MADA: Fahamu zaidi kuhusu mbinu za kilimo cha tikitimaji, faida na changamoto zake

Sangoma

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
342
162
1582275257158.png

Jinsi ya Kulima matikiti maji
Matikiti maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.

Katika shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri, kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.

Hali ya hewa
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota.

Mvua : kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.

Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0

Maeneo yanayofaa kwa kilimo cha matikiti maji
Kwa upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu mpaka wa tisa.

Uandaji wa shamba
Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingne ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonja.

Upandaji
Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)

Upunguzaji wa mimea
Mimea ya michikichi huanza kuota, baada ya kama wiki 2. Hivyo katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio uendelee kukua.

Aangalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki. Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.

Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda.

Wakati mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.

Matandazo (MULCHES)
Matandazo ina maana ya kutumia nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.

Uwekaji wa mbolea
Mbolea za viwandani aina ya NPK au mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10 hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni midogo mpaka pale maua ya kike yatakapoanza kuonekana. Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya urea na potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.

Umwagiliaji
Shamba linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au wakati wa mvua chache. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.

Angalizo; usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa uchavushaji.

Maua na matunda
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume huwa ni madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k

Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.

Hii hufanywa kwa , kukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa zaidi wakati wa Asubuhi.

Magonjwa na wadudu
Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.

Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa kuthibiti ugonjwa magonjwa hayo hapo juu.

Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda.
Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.

Uvunaji Matikiti
Kabla ya kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani miezi mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii hutegemea na aina ya matikiti yenyewe. Tikiti lililo komaa linaatakiwa na mwonekano wake huwa kama ifuatavyo;

Rangi ya mng’ao hupotea upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano. Pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu. Ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.

Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi.

Soko la matikiti maji
Ukubwa wa tikiti na mwonekano wake ni baadhi ya sifa zinazoangaliwa na wananuzi. Matikiti madogo sana huwa hayapendi sana na wanunuzi. Kwa Tanzania wakulima wengi wanauza matikiti katika masoko ya ndani yanayopatikana takribani nchi nzima. Kwa miaka kadhaa tikiti moja limekuwa likiuzwa kwa wasitani wa shilling 1000 kwa tikiti dogo mpaka 3000 kwa tikiti kubwa katika masoko.

Mavuno
Mavuno ya matikiti yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa. Matikiti pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya matikiti. Kwa wastani matikiti yanaweza kutoa kutoa mavuno kati ya TANI 15-36 kwa hekta moja.


Baadhi ya Changamoto za kilimo hiki zilizojadiliwa na Wadau
Habari za majukumu wadau

Sababu za kuanzisha uzi huu nikuwataka wadau mchangie ili watu wajue faida na hasara za kilimo cha matikiti maji maana watu wengi wamekuwa wakisema mambo katika lugha nyepesi ambayo ukitafakari kwa kina lazima ushindwe kupata jibu kamili.

Mimi kwa upande wangu sijawahi ona mtu aliefanikiwa katika kilimo hichi maana wengi nao waona wamekuwa wakilima mara moja na kupotelea mitini kama wewe ni mhanga toa ushuhuda wako.

Ilikiwaje ukapata hasara na kama ni mnufaika wa hii kitu toa maelezo na kwa upande wako ilikiwaje ukapata faida na vp bado unaendelea na hichi kilimo au ishakuwa pasua kichwa.

Nililima eka moja yalianza vizuuri yakazaa Matunda vizuuri watu wakaanza kunisifia wengine kukadiria, mwingine utapata million 4, mwingin 6 mwingine 3, yalipofikisha siku 60 yalianza kuoza, kutobolewa na wadudu, mashina kukauka hovyo, na mengine kupasuka.

