Kilimo cha mboga mboga uhai wa Wilaya ya Lushoto

osieee

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
222
232
Wakuu habari za siku nyingi,

Leo ninakuja na andiko kuhusu namna kilimo cha mbogamboga kinavyowanufaisha wakazi wa wilaya ya Lushoto na halmashauri zake.

Wilaya ya Lushoto inapatikana katika safu za milima ya usambara ndani ya Mkoa wa Tanga, kwa asilimia kubwa wenyeji wa wilaya hii ni kabila la Wasambaa.

Lushoto imekuwa wilaya ambayo inazalisha kwa wingi mbogamboga ambazo kila siku magari huja kuzifungasha na kuzipeleka kwenye masoko makubwa yaliyopo Dar es Saalam Zanzibar Tanga na hata nje ya nchi.

Vijana wengi Lushoto wamepata maendeleo kiuchumi kwa kilimo hiki cha mboga mboga ambacho nyie watoto wa mjini mnakiona takataka, huku Lushoto watu wanajenga na kununua magari kisa kilimo cha mboga mboga, Kijana usikae mjini huku huna kazi njoo uungane nasi vijana wenzako huku Lushoto kuchapa kazi.

Karibuni sana Lushoto tutajirike kupitia kilimo cha mboga mboga.
 
Wapo wengi tu ila sitawataja we njoo huku field uwaone ,just pay a visit to Lushoto
 
Nitajie Bilionea aliyetajirika kwa
Kulima mbogamboga.
Umeonesha umaskini wa akili na hujui kinachoendelea duniani.Ingia YOUTUBE search Hadija Jabir, Mamy Mlangwa na Meshack Maganga.Hao 3 wanakutosha.
Mjini sana wewe,Hata MO na Bakhresa wanatajirika kwa kilimo.Jiulize wewe mwenyewe kila siku unahitaji kula lakini nguo utanunua kila siku HUNA AKILI.
 
Back
Top Bottom