Kilimo cha Maharage: Mbinu za kulima, Ushauri na Masoko yake

Habari za saa wakuu wangu?

Bila kupoteza muda niende katika jambo husika kwenu wahenga na wasamaria mnisaidie maarifa...

Wakuu kama mhitimu bila kupoteza muda ktk kutafuta na kusubiri kupata ajira mwaka huu nilifanya maamuzi ya kuwekeza fedha yangu ya akiba ktk kilimo cha maharage huko Gairo Morogoro, namshukuru Mungu pamoja na changamoto za ukosefu wa mvua nimefanikiwa kupata mavuno yakuridhisha kiasi chake, nililima maharage ya njano na soya... Ktk hali ya ugeni ktk sekta hii na changamoto katika kumuuguza mama ambae kwa mapenzi ya Mungu aliona mama apumzike sikufanikiwa kufanya tafiti za kutosha juu ya soko la maharage

Sasa nimevuna na ninao mzigo kubwa wastani wa tani 5 na bado sijamaliza kuvuna ni maharage ya soya na njano, kwa yeyote mwenye kujua soko lake kwa wafanyabiashara ama taasisi yoyote tafadhali niunganishe nao, natanguliza shukrani za dhati

1 kg ni 1400 bei yaweza kupungua kulingana na ukubwa wa mzigo pia tutaweza fanya kazi endelevu hata baada ya msimu kupita, gharama za usafiri kwa asilimia kubwa zitakuwa kwangu, karibu pm mkuu
Huyu km sio tapeli basi Mungu akulinde wewe utakaempigia huyu mtu mana unaweza kuingizwa mkenge livelive
 
Nataka kuingia kwenye kilimo cha maharagwe Arusha. Je, ni njia zipi zitahitajika kupitia kilimo hiki? Faida, hasara! Angalizi!!mahitaji!!eneo!!!navinginevyo!!!kabla sija anzishaa!!
Naombeni mawazo yenu wapendwa??
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Ni yakweli haya jamaaan
 
HABARI wakuu

SHAMBA+ ni mtandao unaotumia App, Whatsapp channel na SMS utakaokutanisha wadau wote wa kilimo ie Wakulima, Bwana shamba, wauzaji pembejeo na mbegu na madawa, na masoko ya bidhaa za kilimo. Kazi/dhumuni la huu mtandao ni : (i) Ushauri wa kilimo kutoka kwa agronomist - NI BURE kama unatumia WHATSAPP au APP, kama ni SMS utalipia (ii) Maswali na majibu kati ya mkulima, Agronomist, wauzaji pembejeo - NI BURE kama unatumia WHATSAPP au APP, kama ni SMS utalipia (iii) Agronomist kuweza kuona maduka ya pembejeo/mbegu, wakulima mbalimbali na Agronomists wenzao wa mikoa mbalimbali na kuweza kuwasiliana na kujitangaza - NI BURE ila ni kwa kutumia APP NA WHATSAPP tu (iv) Kuona masoko na kuwasiliana na wanunuzi wa mazao - NI BURE ila ni kwa kutumia APP NA WHATSAPP tu
 
habari wakuu....?
nimerahisisha kwa sasa unaweza kuingia kwenye hizo link ukajibu maswali ya survey kirahisi...

hii ni maalum kwaajili ya wakulima

shamba+

habari wadau wa kilimo .....kwa sasa tiyari tushafungua whatsapp channel ya kusubscribe isave hii namba +27634444350 kisha ingia whatsapp na uitumie ujumbe wa neno la shamba+ kwa herufi ndogo hapo moja kwa moja utakuwa umesubscribe....

baadaye wadau wengi wa kilimo wakisha subscribe hii channel itakuwa inasaidia kutoa information kwa mfano mkulima akiingia na kuulizia masuala ya pembejeo au bwana shamba basi moja kwa moja ataweza kupata jibu hapo hapo kupitia bwana shamba aliye hewani kwa mda husika...pia unaweza kufollow page yetu instagram shambaplus_

kwa maelekezo zaidi unaweza kunipigia 0692449416
 
Binafsi mwezi uliopita nilijaribu kuanza kulima harage la njano. Nilianza na nusu heka, sasa hivi yashaanza kutoa maua. Nilifikia uamuzi huu baada ya kugundua asilimia kubwa ya wakulima wanalima kienyeji sana hivyo ubora wa maharage unakuwa mdogo.

Huwa nanunua maharage kwa kiasi kikubwa toka kwenye soko la mazao na kuyasafirisha Dar. Changamoto kubwa ya biashara hii ni endapo mzigo wako ukipata competition ya ubora na mizigo mingine, hapa itabidi ushushe bei kidogo. Kwa upande wa maharage ya njano, mikoa ya Arusha na Tanga ndio wanaongoza kwa ubora then Lilondo na Madaba (Ruvuma). Harage la njano la Songea mjini nilipolifikisha Dar liliuzwa kwa 1700 per Kg,wakati ya Lilondo ni 2000 per Kg na Arusha na Tanga ni 2200 - 2400 per Kg.

Kinachotofautish bei ni unene na ubora wa harage. Utafiti wangu ndio umenifanya nijaribu kulima mwenyewe (nimeanza na nusu heka) ila hapo baadae nitaingia miguu yote miwili pindi nikikamilisha utafiti. Wakulima wengi wanakwepa gharama za utunzaji na uendeshaji kilimo. Ila kama utapanda na kufata taratibu zote za uwekaji mbolea na upuliziaji dawa,nna uhakika outcomes ni nzuri na zao litakuwa bora (hiki ndio nataka nikifanye) then nisafirishe direct hadi Dar.

Ila kwa upande wangu nataka nifanye kilimo cha umwagiliaji,hapa namaanisha nikivuna kwenye ili jaribio langu mvua ndio zitakuwa zinaanza. Nitatulia kwanza then nisubirie kununua kwa wakulima wengine kama kawaida. Then nitaingia shambani tena mwezi wa 3 mwishoni mvua zikianza kupungua ili niexecute plan yangu.

Nikirudi kwako mkuu Kisima, pamoja na mchanganuo uliotutolea kwa upande wako. Ila itakuwa vizuri ukituonesha na picha walau tuone hayo matuta yanakuwaje,upandaji wa hizo mbegu umekaaje na mfumo mzima wa hizo pump za umwagiliaji upoje ili walau tuwe na clear image vichwani mwetu.

Shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbegu umetumia hizihizi za maharage ya dukani au umenunua kutoka duka la pembejeo?
 
NAUZA BIASHARA YA CAR WASH:

LOCATION: KINONDONI BLOCK 41
NAMBA YA SIMU: 0717 26 33 77

MAELEZO:

MACHINE ZOTE, UJENZI, VYOMBO, SIMTANK, KODI n.k JUMLA: TZS 7,000,000
NIMEBAHATIKA KUPATA KAZI SERIKALINI NA KITUO CHANGU KIKO MKOANI, SO NIMEAMUA KUUZA HII BIASHARA.
 
Hii ndo habari njema wakuu!

Mimi nalima harage ya njano. Nalima kwa surface irrigation (furrow method)

Njia hii utaimudu kwa ufasaha kulingana na muonekano wa shamba lako. (natoa huduma hii kwa mhitaji).
Huwa nalima kwa mahesabu make mi ni mwanahesabu tangu kuzaliwa kwangu;

Hiki ndicho nifanyacho:
1) Ekari1 huwa naigawa kwa mistari5 iliyo sawa;
Kawaida 1acre=>4000sqm. Kwahiyo basi
4000/(8m*2m)*10kg*2000Tsh@kg= Tsh5,000,000

Katika hesabu hii:
4000sqm ni eneo lote la ekari kwa square mita.
8m ni urefu wa kila kijaruba kwa kipimo cha mita.
2m ni upana wa kila kijaruba kwa kipimo cha mita
10kg ni uhakika wa mavuno ya kila kijaruba.
2000Tsh ni kiasi cha bei ya maharage ya njano kwa kila kilo.
Tsh 5,000,000/= ni mapato ya jumla katika kila ekari.

Ufuatao ni mchanganuo wa gharama ya hiki kilimo kwa ekari moja kulingana na eneo la kilimo kinapofanyika na msimu husika hasa kipindi cha jua kali.

1) Natumia 6ltr@acre
2) kawaida namwagilia mara 10 mpaka kuvuna maharage kulingana na hali ya hewa.(6ltr*10=2500*6*10=>150,000/-)
3) natumia mbolea ya CAN Kg50@are=>Tsh90000
4) Tsh 200,000 kulima na kuchora muelekeo wa utiririkaji wa maji.
5) Booster 2ltr@6000=>12,000
6) Fungicide=>40,000
7) Insecticide=>48,000
8) Mbolea supergro tsh 250,000.
9) Palizi nafanya mwenyewe
10) Navuna na kupokea mkwanja nikiwa shamba. Siku hiyo lazima nichinje jogoo kwajili ya mteja!

Karibuni sana shamba. Ukiamua kuchagua upande huu utakuwa njia sahihi.

Usimtegemee mwajiri wako maana anakutumia kwa ujira finyu na ukizeeka hatakuhitaji kamwe.

Janjaruka mwanangu usiwe poyoyo!!
Naomba namba zako Kisima tuongee
 
Naomba namba yako Kisima nikupige, yangu ni 0768884019
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom