Kilimo cha Mchaichai(Lemon Grass): Utaalamu, Masoko na changamoto zake

Maskini....pole yake.....alichukua wapi Sungura?.....nashangaa wanakuuzia Sungura 85,000 ila wakizaa wao wanamnunua 24,000 mabanda ununue kwao, emergency kit, vyakula etc. Wahuni tu hawa!!!.....
Kweli hawa wahuni. Kule Rungwe-Mbeya kuna mzimbabwe alikuja na kilimo cha maparachichi haya wanafanyia budding halafu yanazaa muda mfupi. Alinunua na kukodisha heka nyingi. Yeye biashara yake ni ku-export hayo matunda, akawashawishi wanakijiji kwamba wapande hizo miche yake ya muda mfupi na atanunua matunda kwa sh. 2,500 kwa kilo. Akagawa miche bure baadae akauza kwa bei nafuu sana. Wanakijiji wakafyeka kahawa na chai zao wakapanda miparachichi ya muda mfupi. Jamaa muhuni kama hao jamaa wa sungura.. baada ya kuzaa bei ya maparachichi kwa kilo anasema Tzs 400 - 500 inategemea na ubora. Wananchi hawana hamu na huyo kaburu. Hata ukipeleka kama linamchubuko hachukui anakagua kama nini. Wajanja sana hawa watu
 
Sehemu gani mchaichai unasindikwa au kuuzwa kibiashara, wapi ambapo unaweza kupita usione mchaichai umepandwa kwenye fensi na kwenye makopo!
Ohooo.. kumbe wewe ndio hujui. Muombe msamaha uliemtusi.
 
waulizeni kwanza walowafuata kijani kbichi pale morogoro wakafuga Sungura, mende na wakalima mchaichai waliishia waapi. Maisha hayako simple kama mnavyofikiria, ukisikia jambo usikurupuke kama digi digi mjini. inauma saana kuona watu ambao hawana utaalamu wowote wa kilimo wakiwahadaaa wakulima mchana kweupee.

Nilimshaur saana dadaangu kuhusu hizi fursa lakini alikuwa mbishi saana saana. mmatokeo yaake anataka kwenda mahakamani.

Wito wangu fanyia utafit fursa yeyote utafitii wa kutoshaa kabisaa kabisaa teena uufanye wewe mwenyewe na sio kuulizia kwa watu
Asante, mi niliwapigia simu kuuliza a b c lakini nikaona kuwa wanayoyaongea ni tofauti na hali halisi kwenye kilimo cha mchaichai so nikaona niachane nao..

Kweli tuache kufanya kitu bila utafiti maana tutalia
 
Habari, samahani sana wandugu naomba ushauli wenu kuhüsu kilimo cha mchai chai (eneo lakulima na soko lake ndani na nje ya nchi)
 
Daah ningekuwa najua ningekushauri sana..ila mimi nimepanda hapa home kwa ajili ya matumizi yangu binafsi tu... ila usikate tamaa ukijituma utatoka
 
Habar wana JF,

Nimevutiwa na kilimo cha mchai mchai sana, lakin hadi muda huu sina pakuanzia wala kuelekea.
Kwa yeyote ambae anaufaham zaid kuhusu hii project aje aweke wazi ideas, tuingie kazini tuwajibike.

Nawasilisha.
 
1 Jifunze kutengeneza majani ya chai ya mrutundula unaweza kuukausha ukautumia

2 je umelima kiasi gani?

3 pia unaweza kukausha ukapack kama tea bag ukauza mchai chai uliokaushwa

4 pia unaweza kukausha ukakata kata ukapeleka sokoni kuuzia watu wanaouza viungo maana sio wote wananunua ule mbichi maana una changamoto ya kuhifadhi
 
nimeuliza umelima kiasi gani maana kama ni mwingi soko lake liko zanzibar wanakokamua mafuta ya mchai chai
 
Nadhani kauliza kama kinalipa ndio aanze kulima....kama nimemuelewa Mleta uzi.

mkuu kilimo chochote kile kinalipa ni kuona unatumia mbinu gani kupata zaidi
kwa Mfano 1 badala ya kulima mahindi uuze kwa wanaosaga
unaweza kulima ukauza ya kuchoma au ukatenga ya kuchoma na ya kusaga unga
sasa muhindi wa kuchemsha mjini hapa DSM ni sh 1000 kwa muhindi mmoja
kilo ya mahindi ni sh 600 mpaka 800 najua bei inaweza kutofautiana kutokana na hapo ulipo kuna fursa gani kumbuka zao ni lile lile mahindi
Mfano 2 Nililima madodoki baada ya kupata mbegu bora miche mitatu tuu nikapata madodoki kama 400 hivi nikasafisha nikauza madogo sh 500 makubwa sh 1000 tena niliuza mahali tu watu wanapita yaliisha ndani ya siku nne
wakati mwingine nitauza mara 2 ya hiyo bei maana nitakuwa niweka kwenye kifungashio na nitaongeza ubora zaidi
Mfano 3 Kuna mti unaitwa Mlonge ninayo michache
huo sina kumbukumbu nimeingiza kiasi gani maana ni hela nyingi
kuanzia kuuza unga wa majani
mbegu
miche ya kuotesha

kutoka na uzoefu wangu unahitaji kupanga tu vizuri lakini kila kitu kwenye kilimo kinalipa inategemea umejipangaje
 
Back
Top Bottom