Kilimo cha Mihogo(Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake | Page 18 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilimo cha Mihogo(Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by JamiiForums, Aug 7, 2011.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,104
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Wakuu,
  Kutokana na uhitaji wa kuwepo mjadala endelevu na wa tija kwa wajasiriamali, tumeona ni vema tukaweka hii thread kwa maslahi ya wengi.
  Tunashauri Mjadala huu ujikitae kwenye maeneo yafuatayo:

  1. Aina za mihogo na maeneo inakostawi vizuri
  2. Misimu ambayo mihogo inapandwa ni miezi ipi? Inaweza kupandwa misimu yote ya mwaka?
  3. Mihogo inashambuliwa na magonjwa yapi? Zipi mbinu za kukabiliana na maradhi hayo?
  4. Mihogo inachukua muda gani tangu kupandwa hadi kuvunwa?
  5. Hekari moja inaweza kutoa magunia mangapi ya mihogo?
  6. Masoko ya mihogo na bidhaa zake ndani na nje ya nchi yapoje?
  Asante

  ===============================================
  Michango ya wadau mbalimbali kuhusu kilimo cha mihogo
  =============================================
   
 2. l

  luqman16msuya New Member

  #341
  Apr 28, 2018
  Joined: Apr 27, 2018
  Messages: 3
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Sasa kama bei ya china ni 300 kwa kilo.. Unatarajia kuuza sh ngap kwa kilo.?
   
 3. p

  prim cleverley New Member

  #342
  May 12, 2018
  Joined: May 12, 2018
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Daaah aya maeelezo yamenitia hamsha hamsha yakujarbu kufanya I appreciate the knowledge
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #343
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  Kilimo bora cha Mihogo - MUUNGWANA BLOG

  Kilimo bora cha Mihogo

  Muungwana Blog Monday, February 20, 2017 Kilimo  [​IMG]
  Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani.

  Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

  TEKNOLOJIA ZILIZOPO
  Mbegu bora za muhogo
  Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
  Naliendele Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

  Kiroba
  Huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9toka ipandwe.

  Mbinu bora za kilimo cha muhogo

  Uandaaji wa shamba
  Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
  - Kufyeka shamba
  - Kung’a na kuchoma visiki
  - Kulima na kutengeneza matuta
  · Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
  Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.
  · Upanadaji

  Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
  - Kulaza ardhini (Horizontal)
  - Kusimamisha wima (Vertcal)
  - Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

  Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
  Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

  Nafasi ya kupanda:
  Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.

  [​IMG]
  Palizi:
  - Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
  - Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
  - Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
  - Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

  Uvunaji:
  Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

  Usindikaji bora
  Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
  - Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
  - Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
  - Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

  Njia bora za usindikaji
  - Kwa kutumia mashine aina ya Grater
  Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
  - Kwa kutumia mashine aina ya chipper
  - Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

  Matumizi ya Muhogo
  - Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
  - Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
  - Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.

  iii MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
  · Magonjwa
  Kuna magonjwa mawili ambayo ni muhimu sana na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.
  a) Ugonjwa wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawia
  katika muhogo
  Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye miinuko iliyo na urefu chini ya mita 300 na unapatikana kidogo sana kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei kabisa.

  Visababishi:
  Matokeo ya uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ugonjwa huu ulienezwa na mdudu mweuupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.

  Dalili za Ugonjwa
  Sehemui zote za muhogo zinaweza kuonyesha dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa kulinganisha.

  Kwenye majani
  Dalili ya kwanza: Chlorosis rangi ya njani hutokea kwanza pembezoni mwa vena ndogo baadae huathtiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa (chlorosis) la rangi ya njano.
  Dalili ya pili: Rangi ya njano ambayo haihusishwi vizuri na vena isipokuwa katika mbaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa ya lamin inaweza isiathirike, majni yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.

  Kwenye shina
  Huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani, jeraha la zambarau au kahawia linweza kuoneakan nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baaada ya kubandua gome la nje. Pia jeraha la nekrotiki kwenye kovu la shina hutokea baada ya majni kudondoka kutokana na umri wa mmea. Tawi/shina hufa kuanzia kwenye nch kuelekea chini na kusababisha kufa kwa mmea wote.

  Kwenye mizizi
  Kwa kawaida hutokea baada ya dalili za majani na wakati wa kipindi kati ya uambukizo na kufa, amabpo kifo cha mizizi hutokea kuanzia miezi 5 toka kupandwa. Dalili za mizizi zinabadilika nje ya mizizi na zinaweza kuwa kamakizuizimwanga au shimo au kufa kwenye gome.

  Tishu inayo zunguka mshins ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi. Wakati mwingine mizizi huonekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa, lakini ikikatwa huonekana kufainakufa au rangi ya njano.

  [​IMG]
  Uambukizaji na ueneaji
  Ugonjwa wa CBSD unaambukizwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimea iliyoathiriwa vinavyosababisha mmea kuonesha kwenye majani dalili za ugonjwa.
  Kwa kuwa muhogo kwa kawaida huzalishwa kwa njia ya vipandikizi ugonjwa huu huingizwa kwenye sehemu mpya zilizopandwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa.
  Kwa aina zinazovumilia sana kwenye hali za mabondeni, dalili mbaya sanahutokea wakati ugonjwa ukigundulika katika hatua za mwanzo.
  Uchunguzi umeonesha kwamba Bemisia afer ni mdudu/kisababishi ambacho ndicho kinachohusiana na maendeleo ya hivi karibuni kuhusu uhamishaji wa visababishi kama “ipomovirus”. Mara nyingine inaonesha nzi weupe (White flies) na kutokana na hali hiyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.

  Udhibiti/Kuzuia
  ü Njia ya msingi ya kuzuia/kudhibiti ugonjwa wa CBSD ni kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea isiyo na dalili ya ugonjwa.
  ü Ubora wa mashina unahitaji kutunzwa kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza ile iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.
  ü Hakikisha kuwa unapanda mbegu bora za mhogo ambazo zinastahimili uambukizo wa magonjwa.
  ü Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mhogo ichome moto ili kutokomeza ugonjwa huo.
  ü Kuelewa dalili za ugonjwa wa CBSD kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.
  ü Hakikisha kuwa unaendelea kutunza mbegu bora zinazoonekana kuvumilia magonjwa sana.
  ü Hakikisha kuwa shamba la mhogo linakuwa safi kwa ajili ya kupunguza visababishi vya ugonjwa wa CBSD

  b) Ugonjwa wa batobato au ukoma wa majani
  Ni ugonjwa ambao ulienezwa kwamara ya kwanza hapa Tanzani mwaka 1894, na baadae uliripotiwa katika nchi nyingine nyingi za Afrika Mashriki, Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na sasa unafahamika kuwa upo maeneo yote yanayolimwa muhogo Afrika.

  Katika viwango vya kuwepo kwa ugonjwa wa CMD na katika uwingi wa hasara zinazopatikana kutokana na CMD ni kati ya 15% – 20%. Hii ni sawa na tani milioni 15 – 18 zikilinganishwa na makadirio ya shirika la kilimo na chakula duniani ya tani milioni 85 ya mwaka 1997.

  Visababishi
  Tangu ugonjwa wa CMD ulipoenezwa kwa mara ya kwanza, visababishi vilichukuliwa kuwa ni virusi kwa sababu ya kukosekana kisababishi kingine. Kwa hiyo kutokana na kuwa mtazamo huu unalingana na matokeo ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba ugonjwa huu huenezwa na nzi mweupe (white fly).

  Pia uchunguzi wa mara kwa mara umesababisha utambuzi wa virusi vya aina mbalimbali na tofauti kama ifuatavyo:
  · Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Africa cassava mosaic virus
  · Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Afrika mashariki (East Africa cassava mosaic virus)
  · Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya India (Indian cassava mosaic virus)

  [​IMG]
  Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)

  • Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri
  • Sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za
  • Awali za ukuaji wa jani.
  • Sehemu za kloritiki hushindwa kutanuka hadi mwisho, hivyo mvutano unaji-
  • okeza kutokana na ukuaji usiolingana na jani au majani madogo yaliyoharibika
  • Majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa
  • Sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
  • Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.
  • Kloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe
  • yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.

  [​IMG]
  Uambukizaji na uenezaji
  Ukoma wa mhogo huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida
  hutumika kuzalishia mmea.
  Pia huenezwa na inzi mweupe (white fly) aitwae Bemisia tabaci G. Aina mbili za inzi au
  Mbu hao Bemisia (Preisner Hhosny na Aleorodius disperses R) pia huambukiza mihogo
  katika nchi za Afrika na India
  Usambazaji wa vipandikizi unaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa CMD katika
  Maeneo mapya.
  UHIBITI NA KUZUIA

  • -Hatua ya msingi ya kuzuia ugonjwa wa CMD ni kwa kuchagua vipandikizi kutoka kwa
  • Mmea ambao hauna uambukizo wowote.
  • -Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile
  • Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua
  • -Hakikisha kuwa wakati wa kuvuna mihogo kwa ile iliyoathirika na ugonjwa wa CMD
  • inaangamizwa kwa kuchomwa moto.
  • -Hakikisha kuwa unatunza shamba na kuwa safi ili kupunguza wadudu waenezao CMD.
  • -Hakikisha una elimu ya kutosha juu ya dalili za ugonjwa wa CMD>

  WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU

  [​IMG]
  Cassava Mealy Bug (CMB)
  Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.
  [​IMG]
  Cassava Green Mites (CGM)
  Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.

  [​IMG]
  White Scales
  Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.

  Mchwa
  Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
  Wanyama waharibifu
  Hawa hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k

  Udhibiti/Kuzuia
  Kwa upande wa wadudu wanweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:
  ü Kutumia dawa za kuulia wadudu
  ü Kutumia wadudu marafiki wa wakulima
  Kwa upande wa wanyama ni kuweka walinzi.
   
 5. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #344
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  KILIMO CHA MIHOGO ~ JIKWAMUE KIUCHUMI

  KILIMO CHA MIHOGO  [​IMG]

  Zao la muhogo ni muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo na wenye kipato cha chini.Wakulima walio wengi huwa wanachanga zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde,mbaazi na njugumawe n.k.
  Muhogo hustawi zaidi katika maeneo yalipo kwenye mita 0 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari.Pia katika maeneo yanayopata mvua za wastani wa 750mm mpaka 1200mm.Muhogo ushamiri zaidi katika udogo wa kichanga na ustahimili hali ya ukame.Mikoa kama Lindi,Pwani,Tanga,Mwanza,Kigoma,Ruvuma,Morogoro,Mbeya na Shinyanga huwa kilimo cha mihogo kinakubali zaidi.
  MBEGU BORA YA MUHOGO
  Kutokana na wataalamu kuna aina mbili za mbegu ya muhogo ambazo zimethibitishwa na wakulima kama vile:
  (i)Naliendele; hizi ni mbegu ambazon mkulima akizitumia basi anakuwa na uhakika wa kupata tani 19 kwa hekta moja na inaweza kuvunwa kuanzia miezi tisa (9) toka ipandwe.
  (ii)Kiroba; huzaa tani 25 mpaka 30 kwa hekta moja na pia inavunwa kuanzia miezi tisa (9) toka ipandwe shambani.
  Mbegu hizi zinapatikana katika sehemu zifuatzo;
  Agriculture Research Institute Naliendele-Mtwara
  Agriculture Research Institute Tengeru-Arusha
  Agriculture Research Institute Kizimbani-Unguja
  Agriculture Research Institute Uyole-Mbeya
  Agriculture Research Institute Maruku-Kagera
  Agriculture Research Institute Ukiriguru-Mwanza
  Mbegu zinatakiwa zisiwe na magonjwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamekomaa vizuri.
  NAMNA YA UPANDAJI WA MBEGU ZA MUHOGO KATIKA SHAMBA
  Kuna njia tatu ambazo zimezoeleka sna katika kupanda mbegu ya muhogo shambani ambazo ni
  (i)Njia ya kulaza ardhini
  (ii)Kusimamisha wima
  (iii)Na njia ya kuinamisha (Inclined/Slunted)
  NB: Unashauriwa urefu wa kipande cha shina uwe 30cm na pia unategemea sna idadi ya macho yaliyopo kwenye kipande ni vema kipende kiwe na macho 4 mpaka 6.
  Palizi ya kwanza inatakiwa kufanyika mapema kwenye mwezi wa kwanza baada tu ya kupanda ili kuzuia magugu yanayochipia haraka bahada ya mvua kunyesha. Na pia ndani ya miezi minne ya mwazo mihogo haitajiki kuwa na magugu ili kuepuka ushindani ya mahitaji maalumu kati ya muhogo na magugu.
  MAGONJWA YANAYOSUMBUA ZAO LA MUHOGO SHAMBANI
  Kuna magonjwa mawili ambayo yanasababisha kupunguza uzalishaji wa zao la muhogo shambani.
  (a)Ugonjwa wa matekenya/ michirizi ya kahawa katika muhogo.
  Huu ni ugonjwa ambao unapatika katika sehemu za miinuko iliyo na urefu chini ya mita 300 na unapatika katika sehemu ndgo katika maeneo ya miinuko ya mita 500.Ugonjwa huu unaenezwa na mdudu mweupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.
  Dalili za ugonjwa kwenye mmea wa muhogo.
  Hapa tutaangalia katika sehemu tatu za mmea wa muhogo
  (i)Katika majani
  Dalili ya kwanza:hutokea rangi ya njano pembezoni mwa vena ndogo baadae huathiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa la rangi ya njano.
  Dalili ya pili:rangi ya njano ambayo haihisishwi vizuri na vena isipokuwa katika mabaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa lamin inaweza isiathirike,majani yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.
  (ii)Kwenye shina
  Ugonjwa huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani lakini jeraha la zambarau au kahawia linawweza kuonekana nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baada ya kubandua gome la nje.
  (iii)Kwenye mizizi
  Kifo cha mzizi hutokea kuanzia miezi mitano toka kupandwa,dalili za mizizi huonekana kubadili nje ya mizizi na zinaweza kuwa kama kizuizi mwanga au shimo au kufa kwenye gome.Tishu inayozunguka mashina ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi,wakati mwingine mizizi huonenekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa,lakini ikikatwa huonekana kufa.Ugonjwa huu uenezwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimema iliyoathiriwa.
  (b)Ugonjwa wa batobato/ukoma wa majani
  Ugonjwa huu ulienea Tanzania kataka miaka ya 1894 na kuripotiwa katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.Ugonjwa huu usababishwa na inzi mweupe lakini uchunguzi wa mara kwa mara umetambua kuwepo kwa virusi vya aina mbalimbali kama vile; Afrika cassava mosaic virus na Indian cassava masaic virus.
  Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)
  -Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.Piakloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.
  Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za awali za ukuaji wa jani.
  Pia majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
  Ugonjwa huu huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida hutumika kuzalishia mmea.
  [​IMG]
  ukoma wa majani
  JINSI YA KUDHIBITI MAGONJWA HAYA SHAMBANI MWAKAO
  -Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mihogo unatakiwa kuchoma moto ili kutokomeza ugonjwa huo
  -Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua
  -Pia unahitajika kuelewa dalili za magonjwa kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.
  WADUDU WAHARIBIFU KATIKA MIHOGO

  Cassava Mealy Bug (CMB)
  Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.
  [​IMG]
  – White Scales
  Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.
  [​IMG]
  – Cassava Green Mites (CGM);Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.Angalia picha.
  [​IMG]
  – Mchwa
  Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
  Pia kuna wanyama waharibifu ambao hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k
  NB:Unaweza kuzuia wadudu hawa kwa kutumia dawa za wadudu kama DIMETHOATE n.k
  SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI
  Mihogo hulimwa bila kutumia mbolea na inastawi vizuri tu hata katika udongo usikuwa na rutuba ya kutosha, Mtumizi ya mbolea za nitogren hayashauriwi katika kilimo cha muhogo labda kama unataka majani na si muhogo.
  UVUNAJI
  Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 mpaka 12 tangu kupandwa.Pia inashauriwa kuvunwa katika kipindi cha jua,kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #345
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  Muongozo wa Kilimo Bora Cha Muhogo | Mogriculture Tz

  Wakati tunasubiri wataalamu wa masoko, tusome hapa KILIMO CHA MIHOGO

  Utangulizi
  Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania, zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia chakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachuku asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya Lindi na Mtwara.

  Kwa siku za karibuni, muhogo unaongoza kwa kuongezeka katika umaarufu kuliko mazao yote ya chakula nchini. Watalaam wanazungumzia umaarufu wa muhogo kuwa ni (pamoja na mambo mengine) uwezo wake wa kustahamili hali ya hewa mbaya kama ukame na mvua zisizoaminika, kutoa mazao mengi kwa eneo na kustahamili mashambulizi ya magonjwa na wadudu.

  Hata hivyo uzalishaji wa muhogo kwa eneo bado ni wa viwango vya chini mno. Zipo sababu nyingi zinazo sababisha kuwepo kwa hali hii kama vile:
  • Ukosefu wa mbegu bora za mihogo za kutosha
  • Wakulima kuendelea kungangania mbegu zao za asili kuliko mbegu bora licha ya uzalishaji mdogo na kushambuliwa na magonjwa na wadudu.
  • Ukosefu wa masoko ya kuaminika ambayo yangeshawishi wakulima kulima mbegu za kisasa ambazo zimeandaliwa kibiashara.
  • Wakulima wengi kutotumia teknolojia sahihi za usindikaji ambazo ni mbinu mbadala za hifadhi za asili.
  Kwa muda mrefu tatizo kubwa la zao la muhogo ni ukosefu wa teknolojia ambazo zina uwezo wa kuongeza thamani wa muhogo kama chakula chenye ubora kwa familia za mijini na vijijini. Vikundi mbalimbali vya uzalishaji na usindikaji vimeundwa na muhogo umeanza kuthaminwa kwani unga wake unatumika kutengenezea vyakula kama maandazi, chapati, chichili, keki na vingenevyo vingi. Ugali wa muhogo umeongezeka thamani kutokana na ubora wa unga uliosindikwa kwa kwa teknolojia ya kisasa.

  Madhumuni ya Mogriculture Tz kutoa makala hii ni kutoa maelekezo juu kilimo bora cha zao la muhogo ili kusaidia wakulima kuinua viwango vya ubora na wingi wa mazao hivyo kujihakikishia usalama wa chakula na kujiongezea kipato.
  Umuhimu na Matumizi ya Muhogo
  • Muhogo ama (kitaalam) manihot esculentum, ni muhimu sana kwa Tanzania kutokana na sifa zake za kuvumilia ukame, kustawi kwenye maeneo yenye rutuba kidogo hivyo kuhitaji gharama ndogo za uzalishaji. Kwa hali hiyo, zao hili hulimwa sana na wakulima wadogo walio wengi wenye kipato kidogo.
  • Kwa wakazi wa vijijini, muhogo huvunwa, kutolewa ganda la juu na kuanikwa hadi kukauka maarufu kama makopa. Kwa kawaida makopa hutwangwa kwenye kinu na kupata unga ambao hutumika kama uji au ugali. Makopa mara nyingi hutunwa ama kuhifadhiwa kwenye dari ya nyumba ambako hufukiziwa moshi wa moto ili yasipukuswe.
  • Kutokana na hali hiyo, wakulima wengi hulima muhogo mchungu ambao haupukuswi kwa urahisi. Kwa vile muhogo mchungu una sumu nyingi aina ya cyanide, hufanya kiasi kidogo cha muhogo kiliwe kwa kutafuna ukiwa mbichi ama kupikwa kama futari.
  • Kwa wakazi wa mijini, sehemu kubwa ya mihogo hutumika kama futari au kitafunwa kwa chai ama humenywa na kukaangwa kama chips maarufu kama chips dume.
  • Kutokana na kuongezeka kwa teknolojia za usindikaji, unga wa muhogo hutumika kutengenezea biskuti, chapati,maandazi,chichili,keki na vyakula vingine vingi vinavyotengenezwa kwa kutumia unga wa ngano.[​IMG]
  Chakula kilichotengenezwa kwa muhogo

  Mazingira na Aina za Mihogo

  Mazingira yanayofaa
  Muhogo ni zao la jamii ya mizizi. Hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye mwinuko wa mita 0 hadi 1500 toka usawa wa bahari. Zao hili hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa milimita 750 mpaka milimita 1200 kwa mwaka. Muhogo hupendelea udongo wa kichanga usiotuamisha maji. Udongo wa kichanga husaidia mizizi kupenya kwa urahisi na kupevuka. Vile vile muhogo una sifa ya kuvumilia hali ya ukame wa muda mrefu.

  Aina za Mihogo
  Kuna zaidi ya aina 45 za mihogo zinajulikana nchini Tanzania. Zaidi ya asilimia 80 ya mihogo ni ya asili. Hivyo ni kusema wakulima wengi hawatumii mbegu bora. Ingawa wakulima wengi pia hupendelea kulima mihogo michungu kwa sababu haishambuliwi sana na wadudu ama magonjwa shambani na makopa yake yanahifadhika kwa urahisi, zaidi ya asilimia 70 ya mihogo ni mihogo baridi. Bofya hapa kujua mbegu bora mpya za mazao ili uweze kuachana na matumizi ya mbegu za asili.

  Mihogo ya asili
  Mihogo ya asili ni ile iliyoendelea kulimwa miaka mingi iliyopita na kurithiwa vizazi kwa vizazi. Mihogo hii ina sifa za jumla zifuatazo:
  • Hutoa mavuno wastani wa tani kwa Hekta.
  • Mingi inachukua muda mrefu kukomaa
  • Inahifadhika shambani kwa muda mrefu bila kuoza
  • Hushambuliwa na magonjwa kama Ugonjwa wa michirizi ya ki-kahawia, batobato na blaiti.
  • Hushambuliwa na wadudu milibagi
  • Imezoeleka na wakulima hivyo wanaijua tabia yake na jinsi ya kuitunza.
  Mihogo Bora
  Hii ni mihogo iliyofanyiwa utafiti wa pamoja baina ya watalaam na wakulima na kuthibitishwa na Kamati ya Mbegu ya Taifa kama inafaa. Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo cha Naliendele, Mtwara kimebaini mbegu bora aina ya Naliendele na Kiroba ambazo zina sifa zifuatazo:
  • Hutoa mavuno ya tani 19 hadi 30 kwa Hekta.
  • Hustahamili mashambulizi ya ugonjwa Michirizi ya kikahawia, batobato na blaiti.
  • Hukomaa miezi tisa tu baada ya kupanda.

  Kuandaa shamba
  Inashauriwa kuandaa shamba mapema kabla ya msimu wa mvua haujaanza. Zifuatazo ni hatua za msingi katika kuandaa shamba:
  • Kufyeka msitu au vichaka
  • Kung’oa na kuchoma moto visiki
  • kulima na kutengeneza matuta.

  Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
  Aina bora za mbegu za muhogo
  Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimethibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
  • Naliendele
  Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

  • Kiroba
  Huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.
  Katika kuchagua mbegu inayofaa, pamoja na mambo mengine, zingatia yafuatayo:
  • Mbegu itokane na shina lililokomaa vizuri
  • Isitokane na shina la muhogo ulioshambuliwa na magonjwa.
  • Macho yake yasiwe yamekaribiana sana au kuachana sana

  Upandaji wa Muhogo
  Muda wa kupanda

  Kanda ya ziwa: December mpaka January mwishoni Nyanda za juu Kusini: November mwanzoni na
  Kanda ya Mashariki: kuanzia October mpaka December

  Urefu wa kipande cha shina cha kupanda: Baada ya kuchagua mbegu hatua inayofuata ni kukata shina lako la muhogo katika pingili ndogo ndogo tayari kwa kupanda. Inapendekezwa pingili ziwe na urefu wa sentimita 30. Hata hivyo, urefu wa pingili utategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande. Inapendekezwa kipande kimoja kiwe na macho manne hadi sita.

  Nafasi ya kupanda: Nafasi ya kupanda kwa shamba linalokusudiwa liwe na muhogo mtupu ni mita moja toka shina hadi shina na mita moja kati ya mistari. Kwa shamba ambalo mkulima anakusudia kuchanganya mazao, inashauriwa nafasi ya kupanda iwe mita 2 hadi mita 4 (kwa kutegemea aina ya mazao yanayochanganywa) kati ya mistari na mita moja toka shina hadi shina.

  Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
  • Kulaza ardhini (Horizontal)
  • Kusimamisha wima (Vertical) na
  • Kuinamisha ( Inclined/Slunted)
  [​IMG]
  Shamba la mihogo

  Palizi - Kudhibiti magugu
  Katika miezi minne ya mwanzo muhogo unahitaji kupata chakula cha kutosha na mahitaji mengine ya msingi ili uweze kukua na kujenga mizizi mikubwa na imara. Hivyo inashauriwa kufanya palizi la kwanza mapema, angalau mwezi mmoja baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua za mwanzo kunyesha.
  Kwa kawaida palizi hufanywa kwa kutumia jembe la mkono au dawa ya kuulia magugu. Njia nyingine ya kudhibiti magugu ni kupanda mimea yenye majani yanayotanda juu ya udongo. Palizi kwa kawaida hufanywa kila inapoonekana kwamba magugu yameota kiasi cha kuathiri ustawi wa muhogo, hivyo unaweza kupalilia mara 3 au 4 zaidi baada ya palizi ya kwanza hadi muhogo kukomaa.

  Kuchanganya mazao
  Utafiti unaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 80 ya mashamba ya muhogo Tanzania yanachanganywa na mazao mengine. Sababu kubwa zinazotolewa kuhusiana na hali ni kwamba wakulima wanafaidika kwa kupata mavuno ya ziada kama kunde, karanga mahindi maharage, korosho ama njugu.

  Kwa kuchanganya mazao, mkulimalicha ya kuimarisha uhakika na usalama wa chakula, anaweza kuuza mazao mchanganyiko na kujiongezea kipato. Vile vile mazao ya jamii ya mikunde yanasaidia kuongeza rutuba ya udongo.
  Hata hivyo, mazao mchanganyiko ni budi yasilete ushindani na muhogo katika kujipatia chakula, hewa, mwanga, unyevu na mahitaji mengine ya mmea yanayoweza kuathiri ustawi wa muhogo. Inashauriwa pia kuzingatia muda wa kupanda, yaani muhogo upandwe mvua za kwanza ili mazao mchanganyiko yasiweze kuzidi na kuutawala muhogo.

  Uvunaji
  Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua. Mihogo hutoa mavuno ya tani 19 hadi 30 kwa hekta kutegemeana na aina ya mbegu (variety).

  [​IMG]
  Mihogo baada ya kuchimbuliwa

  Usindikaji bora
  Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu tatu:
  • Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
  • Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
  • Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

  Njia bora za usindikaji
  • Kwa kutumia mashine aina ya Grater
  Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
  • Kwa kutumia mashine aina ya chipper
  Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.
  Matumizi ya Muhogo
  • Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
  • Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
  • Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.

  Magonjwa na Wadudu Waharibifu wa Muhogo

  Magonjwa

  Kuna magonjwa mawili ambayo ni muhimu sana na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.
  a) Ugonjwa wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawia katika muhogo
  Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye miinuko iliyo na urefu chini ya mita 300 na unapatikana kidogo sana kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei kabisa.

  Visababishi
  Matokeo ya uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ugonjwa huu ulienezwa na mdudu mweuupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.

  Dalili za Ugonjwa
  Sehemui zote za muhogo zinaweza kuonyesha dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa kulinganisha.
  • Kwenye majani
  Dalili ya kwanza: Chlorosis rangi ya njani hutokea kwanza pembezoni mwa vena ndogo baadae huathtiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa (chlorosis) la rangi ya njano.
  Dalili ya pili: Rangi ya njano ambayo haihusishwi vizuri na vena isipokuwa katika mbaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa ya lamin inaweza isiathirike, majni yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.
  • Kwenye shina
  Huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani, jeraha la zambarau au kahawia linweza kuoneakan nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baaada ya kubandua gome la nje. Pia jeraha la nekrotiki kwenye kovu la shina hutokea baada ya majni kudondoka kutokana na umri wa mmea. Tawi/shina hufa kuanzia kwenye nch kuelekea chini na kusababisha kufa kwa mmea wote.
  • Kwenye mizizi
  Kwa kawaida hutokea baada ya dalili za majani na wakati wa kipindi kati ya uambukizo na kufa, amabpo kifo cha mizizi hutokea kuanzia miezi 5 toka kupandwa. Dalili za mizizi zinabadilika nje ya mizizi na zinaweza kuwa kama kizuizimwanga au shimo au kufa kwenye gome.
  Tishu inayo zunguka mshins ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi. Wakati mwingine mizizi huonekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa, lakini ikikatwa huonekana kufainakufa au rangi ya njano.

  Uambukizaji na ueneaji
  Ugonjwa wa CBSD unaambukizwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimea iliyoathiriwa vinavyosababisha mmea kuonesha kwenye majani dalili za ugonjwa. Kwa kuwa muhogo kwa kawaida huzalishwa kwa njia ya vipandikizi ugonjwa huu huingizwa kwenye sehemu mpya zilizopandwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa.
  Kwa aina zinazovumilia sana kwenye hali za mabondeni, dalili mbaya sana hutokea wakati ugonjwa ukigundulika katika hatua za mwanzo. Uchunguzi umeonesha kwamba Bemisia afer ni mdudu/kisababishi ambacho ndicho kinachohusiana na maendeleo ya hivi karibuni kuhusu uhamishaji wa visababishi kama “ipomovirus”. Mara nyingine inaonesha wadudu weupe (White flies) na kutokana na hali hiyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.

  Udhibiti/Kuzuia
  • Njia ya msingi ya kuzuia/kudhibiti ugonjwa wa CBSD ni kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea isiyo na dalili ya ugonjwa.
  • Ubora wa mashina unahitaji kutunzwa kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza ile iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.
  • Hakikisha kuwa unapanda mbegu bora za muhogo ambazo zinastahimili maambukizi ya magonjwa.
  • Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mhogo ichome moto ili kutokomeza ugonjwa huo.
  • Kuelewa dalili za ugonjwa wa CBSD kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.
  • Hakikisha kuwa unaendelea kutunza mbegu bora zinazoonekana kuvumilia magonjwa sana.
  • Hakikisha kuwa shamba la mhogo linakuwa safi kwa ajili ya kupunguza visababishi vya ugonjwa wa CBSD
  b) Ugonjwa wa batobato au ukoma wa majani (Cassava Mosaic Disease – CMD)
  Ni ugonjwa ambao ulienezwa kwa mara ya kwanza hapa Tanzani mwaka 1894, na baadae uliripotiwa katika nchi nyingine nyingi za Afrika Mashriki, Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na sasa unafahamika kuwa upo maeneo yote yanayolimwa muhogo Afrika. Katika viwango vya kuwepo kwa ugonjwa wa CMD na katika uwingi wa hasara zinazopatikana kutokana na CMD ni kati ya 15 – 20%. Hii ni sawa na tani milioni 15 – 18 zikilinganishwa na makadirio ya shirika la kilimo na chakula duniani ya tani milioni 85 ya mwaka 1997.

  Visababishi
  Tangu ugonjwa wa CMD ulipoenezwa kwa mara ya kwanza, visababishi vilichukuliwa kuwa ni virusi kwa sababu ya kukosekana kisababishi kingine. Kwa hiyo kutokana na kuwa mtazamo huu unalingana na matokeo ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba ugonjwa huu huenezwa na mdudu nzi mweupe (white fly).
  Pia uchunguzi wa mara kwa mara umesababisha utambuzi wa virusi vya aina mbalimbali na tofauti kama ifuatavyo:
  • Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Africa cassava mosaic virus
  • Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Afrika mashariki (East Africa cassava mosaic virus)
  • Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya India (Indian cassava mosaic virus)

  Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease – CMD)
  • Dalili hutokea kwenye jani lenye ruwaraza za michirizi ambazo huathiri sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za awali za ukuaji wa jani.
  • Sehemu za kloritiki hushindwa kutanuka hadi mwisho, hivyo mvutano unajitokeza kutokana na ukuaji usiolingana na jani au majani madogo yaliyoharibika.
  • Majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
  • Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.
  • Kloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.

  Uambukizaji na uenezaji
  • Ukoma wa mhogo huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida hutumika kuzalishia mmea.
  • Pia huenezwa na inzi mweupe (white fly) aitwae Bemisia tabaci G. Aina mbili za inzi au Mbu hao Bemisia (Preisner Hhosny na Aleorodius disperses R) pia huambukiza mihogo katika nchi za Afrika na India
  • Usambazaji wa vipandikizi unaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa CMD katika maeneo mapya.

  Udhibiti/kuzuia
  • Hatua ya msingi ya kuzuia ugonjwa wa CMD ni kwa kuchagua vipandikizi kutoka kwa Mmea ambao hauna uambukizo wowote.
  • Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua
  • Hakikisha kuwa wakati wa kuvuna mihogo kwa ile iliyoathirika na ugonjwa wa CMD inaangamizwa kwa kuchomwa moto.
  • Hakikisha kuwa unatunza shamba na kuwa safi ili kupunguza wadudu waenezao CMD.
  • Hakikisha una elimu ya kutosha juu ya dalili za ugonjwa wa CMD>

  Wadudu/Wanyama waharibifu
  • Cassava MealyBug (CMB)
  Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.
  • Cassava Green Mites (CGM)
  Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.
  • White Scales
  Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.
  • Mchwa
  Hawa hutafuna / hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
  • Wanyama waharibifu
  Hawa hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k
  [​IMG]
  Panzi pia hula majani ya mihogo

  Udhibiti/Kuzuia
  Kwa upande wa wadudu wanaweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:
  • Kutumia dawa za kuulia wadudu
  • Kutumia wadudu marafiki wa wakulima
  • Kwa upande wa wanyama ni kuweka walinzi.
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #346
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  KILIMO BIASHARA: KILIMO BORA CHA MIHOGO

  KILIMO BORA CHA MIHOGO

  KILIMO BORA CHA MIHOGO
  MUHOGO-CASSAVA (Manihot esculenta)

  [​IMG]

  UTANGULIZI
  www.kilimofaida.blogspot.com
  Mihogo ni miongoni mwa mazao ya mizizi ambayo ni muhimu sana kwa chakula, hasa maeneo yenye mvua kidogo na sehemu zenye ukame. Mihogo hutumika kama zao la kinga ya njaa ambapo mizizi yake hutumika kama chakula na majani yake pia hutumika kama mboga.
  Kutokana na baadhi ya maeneo ya nchi yetu kuwa na ukame, wataalamu wa kilimo wanasisitiza na kushauri mazao ya kinga ya njaa yalimwe. Na Mihogo ni miongoni mwa mazao hayo.
  Kwa hiyo basi, uangalizi wa shamba toka kuandaa shamba mpaka mavuno unatakiwa kuzingatiwa.

  HALI YA HEWA ,UDONGO UFAAO NA UTAYARISHAJI WA SHAMBA.

  Ni zao linalostahimili ukame,hustawi vizuri katika maeneo yenye joto la wastani kama ya ukanda wa pwani na yale ya mwinuko usiozidi mita 1500.
  Ili shamba la Mihogo listawi vizuri ni vyema lilimwe kwenye ardhi ya yenye rutuba ya wastani, udongo tifutifu au kichanga na mvua ya wastani. Unyevunyevu ukizidi na mbolea kuwa nyingi husababisha mhogo kukua sana sehemu ya juu na kutoa majani mengi.
  Endapo mihogo inaoteshwa sehemu yenye udongo wa mfinyanzi au mzito, ambao unatuamisha maji, mihogo hushindwa kuweka Viazi itakiwavyo.
  Pia sehemu zenye mawe siyo nzuri kwani huzuia mizizi kusambaa vizuri ardhini.Pia udongo au mchanga wenye asili ya chumvichumvi kwa wingi hufanya baadhi ya mbegu ambazo ni mihogo mitamu kuwa na uchungu,mfano muhogo wa kiroba unaweza kuwa na uchungu kama utachelewa sana kuvunwa kutoka katika eneo la aina hii.

  AINA
  Kuna aina mbalimbali za mihogo. Baadhi ya Sifa zinazoangaliwa wakati wa kutayarisha Mbegu za Mihogo ni;-
  1. Muda wa kukomaa
  2. Mhogo mtamu au mchungu
  3. Uwingi waavuno
  Aina ya mihogo mitamu ni;- Kibaha, Aipin Valeca, Msitu Zanzibar, Kigoma na Kigoma red.kiroba,Binti Athumani,Mzungu
  Aina ya mihogo michungu ni;- Liongo, Ali mtumba, mapangano, Luanda, mzimbatala na Lumbaga.

  KUPANDA
  Mihogo kama mazao mengine, Mkulima hana budi kuzingatia matumizi ya mboga bora ili aweze kupata mavuno mengi na bora.
  Kwa kawaida Mihogo hupandikizwa kwa kutumia vikonyo au pingili zinazotokana na mihogo yenye Sifa zinazotakiwa.www.kilimofaida.blogspot.com
  Pingili ziwe zenye urefu wa wastani wa sentimita 25-30 na wastani wa macho 5-6, na unene wa sentimita 2-4. Mara nyingi sehemu ya shina ndiyo inayofaa kukata pingili.
  Katika kilimo cha sesa, nafasi zinazopendekezwa ni meta 1 kwa meta 1. Katika kilimo cha Matuta nafasi zinazopendekezwa ni meta 1.5 kwa meta 0.75.
  Mkulima asipande pingili changa au zilizokomaa na kuzeeka, na wakati wa kupanda ahakikishe macho 2-3 yako ndani ya ardhi. Aisha hakikisha kuwa pingili urefu wa sentimeta 10-15 unakuwa ndani ya ardhi.
  Mkulima apande pingili kwa kulaza, nyuzi 45 (45°) yaani kimshazari kidogo na macho yatakayotoa machipukizi yawe yameelekea juu. Udongo ugandamizwe kudogo kwa mguu ili pingili ishike vizuri.

  [​IMG]
  PALIZI
  Ipaliliwe mapema inapokuwa hufunika ardhi hivyo majani huzuiwa kuota na kukua vizuri.

  SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI

  Mihogo hulimwa bila kutumia mbolea na inastawi vizuri hata katika udongo usio na rutuba ya kutosha,Matumizi ya mbolea za nitrogeni hayashauriwi katika kilimo cha muhogo labda kama unataka majani na si muhogo.

  MAGONJWA
  Zao la mhogo halina magonjwa mengi lakini ugonjwa wa "Cassava Mosaic" na Batobato ndiyo yanayoathiri sana uzalishaji wa zao hili.Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na nziwadogo weupe.Mmea ulioathirika ukitumika kwa vipando mche mpya nao utakuwa na ugonjwa huu.Majani ya mmea ulioshambuliwa yatakuwa na rangi ya njano na yasiyo na umbo la kawaida. www.kilimofaida.blogspot.com
  Kuzuia ugonjwa huu-panda aina ya muhogo inayostahimili ugonjwa huu,Panda vipandikizi ambavyo havijatoka katika mmea ulioathirika na ugonjwa huu,pia unaweza kuchovya mbegu ulizokata katika maji ya moto kwa muda mfupi na kwa tahadhari kubwa.Pia tumia dawa za wadudu kuua nzi weupe.

  WADUDU
  Mdudu hatari wa mihogo ni " Cassava green mite" ( Buibui wa mhogo) ambaye hupunguza mavuno kwa asilimia 40-80.
  Wadudu wengine ambao wameonyesha madhara makubwa ni cassava mealy bugs ( vidung'ata) ambao wameleta madhara makubwa katika maeneo yalimayo mihogo.

  Mihogo iliyoshambuliwa na wadudu Hawa itaonyesha dalili zifuatazo;-
  1. Shina la mmea huonekana limezungukwa na utando mweupe (white mealy wax)
  2. Kunyauka kwa majani ya mmea.
  3. Mmea hudumaa
  4. Shina la mmea huonekana limepinda
  5. Majani ya mmea hupukutika
  6. Mmea hufa.
  Wadudu hupenda kushambulia majani machanga hasa Yale ya ndani ambako mmea huendelea kukua.

  TIBA ZA KUTUMIA WADUDU
  Kutokana na utafiti, wadudu Hawa wanaweza kuangamizwa kwa njia ya Asili (Biological control). Wataalamu waliagiza manyigu kutoka nje ya nchi pale tu ugonjwa huu iliposhamiri lakini njia hii ilionekana ni gharama kwa Mkulima wa kawaida.

  Kinachoshauriwa ni kupanda Mbegu ambazo hazijashambuliwa na magonjwa.

  Zuia wadudu hawa kwa dawa za wadudu kama vile DIMETHOATE, n.k

  MUDA WA KUKOMAA.
  Muda wa kukomaa unatofautiana kutokana na aina ya mhogo.
  Ila mihogo mingi huanzia miezi sita hadi tisa na kuendelea
  UVUNAJI

  Ikiwa mihogo yako imekomaa ing'oe yote au chagua unayoitaka kuvuna.Epuka kuweka kidonda katika muhogo unaovuna ili kuepusha kuoza kwa urahisi.

  Pia kupata kitabu zaidi cha kilimo cha muhogo kwa njia ya email unaweza kuchangia Tshs.5000/= Kwa M-Pesa 0769429140 au Tigo-Pesa 0675590663 Jina ni ABDALLAH UMANDE.Na utatumiwa Punde tuu baada ya Kulipia na utapata msaada zaidi wa kipindi chote cha kulima muhogo wako.Email yangu ni umande11@gmail.com

  ABDALLAH UMANDE
  0769429140
  umande11@gmail.com
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #347
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  KILIMO CHA MIHOGO
  • Published on July 11, 2016
  [​IMG]
  Abubakari Malinza

  Assistant Program and Field Officer at JBM CONSULTANTS LIMITED
  KILIMO CHA MUHOGO
  Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani

  Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

  TEKNOLOJIA ZILIZOPO
  Mbegu bora za muhogo
  Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.

  Naliendele
  Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

  Kiroba
  Huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

  Mbinu bora za kilimo cha muhogo

  Uandaaji wa shamba

  Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
  - Kufyeka shamba
  - Kung’oa na kuchoma visiki
  - Kulima na kutengeneza matuta

  Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
  Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamekomaa vizuri.

  Upanadaji
  Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
  - Kulaza ardhini (Horizontal)
  - Kusimamisha wima (Vertcal)
  - Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

  Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
  Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

  Nafasi ya kupanda:
  Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.

  Palizi:
  - Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
  - Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
  - Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
  - Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

  Uvunaji:
  Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

  Usindikaji bora
  Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
  - Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
  - Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
  - Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

  Njia bora za usindikaji
  - Kwa kutumia mashine aina ya Grater
  Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
  - Kwa kutumia mashine aina ya chipper
  - Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

  Matumizi ya Muhogo
  - Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
  - Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
  - Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.

  MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
  Magonjwa
  Kuna magonjwa mawili ambayo ni muhimu sana na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.

  a) Ugonjwa wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawia
  katika muhogo
  Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye miinuko iliyo na urefu chini ya mita 300 na unapatikana kidogo sana kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei kabisa.

  Visababishi:
  Matokeo ya uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ugonjwa huu ulienezwa na mdudu mweuupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.

  Dalili za Ugonjwa
  Sehemui zote za muhogo zinaweza kuonyesha dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa kulinganisha.

  - Kwenye majani
  Dalili ya kwanza: Chlorosis rangi ya njani hutokea kwanza pembezoni mwa vena ndogo baadae huathtiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa (chlorosis) la rangi ya njano.
  Dalili ya pili: Rangi ya njano ambayo haihusishwi vizuri na vena isipokuwa katika mbaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa ya lamin inaweza isiathirike, majni yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.

  - Kwenye shina
  Huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani, jeraha la zambarau au kahawia linweza kuoneakan nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baaada ya kubandua gome la nje. Pia jeraha la nekrotiki kwenye kovu la shina hutokea baada ya majni kudondoka kutokana na umri wa mmea. Tawi/shina hufa kuanzia kwenye nch kuelekea chini na kusababisha kufa kwa mmea wote.

  - Kwenye mizizi
  Kwa kawaida hutokea baada ya dalili za majani na wakati wa kipindi kati ya uambukizo na kufa, amabpo kifo cha mizizi hutokea kuanzia miezi 5 toka kupandwa. Dalili za mizizi zinabadilika nje ya mizizi na zinaweza kuwa kama kizuizimwanga au shimo au kufa kwenye gome.

  Tishu inayo zunguka mshins ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi. Wakati mwingine mizizi huonekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa, lakini ikikatwa huonekana kufainakufa au rangi ya njano.

  Uambukizaji na ueneaji
  Ugonjwa wa CBSD unaambukizwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimea iliyoathiriwa vinavyosababisha mmea kuonesha kwenye majani dalili za ugonjwa.
  Kwa kuwa muhogo kwa kawaida huzalishwa kwa njia ya vipandikizi ugonjwa huu huingizwa kwenye sehemu mpya zilizopandwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa.
  Kwa aina zinazovumilia sana kwenye hali za mabondeni, dalili mbaya sana hutokea wakati ugonjwa ukigundulika katika hatua za mwanzo.

  Uchunguzi umeonesha kwamba Bemisia afer ni mdudu/kisababishi ambacho ndicho kinachohusiana na maendeleo ya hivi karibuni kuhusu uhamishaji wa visababishi kama “ipomovirus”. Mara nyingine inaonesha nzi weupe (White flies) na kutokana na hali hiyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.

  Udhibiti/Kuzuia
  Njia ya msingi ya kuzuia/kudhibiti ugonjwa wa CBSD ni kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea isiyo na dalili ya ugonjwa.

  Ubora wa mashina unahitaji kutunzwa kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza ile iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.

  Hakikisha kuwa unapanda mbegu bora za mhogo ambazo zinastahimili uambukizo wa magonjwa.

  Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mhogo ichome moto ili kutokomeza ugonjwa huo.

  Kuelewa dalili za ugonjwa wa CBSD kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.

  Hakikisha kuwa unaendelea kutunza mbegu bora zinazoonekana kuvumilia magonjwa sana.

  Hakikisha kuwa shamba la mhogo linakuwa safi kwa ajili ya kupunguza visababishi vya ugonjwa wa CBSD

  b) Ugonjwa wa batobato au ukoma wa majani
  Ni ugonjwa ambao ulienezwa kwamara ya kwanza hapa Tanzani mwaka 1894, na baadae uliripotiwa katika nchi nyingine nyingi za Afrika Mashriki, Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na sasa unafahamika kuwa upo maeneo yote yanayolimwa muhogo Afrika.

  Katika viwango vya kuwepo kwa ugonjwa wa CMD na katika uwingi wa hasara zinazopatikana kutokana na CMD ni kati ya 15% – 20%. Hii ni sawa na tani milioni 15 – 18 zikilinganishwa na makadirio ya shirika la kilimo na chakula duniani ya tani milioni 85 ya mwaka 1997.

  Visababishi
  Tangu ugonjwa wa CMD ulipoenezwa kwa mara ya kwanza, visababishi vilichukuliwa kuwa ni virusi kwa sababu ya kukosekana kisababishi kingine. Kwa hiyo kutokana na kuwa mtazamo huu unalingana na matokeo ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba ugonjwa huu huenezwa na nzi mweupe (white fly).

  Pia uchunguzi wa mara kwa mara umesababisha utambuzi wa virusi vya aina mbalimbali na tofauti kama ifuatavyo:

  • Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Africa cassava mosaic virus

  • Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Afrika mashariki (East Africa cassava mosaic virus)

  • Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya India (Indian cassava mosaic virus)

  Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)

  Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri

  Sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za

  Awali za ukuaji wa jani.
  Sehemu za kloritiki hushindwa kutanuka hadi mwisho, hivyo mvutano unajitokeza kutokana na ukuaji usiolingana na jani au majani madogo yaliyoharibika.

  Majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.

  Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.
  Kloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.

  Uambukizaji na uenezaji
  Ukoma wa mhogo huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida hutumika kuzalishia mmea.
  Pia huenezwa na inzi mweupe (white fly) aitwae Bemisia tabaci G. Aina mbili za inzi au Mbu hao Bemisia (Preisner Hhosny na Aleorodius disperses R) pia huambukiza mihogo katika nchi za Afrika na India Usambazaji wa vipandikizi unaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa CDM katika Maeneo mapya.

  UHIBITI NA KUZUIA
  -Hatua ya msingi ya kuzuia ugonjwa wa CMD ni kwa kuchagua vipandikizi kutoka kwa Mmea ambao hauna uambukizo wowote.

  -Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua

  -Hakikisha kuwa wakati wa kuvuna mihogo kwa ile iliyoathirika na ugonjwa wa CMD inaangamizwa kwa kuchomwa moto.

  -Hakikisha kuwa unatunza shamba na kuwa safi ili kupunguza wadudu waenezao CMD.

  -Hakikisha una elimu ya kutosha juu ya dalili za ugonjwa wa CMD>

  WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU
  - Cassava Mealy Bug (CMB)

  Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.

  - Cassava Green Mites (CGM)

  Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.

  - White Scales
  Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.

  - Mchwa
  Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
  - Wanyama waharibifu
  Hawa hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k

  Udhibiti/Kuzuia
  Kwa upande wa wadudu wanweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:

  Kutumia dawa za kuulia wadudu

  Kutumia wadudu marafiki wa wakulima

  Kwa upande wa wanyama ni kuweka walinzi.
   
 9. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #348
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  UBUNIFU KATIKA KILIMO CHA MUHOGO NA FURSA ZAKE ~ Green Agriculture Company

  UBUNIFU KATIKA KILIMO CHA MUHOGO NA FURSA ZAKE  [​IMG]

  BIASHARA NA MASOKO YA ZAO LA MUHOGO
  Zao hili la muhogo kitaalamu husifika sana kwa kuwa na kiasi kingi cha wanga na hiyo wataalamu wanaliweka katika kundi la vyakula vya wanga(carbohydrate), mihogo hupendwa sana kutumika kama kitafunwa, ukiwa mbichi au ukiwa umepikwa kwa makabila mengi hapa Tanzania na duniani kwa ujumla na kufanya uhitaji wake uwe mkubwa na pia liwe zao la biashara. katika maeneo mengi ya pwani na kusini mwa Tanzania mhogo hupendwa sana na watu huutumia kama chakula chao kwa mara nyingi.
  katika biashara ya mhugo tukianzia kwa wakulima kwa soko lilivyo sasa hasa kwa mikoa ya pwani kwa hekari moja mkulima akiuzia mihogo yake shambani anapata Tsh 3,000,000/=. na pia inaposafirishwa mpaka sokoni wachuuzi mbalimbali huuza mhogo mmoja kuazia shilingi 500-1000 kulingana na ukubwa.
  [​IMG]
  KILIMO BORA CHA ZAO LA MUHOGO
  Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani.
  Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750 - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.
  • TEKNOLOJIA ZILIZOPO
  Mbegu bora za muhogo
  Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
  Naliendele Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.
  Kiroba
  Huzaa tani 25 – 30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.
  • Mbinu bora za kilimo cha muhogo
  Uandaaji wa shamba
  Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
  Kufyeka shamba Kung’a na kuchoma visiki Kulima na kutengeneza matuta .
  Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamekomaa vizuri.
  Upanadaji
  [​IMG]

  Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo: Kulaza ardhini (Horizontal) Kusimamisha wima (Vertcal)Kuinamisha ( Inclined/Slunted)
  Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
  Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).
  Nafasi ya kupanda:
  Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.
  Palizi:
  Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi minne ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindani wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu. Palizi hufanyika kwa kutumia jembe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.Palizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.
  Uvunaji:
  [​IMG]
  Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.
  Usindikaji bora
  Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
  Kurahisisha/kuharakisha ukaushajiKuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogoKuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.
  Njia bora za usindikaji

  [​IMG]
  HAND OPERATED

  [​IMG]
  POWER OPERATED GRATER

  Kwa kutumia mashine aina ya Grater Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.Kwa kutumia mashine aina ya chipperMashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.
  Matumizi ya Muhogo
  Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza ungaUnga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.

  MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
  Magonjwa
  Kuna magonjwa mawili ambayo ni muhimu sana na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.
  a) Ugonjwa wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawia katika muhogo
  Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye miinuko iliyo na urefu chini ya mita 300 na unapatikana kidogo sana kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei kabisa.
  Visababishi:
  Matokeo ya uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ugonjwa huu ulienezwa na mdudu mweupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.
  Dalili za Ugonjwa
  Sehemui zote za muhogo zinaweza kuonyesha dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa kulinganisha.
  Kwenye majani
  Dalili ya kwanza: Chlorosis rangi ya njani hutokea kwanza pembezoni mwa vena ndogo baadae huathtiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa (chlorosis) la rangi ya njano.Dalili ya pili: Rangi ya njano ambayo haihusishwi vizuri na vena isipokuwa katika mbaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa ya lamin inaweza isiathirike, majni yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.
  Kwenye shina
  Huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani, jeraha la zambarau au kahawia linweza kuoneakan nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baaada ya kubandua gome la nje. Pia jeraha la nekrotiki kwenye kovu la shina hutokea baada ya majni kudondoka kutokana na umri wa mmea. Tawi/shina hufa kuanzia kwenye nch kuelekea chini na kusababisha kufa kwa mmea wote.
  Kwenye mizizi
  Kwa kawaida hutokea baada ya dalili za majani na wakati wa kipindi kati ya uambukizo na kufa, amabpo kifo cha mizizi hutokea kuanzia miezi 5 toka kupandwa. Dalili za mizizi zinabadilika nje ya mizizi na zinaweza kuwa kamakizuizimwanga au shimo au kufa kwenye gome.
  Tishu inayo zunguka mshins ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi. Wakati mwingine mizizi huonekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa, lakini ikikatwa huonekana kufainakufa au rangi ya njano.
  Uambukizaji na ueneaji
  Ugonjwa wa CBSD unaambukizwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimea iliyoathiriwa vinavyosababisha mmea kuonesha kwenye majani dalili za ugonjwa.
  Kwa kuwa muhogo kwa kawaida huzalishwa kwa njia ya vipandikizi ugonjwa huu huingizwa kwenye sehemu mpya zilizopandwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa.
  Kwa aina zinazovumilia sana kwenye hali za mabondeni, dalili mbaya sanahutokea wakati ugonjwa ukigundulika katika hatua za mwanzo.
  Uchunguzi umeonesha kwamba Bemisia afer ni mdudu/kisababishi ambacho ndicho kinachohusiana na maendeleo ya hivi karibuni kuhusu uhamishaji wa visababishi kama “ipomovirus”. Mara nyingine inaonesha nzi weupe (White flies) na kutokana na hali hiyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.
  Udhibiti/Kuzuia
  Njia ya msingi ya kuzuia/kudhibiti ugonjwa wa CBSD ni kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea isiyo na dalili ya ugonjwa. Ubora wa mashina unahitaji kutunzwa kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza ile iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.ü Hakikisha kuwa unapanda mbegu bora za mhogo ambazo zinastahimili uambukizo wa magonjwa.ü Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mhogo ichome moto ili kutokomeza ugonjwa huo.ü Kuelewa dalili za ugonjwa wa CBSD kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.ü Hakikisha kuwa unaendelea kutunza mbegu bora zinazoonekana kuvumilia magonjwa sana.ü Hakikisha kuwa shamba la mhogo linakuwa safi kwa ajili ya kupunguza visababishi vya ugonjwa wa CBSD

  b) Ugonjwa wa batobato au ukoma wa majani(cassava mosaic disease)
  [​IMG]
  MAJANI YALIOATHIRIKA
  [​IMG]
  MIHOGO ILIYOATHIRIKA NA CMD
  Ni ugonjwa ambao ulienezwa kwamara ya kwanza hapa Tanzani mwaka 1894, na baadae uliripotiwa katika nchi nyingine nyingi za Afrika Mashriki, Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na sasa unafahamika kuwa upo maeneo yote yanayolimwa muhogo Afrika.
  Katika viwango vya kuwepo kwa ugonjwa wa CMD na katika uwingi wa hasara zinazopatikana kutokana na CMD ni kati ya 15% – 20%. Hii ni sawa na tani milioni 15 – 18 zikilinganishwa na makadirio ya shirika la kilimo na chakula duniani ya tani milioni 85 ya mwaka 1997.
  Visababishi
  Tangu ugonjwa wa CMD ulipoenezwa kwa mara ya kwanza, visababishi vilichukuliwa kuwa ni virusi kwa sababu ya kukosekana kisababishi kingine. Kwa hiyo kutokana na kuwa mtazamo huu unalingana na matokeo ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba ugonjwa huu huenezwa na nzi mweupe (white fly).
  Pia uchunguzi wa mara kwa mara umesababisha utambuzi wa virusi vya aina mbalimbali na tofauti kama ifuatavyo:
  Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Africa cassava mosaic virusUgonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Afrika mashariki (East Africa cassava mosaic virus)Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya India (Indian cassava mosaic virus)Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)

  Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri
  Sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za
  Awali za ukuaji wa jani.
  Sehemu za kloritiki hushindwa kutanuka hadi mwisho, hivyo mvutano unaji-
  tokeza kutokana na ukuaji usiolingana na jani au majani madogo yaliyoharibika.
  Majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa
  Sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
  Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.
  Kloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe
  yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.

  Uambukizaji na uenezaji
  Ukoma wa mhogo huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaidahutumika kuzalishia mmea.Pia huenezwa na inzi mweupe (white fly) aitwae Bemisia tabaci G. Aina mbili za inzi auMbu hao Bemisia (Preisner Hhosny na Aleorodius disperses R) pia huambukiza mihogokatika nchi za Afrika na IndiaUsambazaji wa vipandikizi unaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa CMD katikaMaeneo mapya.

  UDHIBITI NA KUZUIA
  Hatua ya msingi ya uzuia ugonjwa wa CMD ni kwa kuchagua vipandikizi kutoka kwa Mmea ambao hauna uambukizo wowote.Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ileMihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.Hakikisha kuwa wakati wa kuvuna mihogo kwa ile iliyoathirika na ugonjwa wa CMDinaangamizwa kwa kuchomwa moto.Hakikisha una elimu ya kutosha juu ya dalili za ugonjwa wa CMD>
  WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU
  Cassava Mealy Bug (CMB)
  [​IMG]
  CASSAVA MEALY BUGS
  [​IMG]
  LEAVES AFFECTED BY MEALY BUGS
  Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.
  Cassava Green Mites (CGM)
  [​IMG]
  [​IMG]
  Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.
  White Scales
  [​IMG]
  [​IMG]
  Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.
  Mchwa
  Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
  Wanyama waharibifu
  Hawa hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k
  Udhibiti/Kuzuia
  Kwa upande wa wadudu wanweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:
  i Kutumia dawa za kuulia wadudu
  ii Kutumia wadudu marafiki wa wakulima

  iii Kwa upande wa wanyama ni kuweka walinzi.

  [​IMG]

  Mkulima wa zao la mhogo
  Mr Anthony Mbuja , eneo la Bungu Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani
  (0715934398).
  pia Bw. Anthony analima mazao mengine kama papai, Nanasi, Nyanya, Mhindi pia ni mfugaji wa samaki
  na Anahudumia na Kampuni ya Green Agriculture Company ambayo inatoa huduma za ushauri na uuzaji wa bidhaa na pembejeo za kilimo kama mbegu,mbolea,madawa, drip irrigation, Green house,kupima udongo, Ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua n.k
  Soma zaidi kuhusu fursa ya zao hili
  Octavian Justine Lasway
  Irrigation and Water resources Engineer
  0763347985/0673000103
   
 10. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #349
  May 21, 2018
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. GITWA

  GITWA JF-Expert Member

  #350
  May 25, 2018
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 751
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Hiki kilimo ni kizuri sana kwa wenye nafasi ya ufatiliaji
   
 12. Mkulima Jr

  Mkulima Jr New Member

  #351
  Jul 17, 2018 at 8:38 PM
  Joined: Jul 20, 2016
  Messages: 3
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Wadau natumaini mko pouwa, mimi pia nimkulimaa naanda shamba langu kwa ajili ya msimu wa mwezi wa tisa ekari 25 zote nalimaa mihogo ila pia kwa sasa nilpanda mikorosho miezi minne iliyopita. kama kuna group lolote la whatsup la wakulima wa mihogo naomba uni inbox number ya admin nijiunge, napenda kujua hasa masoko na kupeana mawazo jinsi ya kusukumaa hichi kilimo cha mihogo, mimi nalimiaa kisarawe kijiji kinaitwa mwaga
   
Tags:
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.

Loading...