Yaan niliishia kupokea pole kama mtu aliyefiwa. Kweli nilikuwa nayahudumia madawa mbolea na maji kwa kufuata utaalam, sasa nimejuta, nilitumia laki8 nikaambulia laki3.5 so usikurupuke changamoto ni nyingi sana

FAIDA ZA KILIMO HIKIZILIZOELEZWA NA WACHANGIAJI
Hii kitu inafaida sio ndugu ipo kubwa tu,

Mwaka huu mwezi wa tano nimelima hekari almost nne ingawa hazikutimia vizuri,

Roughly tulitumis kama 4million coz tupo wawili,

Tuliyauzia shambani kule kule kwa 10million,

Hatukutaka usumbufu wa sokoni,

Mimi nilichokifanya nilitafuta mtaalamu anayelima tukashare nae,

So kwa uzoefu wake miaka yote nilijua hatuwezi kuchoma pesa,

Baada ya hapo tuligawana mitaji yetu na pesa iliyobaki tukaifanya mtaji tena wa project zilizofuata,

Tayari tuna hekari tatu ambazo zina mwezi mmoja,

Na zingine tano tutapanda mwezi tarehe moja mwezi wa 8

Mungu bariki kazi ya mikono yangu
===
Habari,

Mimi ni graduate ktk fani ya IT, mwaka 2015, katika chuo kimoja wapo jijin Dar es Salaaam, nilihitimu chuo mwaka 2015 july, nikabahatika kuaply nafasi ya customer care katika moja ya kampuni jijin arusha kupitia zoom nikaipata hiyo nafasi, kwa kweli maisha yalienda sawa kwani walikuwa wana nipa 900k per month.

Niliona uzi wa kilimo cha tikiti maji kuwa kinalipa na mimi nikaamua kujaribu kilimo hiko huku nikiwa kazini. Nilikodi shamba heka mbili kwa kila heka ni 100k, kulima heka moja ni 30k, kukata matuta ni 30k per heka, niliamua kulima heka mbili, na jana niliuza matikiti yangu shambani kwa bei ya 9M, nimeuza kwa kupima kwa kilo,

Nashukuru wana jamvi kwani ujuzi na ujasiri nimeupata humu humu jamii forum, nawashauri vijana
===
Watu8,
NAOMBA NIKUJIBU
1. Kilimo ni ARUSHA, wilaya ya ARUMERU, maeneo ya Nduruma

2. niiweka mtaji wa 2M, nikafanikiwa kupata 9M

3. baada ya matikiti kukomaaa, huwa kuna wafanya biashara wanatembelea mashamba kuweka booking ya zao likiwa tayar uwauzie, wakiwemo na madalali wao, hvyo walikuwa wengi, but niliamua kuuza kwa mwenye bei ya juu kdg kwa kilo

NB, kilmo cha tikiti hakina garama sana, garama iko kwenye mbegu, kwani mbegu ya pundamilia ya kutosha heka moja ni 216k.

Gharama niliyo kumbana nayo ni kipindi hiki cha kumwagilia , kiangazi , maji yamepungua, hivyo kuna kuwatoa wenyekiti wa miferegi ya maji kitu kdg upate maji walau mara mbili kwa wiki kuokoa mmmea
===
kama kichwa kinavyojielezea najua wengi mmepata hasara kwenye kilimo hiki! me cjawahi pata hasara hata mara moja labda nipate faida ndogo zaidi ya nliyoiwazia.

nimelima hii ni mara ya 4 mara ya kwanza nlilima heka moja mara ya pili 2 mara ya 3 mbili sasa hiv nalima heka 3 na nusu.

kikubwa tkiti inahitaji mtaji mkubwa yaaani tikiti ni kama kumhudumia mwanamke jinsi unavyozidi kumhonga ndo anavyopendeza ntajibu maswali kwa kadri nitakavyoweza.




 
Nililima eka moja yalianza vizuuri yakazaa Matunda vizuuri watu wakaanza kunisifia wengine kukadiria, mwingine utapata million 4, mwingin 6 mwingine 3, yalipofikisha siku 60 yalianza kuoza, kutobolewa na wadudu, mashina kukauka hovyo, na mengine kupasuka.

Yaan niliishia kupokea pole kama mtu aliyefiwa. Kweli nilikuwa nayahudumia madawa mbolea na maji kwa kufuata utaalam, sasa nimejuta, nilitumia laki8 nikaambulia laki3.5 so usikurupuke changamoto ni nyingi sana
 
Ni vizuri mmeanza kuleta mrejesho, kama hujawah kufanya kilimo, usikurupuke kuingia kichwa kichwa na kama ww ni wakukata tamaa basi kilimo sio mahala pako. kilimo ni umiza mgongo na kilimo kina faida. Ndio biashara ambayo faida itazidi mtaji.
 
Nililima eka moja yalianza vizuuri yakazaa Matunda vizuuri watu wakaanza kunisifia wengine kukadiria, mwingine utapata million 4, mwingin 6 mwingine 3, yalipofikisha siku 60 yalianza kuoza, kutobolewa na wadudu, mashina kukauka hovyo, na mengine kupasuka. Yaan niliishia kupokea pole kama mtu aliyefiwa. Kweli nilikuwa nayahudumia madawa mbolea na maji kwa kufuata utaalam, sasa nimejuta, nilitumia laki8 nikaambulia laki3.5 so usikurupuke changamoto ni nyingi sana
Duh! tunashukuru kwa mrejesho.. kumbe mambo sio rahisi kama nilivofikiri

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
Thread za kuanzisha project ni nyingi ila thread za mrejesho ni hakuna.

Hii inamaanisha kilimo si mchezo mchezo.

Kikubwa ni kutokata tamaa na uvumilivu.

Kilimo kunawakati kina lipa hata miaka mi 5 mfululizo na kikikaa kushoto ndo hivyo tena.

Unapoingia kwenye kilimo tegemea vyote.
 
Mimi kuna jamaa yangu alijikita akahamia shamba na mashine ya umwahiliaji, mara ya kwanza alipovuna bei ikawa chini akala hasara, akalima tena mvua ikazd yakaharibika. Akarudia tena yakanyauka akaacha akahamia kwenye matango.

Kavuna bei iko chini wateja nao shida yani kakata tamaa
 
Hii kitu inafaida sio ndugu ipo kubwa tu,

Mwaka huu mwezi wa tano nimelima hekari almost nne ingawa hazikutimia vizuri,

Roughly tulitumis kama 4million coz tupo wawili,

Tuliyauzia shambani kule kule kwa 10million,

Hatukutaka usumbufu wa sokoni,

Mimi nilichokifanya nilitafuta mtaalamu anayelima tukashare nae,

So kwa uzoefu wake miaka yote nilijua hatuwezi kuchoma pesa,

Baada ya hapo tuligawana mitaji yetu na pesa iliyobaki tukaifanya mtaji tena wa project zilizofuata,

Tayari tuna hekari tatu ambazo zina mwezi mmoja,

Na zingine tano tutapanda mwezi tarehe moja mwezi wa 8

Mungu bariki kazi ya mikono yangu
 
Wakuu tukitaka kulima zao fulani tusikurupuke,

Tufanye utafiti wa kina kuhusu tunachotaka kukifanya na tusifanye kwa sababu ya thread za JF,

Tafuta wataalamu wa ile kitu kaa nao ana kwa ana uhoji kwa kina,

Tembelea mashamba ya kilimo hicho angalia ulizia gharama vizuri ujiridhishe,

Kama huwezi kukaa shambani tafuta mtu utakayemwamin uingie nae ubia hapa nashuri awe mkulima mwenye mtaji mdogo,

Ongea nae mwambie m nipo busy nafanya hiki na kile so naomba tuchangie tulime shamba kubwa wewe ndo utakuwa msimamizi,

If possible hata kwenye mgawo awe na pesa yake ya usimamizi,

Fanya kutembelea shamba walau mara mbili mara tatu kwa week kama upo karibu na kama uko mbali hata once kwa mwezi sio mbaya hakikisha unaingia shambani unaangalia kinachoendelea,

Sasa sisi tunalima kwa simu tgo pesa mpesa airtel money ndo link yetu hapo lazima uwe na hasara,

Sisi hao pesa tunazitaka na mambo yasiyo ya msingi tunayataka lazima kimoja kiponyoke na alwayz kinachoponyoka ndo huwa na faida.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom