kilimo cha mananasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kilimo cha mananasi

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by mymy, Aug 22, 2012.

 1. m

  mymy JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Naombeni msaada kwa yeyote mwenye ujuzi wa kilimo cha mananasi! Nataka kupanda mananasi eneo la Bupu - Mkuranga je,
  1. Itanigharimu muda gani na kiasi gani kuitunza hadi ikue na kufikia mauzo?
  2. Shamba ninalo ekari 4 je kwa wastani nitahitaji miche mingapi?
  3. Mbegu nzuri zake zinapatikana wapi zaidi?
  4. Soko la mananasi kwa sasa?
  5. Angalau kwa kiwango cha chini nanasi moja naweza kuiuza kwa shliingi ngapi??
  Asanteni wapendwa!
   
 2. yatima

  yatima JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Nitakujibu kama nijuavyo mimi (ila mimi sio mtaalamu ila nina experience)

  1. Itakuchukua muda wa miaka 2 hadi mavuno
  2. Kila ekari unahitaji miche 10,000 hadi 15,000
  3. Mbegu nzuri - ni PM nitakuuzia
  4. Soko - bei ya shambani - kama kubwa 1,000 dogo 500

  Mungu akubarikis ana kwa kuchagua kilimo hiki - ni kizuri - mradi utumie mbolea - na utakapovuna WEWE utauza NANASI na MBEGU pia
  Usikate tamaa kusubiri 2 years kabla ya kuanza kuuza

  Soko - Kwa Bakhresa, Mahotelini, Masokoni na Mtaani pia.
   
 3. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kwa ekari moja kwa hesabu za hapo juu inaonyesha unaweza kupata sio chini ya 5M ukiwa na ekari 10 unapata 50M
  Duuuuu,sidhani kama hizi hesabu zipo realistic but all in all nisikukatishe tamaa just try but I'm sure kinalipa tu hicho kilimo
   
 4. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2014
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu tena hiyo hesabu iko chini. Nimesoma article moja yeye anasema unaweza kupanda miche Hadi 25,200 Kwa ekari which means ni mara mbili ya mahesabu ya huyu. Inaonyesha kilimo cha nanasi kinalipa. Nami naenda kulima aiseee. KILIMO BORA CHA MANANASI  Zao la mananasi hulimwa sana hapa nchini maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Geita, Mwanza, Tanga, Mtwara, Lindi na maeneo mengine. Zao hili lina kiasi kikubwa cha vitamini A na B na kiasi kidogo cha vitamini C, pia kuna madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam
  [​IMG]

  HALI YA HEWA
  Manansi hustawi sana ukanda wa pwani usawa usiozini mita 900 toka usawa wa bahari ambapo kuna mvua nyingi kiasi cha milimita 1500 na unyevu wa kutosha, pia unaweza kupanda kwenye maeneo yenye mvua chache lakini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, Hali ya joto ni kuanzia sentigredi 15 - 32, huwa haya stahimili baridi

  UDONGO
  Udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji ndi unaofaa kwa ajili ya kilimo cha mananasi, unaweza kutumia samadi au mbole vunde ili kuongezea rutuba ya udongo wako.

  MSIMU
  Kwa ukanda wa pwani wenye mvua mbili kwa mwaka upandaji wa mananasi huanza mara baada ya mvua za kwanza kuanza, ni vizuri kupanda kwa muda mfupi ili uzaaji usipishane sana na pia kusaidia kupata mvua za kutosha kabla ya msimu kuisha.

  UPANDAJI
  Tumia miche ya aina moja na yenye umri sawa ili huduma zifanane na pia uzaaji uwe wa mpangilio, umbali toka mmea hadi mmea ni sentimeta 30 na mstari hadi mstari ni sentimeta 60, na umbali kila baada ya mistari miwili miwili ni sentimeta 90

  [​IMG]
  Kwa ekari moja unaweza kupanda miche 25,200 na kwa hekta moja unaweza kupanda miche 44,000. ili mananasi yako yastawi vizuri basi tengeneza kama mtaro mdogo na kwenye mitaro ndio upande mananasi yako, hii husaidia kupata unyevu zaidi

  MBOLEA
  Kwa wale wanaotumia mbolea za viwandani, ni vizuri kutumia NPK na DAP ambazo utaweka miezi miwili baada ya kupanda na miezi 12 baada ya kupanda baada ya hapo hautahitaji mbolea tena, lakini ni vizuri zaidi kama utatumia mbolea za asili

  WADUDU
  Wadudu wanaoshambulia mananasi ni aina ya mealybug ambao huondolewa kwa kupulizia dawa kama dume na karate.
  [​IMG]

  Ugonjwa wa kuoza moyo wa miche unaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za copper oxychloride au kwa kuzamisha miche kwenye dawa za fungasi (fungicides)kabla ya kupandwa shambani

  UVUNAJI
  Mananasi huwa tayari kuvunwa miezi 18 mpaka 24 baada ya kupandwa kutegemeana na mbegu na matunzo ikiwemo kiasi cha mvua, mbolea na unyevu shambani, Uvunaji hufanyika kwa kutumia visu na vibebeo maalum kuhakikisha ubora wa zao hili
  [​IMG]
   
Loading...