19chazkama
New Member
- May 1, 2016
- 1
- 0
Kwa ekari moja unaweza vuna gunia ngapi za mbaziKwa miaka hii miwili soko na bei nzuri ya mbaazi imeamsha ari na nguvu kuu kwa kila mkulima kuvutika kulima zao hili.
Huko mashambani plastic ya lita 20 inafika hadi sh60,000!
Kiukweli mwenyewe nimevutika haswaa!!
Uzuri wa zao hili kwa mkulima ni kwamba pesa na soko ni chapchap huna haja ya kuweka stoo.
Nendeni shamba wanaJF msibweteke na hizo salaries fikiria juu ya kesho yako. Utagundua kuwa kuishi kwako kwa kutegemea mshahara tu ni utumwa na kifungo.
Kawaida mbaazi kwa ukanda wa pwani na Moro hupandwa kwenye mvua za vuli mwezi october hadi november na utavumilia hadi august ndo mavuno na papo kwa papo unauza mbaazi zako make soko huwa "HOT" kipindi hiki hadi september.
Uzuri kipato cha mbaazi ni kikubwa kuliko ufuta, bei juu na ni nafuu katika kulima kwake na nzuri zaidi zao hili huhitaji mvua za wastani.
Anayehitaji shamba la kukodi asisite kunitafta. Zipo ekari 20 kwajili yako tena ni bonde mwinuko lenye uhakika wa kuvuna!