MADA: Fahamu zaidi kuhusu mbinu za kilimo cha tikitimaji, faida na changamoto zake

Mkuu asikudanganye mtu kilimo ni pasua kichwa, ndio maana unaona watu wanasema kilimo kinalipa lakini wakilima mara moja hawarudii tena. Wewe kama umeajiriwa usithubutu kuacha kazi yako ya ajira ukaenda kulima, utaona kila rangi nakuhakikishia.
 
Kwa wastani ekari moja inaweza kuwa na miche mingapi ya matikiti? Na mche mmoja wa tikiti unaweza kutoa matikiti mangapi??
 
Hii ni nzuri zaidi

ploudly ngosha

Tabu yenu wenye pesa tukiwapa mipango na bajeti huwa mnatuona wezi, wenzenu wanatoka nasi pia tunatoka kupitia hào hao. Hivi ukiweka 4M nawe ukapata 5M nani 2M baada ya kutoa gharama kuna hasara gani kwako.?
 
Habari,

Mimi ni graduate ktk fani ya IT, mwaka 2015, katika chuo kimoja wapo jijin Dar es Salaaam, nilihitimu chuo mwaka 2015 july, nikabahatika kuaply nafasi ya customer care katika moja ya kampuni jijin arusha kupitia zoom nikaipata hiyo nafasi, kwa kweli maisha yalienda sawa kwani walikuwa wana nipa 900k per month.

Niliona uzi wa kilimo cha tikiti maji kuwa kinalipa na mimi nikaamua kujaribu kilimo hiko huku nikiwa kazini. Nilikodi shamba heka mbili kwa kila heka ni 100k, kulima heka moja ni 30k, kukata matuta ni 30k per heka, niliamua kulima heka mbili, na jana niliuza matikiti yangu shambani kwa bei ya 9M, nimeuza kwa kupima kwa kilo,

Nashukuru wana jamvi kwani ujuzi na ujasiri nimeupata humu humu jamii forum, nawashauri vijana
 
Hata sio gazeti mbona kauzi kafupi kabisa haka...

Hongera kwa uthubutu na ni jambo jema ulilofanya kwa kugawa ujuzi kwa wengine...

Sasa kuna maswali kadhaa hapa:
1. Kilimo ulikiendeshea maeneo gani ya TZ na miezi ipi?

2. Uliwekeza jumla ya mtaji wa kiasi gani na ukafanikiwa kupata faida kiasi gani?

3. Baada ya kufikia umri wa uvunaji matikiti, ulipataje soko la bidhaa yako?
 
Watu8,
NAOMBA NIKUJIBU
1. Kilimo ni ARUSHA, wilaya ya ARUMERU, maeneo ya Nduruma

2. niiweka mtaji wa 2M, nikafanikiwa kupata 9M

3. baada ya matikiti kukomaaa, huwa kuna wafanya biashara wanatembelea mashamba kuweka booking ya zao likiwa tayar uwauzie, wakiwemo na madalali wao, hvyo walikuwa wengi, but niliamua kuuza kwa mwenye bei ya juu kdg kwa kilo

NB, kilmo cha tikiti hakina garama sana, garama iko kwenye mbegu, kwani mbegu ya pundamilia ya kutosha heka moja ni 216k.

Gharama niliyo kumbana nayo ni kipindi hiki cha kumwagilia , kiangazi , maji yamepungua, hivyo kuna kuwatoa wenyekiti wa miferegi ya maji kitu kdg upate maji walau mara mbili kwa wiki kuokoa mmmea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom