu hata zaidi ya kumi.

Ghalama nyingine za ziada ni kudhibiti panya na nguruwe huku swala hili limekuwa tatizo kubwa sana maana labda uweke wigo au mfanye ulinzi nyakati za usiku, fikiria muhogo unaotakiwa uwe mzito zaidi utakaa shambani kwa muda gani?.

Mwisho wa yote bei iliokuwa inatolewa hapa ni 50 -100 @ kilo na wanataka upeleke muhogo uliomenywa baganda na bado gharama ya kuusafirisha kupeleka kiwandani.

hapo sijataja gharama za palizi kwahuku palizi kwa msimu mmoja tunafanya hata mara nne kutokana na nyasi na rutuba ya udongo, bado gharama za watu watakaovuna pia.

But kila lakheri.

Mkuu
Mzuzu, tunaomba ufafanuzi juu ya hili ili tuwe comfortable.
 
Kwa hiyo mkuu inawezekana mkamkodisha mtu vifaa (bulldozer) vya kusafishia shamba na tractor ya kulimia then mkamkata kwenye malipo? That's a kind of a soft loan kama ni hivyo huo mpango mtauanza sasa hivi au awamu nyingine? Nijibu tafadhali hii itasaidia sana interested wakulima hasa wadogo kumake decision kuanza na awamu ipi
Yes inawezekana mkuu na tutafanya lakini sio kwa awamu hii. Hatuna kiasi cha kutosha cha fedha kwa hiyo tunataka watu watakaoweza kufanya sehemu kubwa ya shughuli kwa awamu hii.

Kwa upungufu wa fedha tunataka kufanya mambo ya kimsingi tu au major issues kama kuhakikisha kiwanda kinajengwa na kuanza, kulima sehemu kiasi, kununua mashine za kimsingi kama matrekta, planter na harvester ili kuhakikisha soko linakuwepo by next year tusijakufrustrate wadau then tutaongeza huduma zaidi baada ya hapo. Kwa sasa tusaidiane
 
mkuu Mzuzu

naomba kujua kuhusu output product yaani starch ya muhogo huu mnaotarajia ku-process . Je, wajasiriamali wadogo wadogo wanaweza kuitumiaje starch ya muhogo mtakaotengeneza kama raw material na kuweza kuprocess by products gani zitakazotumika locally ?

Tutatengeneza industrial starch sidhani km wajasiriamali wadogo itawafaa, labda kwa kupigia pasi na sijui vingine maana hii inatumika zaidi kwenye viwanda vikubwa kama vya nguo, karatasi, chipboards, bio-plastics, ketchups, gypsum boards nk.
 
Mkuu Mzuzu, aksante sana kwa maelezo ambayo kimsingi yalikuwa ndiyo maswali yangu. Nimemaliza kupiga hesabu za magazijuto hapa na kugundua mkiunga nguvu watu kumi na kuchukuwa ekari 50, kwa gharama ulizotaja at most kila memba atachangia T shs. 1,750,000/= INAWEZEKANA.
Tatizo langu linabaki kwenye bei ya kununulia naona ipo chini au inajadilika?

Bei ya muhogo itategemeana sana na soko la starch la kimataifa so itakuwa inabadilika na pia tutakuwa tunakaa na wadau kuona na kuset bei tutakayotumia kwa mwaka mzima. Tunaweka kwa dola ili wadau wapate stability kwenye planning na kuweza kupredict kama italipa kabla hatujasign contract na kuengage kwenye biashara

Hata hiyo bei hiyo kwa sasa bado ina return nzuri tu ya zaidi ya 100% yani pesa utakayoinvest inaweza kurudi na faida ikwa zaidi ya mtaji! Na tena itakuja kuwa affected sana na amount ya muhogo utakaolimwa kwa sasa huwezi kujua kwa kuwa hamna uzalishaji wowote hapa wa kuweza kulisha kiwanda.
 
Tuwe wakweli ndugu hayo mahesabu uliopiga hapo hayawezekani, mimi nina uzoefu na kilimo cha muhogo, isitoshe mimi mwenyewe nina shamba hukohuko Bungu.

Kusafisha shamba kwasasa ni 50,000 kwa heka, kumbuka shamba opri lina hatua tatu za kusafisha
1. Kuvunja msitu,
2. Kukusanya mara ya kwanza, kukusanya mara ya pili baada ya kuchoma moto.
3. kungoa visiki alafu na kuchoma moto tena au kutolewa nje ya shamba, mwisho ndio kulima.

jambo jingine ni kuhusu mbegu ya muhogo kweli fungu ni 3000 lakini heka moja inaweza kuchukua mafungu hata zaidi ya kumi.

Gharama nyingine za ziada ni kudhibiti panya na nguruwe huku swala hili limekuwa tatizo kubwa sana maana labda uweke wigo au mfanye ulinzi nyakati za usiku, fikiria muhogo unaotakiwa uwe mzito zaidi utakaa shambani kwa muda gani?.

Mwisho wa yote bei iliokuwa inatolewa hapa ni 50 -100 @ kilo na wanataka upeleke muhogo uliomenywa maganda na bado gharama ya kuusafirisha kupeleka kiwandani.

hapo sijataja gharama za palizi kwahuku palizi kwa msimu mmoja tunafanya hata mara nne kutokana na nyasi na rutuba ya udongo, bado gharama za watu watakaovuna pia.

But kila lakheri.
Nakubaliana na wewe mkuu lakini estimates nilizotoa ni tulizotumia kufanya hii project na tume maximize km ukiangalia umeongelea shamba pori stage zote 3 za 50,000 sisi tumeweka mara 4 kucover zote. Then tunaplan kutumia buldozer ambalo hizo stages zitakuwa 1 na kusafisha ya pili.

Tunafanya kazi hii na kituo cha utafiti cha muhogo ARI Kibaha so mambo yote ya kiufundi tutakuwa nao usiwe na shaka sana na pia tunaanza so tunategemea challenges na tutazikabili. Kumbuka huu ndio utakuwa mradi mkubwa wa muhogo wa kwanza.

Mbegu pia guidance ni kutoka ARI na pia kuhusu nguruwe tunajua na tunafikiria kutumia mbegu za mihogo michungu haya ni ya kitaalamu na yanafanyiwa kazi. Michungu hamna mdudu wala nguruwe anashambulia kwa vile iliyopo ni sumu na wanajua.

Gharama zingine kama palizi nk zipo included kwenye estimates hapo kumbuka wewe unafanya in low scale tena kwa jembe la mkono haiwezi kuwa na tija kama tutakapofanya na mashine kwa sehemu kubwa tena manpower ni shida Rufiji najua so ni kujipanga ili kupunguza kutegemea jembe la mkono.

Plan yetu ina mpango wa kujenga logistic system ili kurahisisha usafirishaji kwa gharama zetu. Kwa kuanzia matrecta yote yatafanya usafirishaji pia baadaye tutafanya cost sharing lakini sasa hilo ni letu na pia sisi hatutahitaji umenye muhogo. Vuna shambani pakia then unafika kiwandani tunapima uzito na quality unalipwa cheque yako unaondoka!
 
Mzuzu pole na kazi.Nimechelewa kuona mpango huu,je twaweza kurusha application yetu?
 
Mzuzu,niko interested na hiyo project;naona kama inatalipa vizuri kwa siku za baadaye kuliko sasa/mwanzoni.Nafikiri kuwekeza kiasi changu in terms of cash na mawazo;ila ninaona kama itakuwa nzuri kufanya hivyo kwa umoja ni nguvu kuliko utengano ni dhaifu.

Hebu nitajaribu ku-team up na wanaJF wenzangu ambao wako tayari kuwekeza katika hii project. Good move keep it up,and make it happen.
 
Habari wana jamvi natumai mu wazima wa afya,nina mpango wa kuanzisha kilimo cha mihogo k'sarawe na kuleta Dar kwa ajili ya kuuza.Nishafanya utafiti mdogo naweza kupata shamba la kuazima kwa bei nafuu na pia sehemu za kuuzia kwa hapa Dar pia zipo.Je kuna yeyote mwenye uzoefu na shughuli hiyo anisaidie kwa ushauri ili nijue changamoto zake.

Natanguliza shukrani zenu.
 
H.jpg

Roots and Tuber Crops Research Programmer.​

  1. Is one among the programs in the Ministry of Agriculture and has the National mandate of conducting research on cassava sweet potato and yams. This program seek to develop improved varieties tolerant to diseases and pests and high yielding Naliendele Agricultural Research Institute (NARI) is involved in the Co- ordination of the program whose lead scientist is the National.

  1. ACTIVITIES Co – ordinator for the program.

        1. Breeding of high yielding varieties pest and disease tolerant varieties of sweet cassava and yams.
        2. Gerurplasim collection maintenance and screening of pest and disease tolerant genotypes.
        3. Multiplication and dissemination of improved varieties to farmers.
        4. demonstrating cassava processing technologies using motorized chippers and grater and dewatering machine to extension staff farmers private
Major areas of Research (Cassava).

  1. To develop high yielding varieties.
  2. To identify insects disease of cassava in southern zone
  3. To develop/address Agronomy practices of cassava
  4. To multiply and disseminate improved varieties and techuics which we have developed.

Staffing.
The staff disposition in the Roots and Tuber crops in the Southern zone is made up of the following.
Researchers.

  1. Dr. G.S.Mkamilo - Program Lead Scientist National Co –ordinator PHD holder.
  2. Mr. Aloyce Kundy - Agricultural Research Officer BSC.
  3. Mr. Davis F. Mwakanyamale - Agricultural Research Officer BSC.
  4. Mr. Athanas J.Minja - Agricultural Research Officer BSC
  5. Mr. Njapuka Abdallah - Principal Agricultural Officer.
  6. Mr. Divasi Gambo - AFO
  7. Mr. Muhsin Abdul - Driver.

Wenye majibu ya swali lako ndio hawa, website yao ilivyo mbovu inaonekana kama ni taasisi ya kutafuna fedha za serikali. Jaribu kuwasiliana na Dr G S Mkamilo kwa email yao labda atakuwa na msaada.

Naliendele Agriculture Research Institute
 
Wakuu nilipotea kitambo chimbo kukamilisha documentation za kazi hii zinazohusu mazingira na za kisheria na sasa tupo tayari kuanza rasmi mradi huu. Tunataka wakulima sasa kwa ajili ya kuwapa contracts kwa lengo la kulima muhogo kwa ajili ya kiwanda tuachokijenga kule Rufiji.

Kufikia Sept 2013 tutakuwa tayari kununua muhogo tani 60 kwa siku kwa hiyo anayeweza kufanya sasa hajachelewa sana na inawezekana pia kufanya umwagiliaji kwa kuchimba visima vichache. Muhogo hauhitaji maji mengi na ardhi ya Rufiji ina unyevu wa kutosha kilimo mwaka mzima. Kifupi ni kwamba wanalima muhogo mara mbili kwa mwaka.

Karibuni sana na ofisi yetu sasa ipo EPZ Mabibo external.
 
Tunashukuru kwa taarifa mkuu vp tunaweza kuja kukuona ofisini? Tulishatuma EOI vp mtazijibu?
 
Wakuu nilipotea kitambo chimbo kukamilisha documentation za kazi hii zinazohusu mazingira na za kisheria na sasa tupo tayari kuanza rasmi mradi huu. Tunataka wakulima sasa kwa ajili ya kuwapa contracts kwa lengo la kulima muhogo kwa ajili ya kiwanda tuachokijenga kule Rufiji.

Kufikia Sept 2013 tutakuwa tayari kununua muhogo tani 60 kwa siku kwa hiyo anayeweza kufanya sasa hajachelewa sana na inawezekana pia kufanya umwagiliaji kwa kuchimba visima vichache. Muhogo hauhitaji maji mengi na ardhi ya Rufiji ina unyevu wa kutosha kilimo mwaka mzima. Kifupi ni kwamba wanalima muhogo mara mbili kwa mwaka.

Karibuni sana na ofisi yetu sasa ipo EPZ Mabibo external.

Shukrani sana mkuu

Na sisi pia tumekua busy na lega team kuangalia namna kuwekana sawa hasa kwenye masuala ya kulipana kwa haki na timely maana hizi monopolies huwa zinasumbua.
 
Kididimo iko Mkuranga,mara baada ya kupita kijiji cha Mbezi njia ya kisiju kabla ya kufika Mpafu, panalimwa sana tikiti. Nikipata bei yake nitaiweka peupe mkuu. Maji ya kubangaiza yapo.

Ukanda wa pwani una nyani balaa,nguruwe pori ni wengi sana. Tusikate tamaa.
Mkuu maeneo haya ya mkuranga. Kilimo cha mihogo msimu mzuri wa kupanda ni miezi gani?
 
mkuu maeneo haya ya mkuranga..kilimo cha mihogo msimu mzuri wa kupanda ni miezi gani?

Fuata kalenda ya mvua za pwani, kuna vuli na masika. Sema siku hizi mvua na zenyewe hazieleweki kama zamani. Vuli ya zamani ilikuwa kt ya sept na nov na kisha masika ni march. Hiki kipindi cha vuli ndio kizuri kuotesha mhogo, kulingana na wenyeji wangu wanavyofanya.

Sijui kama kuna kilimo cha umwagiliaji kwa zao la mhogo! Ikibidi tutaanzisha kilimo cha umwagiliaji mhogo, cheze sayansi weeeee.
 
Kididimo iko Mkuranga,mara baada ya kupita kijiji cha Mbezi njia ya kisiju kabla ya kufika Mpafu, panalimwa sana tikiti. Nikipata bei yake nitaiweka peupe mkuu. Maji ya kubangaiza yapo.

Ukanda wa pwani una nyani balaa,nguruwe pori ni wengi sana. Tusikate tamaa.
Hao nguruwe pori hawaliwi mkuu?
 
Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom