MADA: Fahamu zaidi kuhusu mbinu za kilimo cha tikitimaji, faida na changamoto zake

Asante sana kwa Uzi mzuri kama huu, natarajia mwezi wa 12 nami nianze hiki kilimo, lakini mwezi wa 12 ni msimu wa mvua Je nilime tu au niache kwanza?
Acha tu mkuu mvua ikizd na tikit limefika kipnd cha kukomaaa linapasuka.
 
Asante sana kwa Uzi mzuri kama huu, natarajia mwezi wa 12 nami nianze hiki kilimo, lakini mwezi wa 12 ni msimu wa mvua Je nilime tu au niache kwanza?
Watu wamekuwa na uoga wa kulima kipindi cha Mvua matikiti. Mimi nimelima padogo, nataka nijionee, naamini hata yakipasuka hayatapasuka yote. Nitapata tu. Kama kulima wewe lima Mkuu, tusijenge uoga kikubwa kumbuka kuweka majani makavu chini ya kila tikiti, majani yawe mengi kidogo. Utapata matikiti. Nimepanda juzi, nitakujaleta mrejesho hapa February.2021.
 
Wengi huwa hawaleti mrejesho kama wanavyosema. Sijui ndo wakishapigwa wanapoteana kabisa! Ngoja tukusubiri hiyo February.
 
Kama yanapasuka Kwa sababu ya maji kuwa mengi ( mvua). Kuwa na utaratibu wa kupulizia OMEX Cal Max. Kazi yake ni kufanya ngozi ya juu ya tikiti kuwa nguma na kuhimili wingi WA maji. Na kuzui kupasuka.
 
Ahsante Mkuu, hii unaitumia kipindi matunda yametoka si ndiyo?

Kwa huku niliko sidhani Kama inapatikana, nitakutafuta nikikosa nitarudi kwako. Madukani ulipo inatembea kiasi gani? Bei
 
Kama yanapasuka Kwa sababu ya maji kuwa mengi ( mvua). Kuwa na utaratibu wa kupulizia OMEX Cal Max. Kazi yake ni kufanya ngozi ya juu ya tikiti kuwa nguma na kuhimili wingi WA maji. Na kuzui kupasuka.
Mkuu niombe unisaidie kampuni inayosambaza hapa Tanzania maana nimejaribu kuitafuta mtandaoni sijaona kwa Tanzania.
 
Watu wamekuwa na uoga wa kulima kipindi cha Mvua matikiti. Mimi nimelima padogo, nataka nijionee, naamini hata yakipasuka hayatapasuka yote. Nitapata tu. Kama kulima wewe lima Mkuu, tusijenge uoga kikubwa kumbuka kuweka majani makavu chini ya kila tikiti, majani yawe mengi kidogo. Utapata matikiti. Nimepanda juzi, nitakujaleta mrejesho hapa February.2021.
Mkuu February ndio hii vipi mrejesho?
 
Kila la kheri. Matikiti ukiyapatia utafurahi.
Kuna mtu alilia huku kitaa.
Unapotoa ndipo unarudisha mara tatu au nne ya kile ulichotoa ila tu inahitaji kujipanga kwa pesa katika kilimo hiki cha matiki maji pesa ni ndefu ila mimi ni mkulima ila ninalima bamia na mipapai tu ndio ninayoiweza kwa mimi tu!!
 
Tikiti gumu kulima.unatakiwa ujipange kweli.na mbegu iwe nzuri
Unapotoa ndipo unarudisha mara tatu au nne ya kile ulichotoa ila tu inahitaji kujipanga kwa pesa katika kilimo hiki cha matiki maji pesa ni ndefu ila mimi ni mkulima ila ninalima bamia na mipapai tu ndio ninayoiweza kwa mimi tu!!
 
Mkuu February ndio hii vipi mrejesho?
Mkuu, kwanza nikupe hongera kwa umakini ulionao. Kwakuwa niliahidi kuleta mrejesho hapa, leo nimeona ndiyo siku muafaka ya kuleta maana nilikuwa sijafunga shughuli rasmi (kuvuna).

Tarehe 10/11/2020 nilipanda matikiti maji eneo la ukubwa wa robo Ekari. Kimsingi nilisia (panda) Mbegu 880 aina ya Sugar Queen F 1. Kilichopelekea kupanda Mbegu chache, hivyo nilifanya kama shamba darasa Kwangu binafsi.

Mitaani, mitandaoni kumekuwa na maneno mengi kwamba matikiti maji masika ukipanda huwezi kuvuna bali utaambulia hasara ya jumla. Ni maneno haya yalinifanya nijiridhishe ukweli na uhakika wa Jambo hili. Yafuatayo ni matokeo ya kujiridhisha Kwangu.
1. Tikiti masika linastahili kulima kwa wingi tu na kufuata taratibu za kilimo zote.
2. Tikiti masika linahitaji upuliziaji wa dawa za Fangasi, (tumezoea kusema ukungu) mara kwa mara, isizidi siku tano kama mvua inanyesha.
3. Hakikisha shamba lako lote umefunika majani makavu kwa wingi. Matikiti yakigusana na maji kwenye udongo yanaoza Sana. Na hapa ndipo nilipofikia hitimisho kuwa wengi huwa hawaweki majani makavu kabisa. Hivyo matikiti yao kuwa kwenye udongo kiasi kwamba mvua zinaponyesha matikiti huoza. Hili nimeshuhudia hata sehemu ambayo majani yalikuwa kidogo matikiti yalioza ila sehemu ambayo majani makavu yalikuwa mengi tikiti nimevuna na limekuwa kubwa. na
4. Masika minyoo ya ardhini inakuwa mingi unapaswa kupiga dawa kwa umakini sehemu lilipo tunda la tikiti ili kulilinda.

Hichi ndicho nilicho kiona karibu tuendelee kupambana Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe.
 
Katika Mbegu hizo nimepata matikiti 1300 makubwa, naamini sijafeli maana sikuwa na mwalimu wa kuniongoza.

Safari ijayo nitarealize full potential.
 
Naomba kujua wapendwa wa kilimo cha matikiti.tikiti linazaa watoto wangapi ambao unaweza kuvuna na ukauza!
 
Katika Mbegu hizo nimepata matikiti 1300 makubwa, naamini sijafeli maana sikuwa na mwalimu wa kuniongoza.

Safari ijayo nitarealize full potential.
Ulipata faida sh. Ngapi na mtaji ulikuwa sh. ngapi.
Soko vipi, uliuza kiurahisi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom