Lifahamu zao la Macadamia (Karanga Pori) na jinsi ya kulilima

ASANTE,
Marekebisho kidogo, Macadamia zinalimwa sehemu nyingi sana Tanzania, sehemu nyingine ni Arusha, Moshi na Tanga, lakini baba lao ni Sahare Mission Tanga. Pale lipo shamba lililoanzishwa na RC, Benedictine Fathers mwaka 1945 kabla ya Uhuru.

Kiwanda cha kubangulia zao hili cha kwanza kilikuwa Ndanda Mission kule Lindi kikipotea mzigo toka Sahare Mission Tanga. Kiwanda kingine kipo Rungwe kwenye shamba la Parachichi la Rungwe avocado pale juu ya Rungwe secondary ukishapita Moravian head Quarter.

Tatizo la macadamia ni ukuaji wake, growthrate ni ndogo sana, ila ukitumia grafted muda ni mfupi, changamoto ni kupata miche hiyo ya muda mfupi, bei ni kubwa kwa scale kubwa, bei ya jamaa wale wa Mbozi wenye kitalu ni Tsh 4000/ kwa mche. Kama unanunua mzigo mkubwa wanakuletea mpaka shambani kama uko pande za nyanda za juu kusini.
 
Ungeenda zaidi na kusema zinapatikana wapi kwingine kuwaelimisha wengine.
Tanzania nzima maeneo yenye ubichiubichi. ukienda bukoba/kagera, Dabaga Iringa, Tukuyu, Lushoto, maeneo mengi ya mkoa wa kilimanjaro, biharamuro etc. kwa wale walioishi maeneo hayo kama hawazijui karanga miti itakuwa ajabu.
 
wazungu hasa wamisionari ndio walizileta hizi. zipo maeneo mengi yenye umisionary wa kikatoliki na kilutheri. ukilimwa tu kwenye mission, inasambaa kijiji kizima na vijiji vingine waumini wanaenda kulima majumbani mwao. ila kama ni za gharama namna hiyo, basi yafaa zilimwe kuwatoa watz toka kwenye vyuma vilivyokaza.
 
Mkuu kama una Macadamia basi tuwasiliane.

Soko lipo ndugu yangu.
Mkuu nataka ingia with both feet maana niko na eka kama tano nataka tupia huu mmea maana ndo Pension yenyewe hii na inalipa kuliko hawa jamaa wa fao la kujitoa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom