LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 15,099
- 27,067
Fafanua kuhusu kilimo cha madodoki mkuu ..mkuu kilimo chochote kile kinalipa ni kuona unatumia mbinu gani kupata zaidi
kwa Mfano 1 badala ya kulima mahindi uuze kwa wanaosaga
unaweza kulima ukauza ya kuchoma au ukatenga ya kuchoma na ya kusaga unga
sasa muhindi wa kuchemsha mjini hapa DSM ni sh 1000 kwa muhindi mmoja
kilo ya mahindi ni sh 600 mpaka 800 najua bei inaweza kutofautiana kutokana na hapo ulipo kuna fursa gani kumbuka zao ni lile lile mahindi
Mfano 2 Nililima madodoki baada ya kupata mbegu bora miche mitatu tuu nikapata madodoki kama 400 hivi nikasafisha nikauza madogo sh 500 makubwa sh 1000 tena niliuza mahali tu watu wanapita yaliisha ndani ya siku nne
wakati mwingine nitauza mara 2 ya hiyo bei maana nitakuwa niweka kwenye kifungashio na nitaongeza ubora zaidi
Mfano 3 Kuna mti unaitwa Mlonge ninayo michache
huo sina kumbukumbu nimeingiza kiasi gani maana ni hela nyingi
kuanzia kuuza unga wa majani
mbegu
miche ya kuotesha
kutoka na uzoefu wangu unahitaji kupanga tu vizuri lakini kila kitu kwenye kilimo kinalipa inategemea umejipangaje