Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Timtim

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
608
124
Cashew-Nut-.jpg


Naomba niwasilishe kutaka kuelezwa zaidi juu ya kilimo cha Korosho kwa Mkoa wa Pwani. Naomba mwenye kuelewa atufahamishe mimi na wengine gharama toka awali za kupanda mikorosho katika shamba la ekari 20. Gharama na takwimu hadi kuvuna na kiasi cha mavuno kwa mwaka.

Natanguliza shukrani zangu.

WADAU WENGINE WANAOHITAJI UELEWA WA KILIMO HIKI
Naomba niwasilishe kutaka kuelezwa zaidi juu ya kilimo cha Korosho kwa Mkoa wa Pwani. Naomba mwenye kuelewa atufahamishe mimi na wengine gharama toka awali za kupanda mikorosho katika shamba la ekari 20. Gharama na takwimu hadi kuvuna na kiasi cha mavuno kwa mwaka.

Natanguliza shukrani zangu
Habari ndugu zangu,

Nahitaji mawasiliano ya kituo cha utafiti cha NALIENDELE kilichopo kusini,ili nipate kujua taratibu za kupata miche ya mikorosho. Pia kama kuna mtu anayejua kuhusu upatikanaji wa mivhe ya mikorosho, upandaji wake naomba anisaidie.
Wanajamvi,

Nataka kuanzisha shamba la korosho la ukubwa wa 32 acres! Naomba wenye utaalaam na kilomo hiki wanijuze juu ya hatua muhimu za kuzingatia tukianzia na kusafisha shamba kwani kwa sasa ni msitu kabisa ambao haujawai limwa chochote.

Pili garama mbali mbali kwa kila hatua na any other information ambayo unadhani itanisaidia!

Natanguliza shukrani.
Katika pitapita zangu kwenye kata mbalimbali zilizopo Lindi, aisee nimejifunza kuwa watu wengi waliochukua miche ya korosho msimu huu hakika wamekwenda kuipanda katika mashamba niseme machafu au ambayo hayakuandaliwa vizuri!

Nadhani kuna haja ya elimu ya kutosha itolewe kwa wakulima juu ya maandalizi ya shamba hatua kwa hatua mpaka mche wa mkorosho unapopandwa.

Mengi ya mashamba hayo yanamilikiwa na watu waliopo mijini ambao wameweka vijana au mwanakijiji msimamizi ambae anatoa taarifa ya maendeleo ya shamba kupitia simu au picha za WhatsApp!

Ndugu zangu ambao mna interest ya kuwekeza katika kilimo hiki napenda niwakumbushe kuwa kazi ya kilimo hata siku moja haijawai kufanywa au kusimamiwa kwa simu.

Wengi wetu tumeweka mategemeo makubwa sana tukiwa na calculator zetu mezani tuki reffer ile bei ya 3970 kwa kilo times namba ya kilo kwa mkorosho mmoja times idadi ya ekari ulizoambiwa na “mfanyakazi/msimamizi” wako kule Lindi kuwa zimepandwa msimu huu.

Changamoto ni kubwa na kinachoendelea Lindi na maeneo mengine katu hayataweza kututoa hapa tulipo kama juhudi binafsi katika kusimamia uwekezaji huu hazitachukiwa!

Naomba magwiji wa kilimo hiki ambao wamejaa tele katika jukwaa hili watufundishe hatua mbali mbali za maandalizi ili kuokoa jahazi ambalo kwa mtazamo wangu tayari limeshageuzwa lilikotoka na linakaribia kuzama!!

“”NIISHIE HAPO KWA SASA””
Habari wana JF.

Naomba mwenye uzoefu au utaalamu wa zao la korosho anisaidie kujua mahitaji ya kuanzisha kilimo hiki. Nataka nitafute shamba(virgin land) kwa kilimo hiki, napenda nijue maeneo ambayo zao hili hustawi sana, mbegu bora ya muda mfupi, gharama za kuhudumia hadi kuanza kuvuna ikiwa ni pamoja na madawa, mbolea kama itahitajika na masuala mengineyo.

MICHANGO YA WADAU
USHAURI: MAANDALIZI NA UPANDAJI

Ndugu Hongera Tena kwa kuwa na kiasi hicho cha shamba kwani kama ukifanikiwa kupanda shamba lote unauhakika wa kuwa na miti sio chini ya elfu 3 ambacho ni kiasi kikubwa sana kwa kuanzia.

Nakushauri upande mikorosho iliyo bebeshwa kwani unaweza kupanda idadi kubwa kwenye shamba dogo pia inauvumilivu mkubwa wa magonjwa na inatoa mazao mapema.

Kwa kuandaa shamba ukisha safisha nivema kama mengi ni majani itakuwa vema kama ukiyachoma moto huwa inasaidia kuangamiza magojwa mbalimbali yaliyokuwa kwenye mimea hiyo ya mwanzo.

Umbali kati ya shimo na shimo unaweza kuweka kati ya mita 5-6 na umbali kati ya mstari unaweza kuweka mita 6-7

kwa vipimo hivyo unaweza kuwa na mashimo 100-120 kwa heka moja.

Na uchimbaji wa mashimo unaweza kuchimba sentimeta 50 kwenda chini na upana wa sentimeta 50, ni vema udongo wa juu nusu ya shimo yani sentimeta 25 ukautenga na ule wa chini wa sentimeta 25,Huu udongo wa juu utautumia kuchanganya na mbolea ya samadi wakati wa kupanda mmea.

Inashauriwa kupanda mmea wakati wa mvua na kabla ya kupanda changanya ule udongo na mbolea na kuacha kwa wiki mbili ili kuwezesha samadi kuchanganyika vizuri na udongo ndipo upande mmea.

Wakati wa kupanda unashauriwa kuweka ule udongo uliochanganya na samadi ujae robo ya shimo ndipo upande mmea wako na na wakati wa kufukia fukia nusu ya shimo kwa utaratibu huo utakuwa umefukia shimo lako na mmea kwa robotatu hiyo itasaidia kuacha eneo la maji kutuama wakati wa mvua au wakati wa kumwagilia na pia mmea kupumua vizuri.

Hii nimekupa picha kidogo juu ya maandalizi hayo ila nakushauri nenda Kituo cha naliendele Nimeweka post zake kadhaa hapa na anuani zake pale utapata maelekezo mengi juu ya magojwa na tiba zake kwakuwa mradi wako unaonekana ni mkubwa huna budi kufika pale.

Contact

Zonal Director (South),

Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),

10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.

Tel.: +255 732 934 035

Fax.: +255 732 934 103

e-mail: utafiti@iwayafrica.com

LUMUMBA

USHAURI: MATUMIZI YA ARDHI

Napenda kukuongezea ujuzi wa faida kidogo juu ya matumizi bora ya ardhi kuhusu kilimo mseto, iko hivi kipindi unasubiri mikorosho yako ya kisasa(hybride) ianze kutoa matunda ili upate faida takribani miaka 3-5 jaribu kupanda mahindi kwa kipindi cha misimu miwili ya mwanzo kwa hilo eneo lako ili lisipotee bure na hii itapelekea kupata faida ya zao moja under zero cost of production.

(a) gharama za uzalishaji
- Kulima ni bure kumbuka umelima kwa ajili ya korosho.

- Mbegu ni mifuko 128 kila ekari ni mifuko 4 na kila mfuko ni 12,000/=(1,536,000/=)

- Kupanda ekari moja maeneo mengi ni 30,000/=(960,000/=)

- Palizi hapa ni ile itakayotumika kupalilia mikorosho(bure)

- Sijaweka mbolea kwa sababu shamba kama ulivosema ni virgin.

Jumla ya gharama za uzalishaji/matumizi upande wa mahindi itakuwa ni Tshs 2,496,000/=

(b) Mapato
Ekari moja inatoa wastani wa gunia 8-10 chini ya uangalizi mzuri kwa mtu aliezamilia kama wewe,

Hivyo basi utapata magunia 256 kwa ekari 32.

Mapato/mauzo kwa sasa ni 60,000/= kwa gunia (15,360,000/=)

Utakuwa na faida ya 12,864,000/= kumbuka hii umelima msimu mmoja tu na nimesema ulime misimu miwili ya wawli maana mikorosho inakuwa bado ni michanga na itakuwa ni sehemu ya ulinzi wa shamba kwa mifugo na watu wanaokuzunguka hivyo. 12,864,000/=x misimu 2 (25,728,000/=).

Nakutakia kazi njema mkuu kwa haya maamuzi yako mazuri.

USHAURI: GHARAMA ZA USAFI

Garama za usafi zinategemea mambo makubwa matatu

1. Aina ya msitu/miti iliyopo

2. Mkataba unaoingia na wasafishaji kwa maana ya garama zipi zitabebwa na mwenye shamba na zipi zitakuwa za wasafishaji. (Hapa kuna mambo meeeeengiiii yakujadili)

3. Aina ya wafanyakazi unaowatumia. Utatumia wenyeji au wageni wanao toka mbali na eneo husika (Hapa kuna vitu vingi tena vya kuviangalia na changamoto zake)

Ila kwa kifupi garama zilizopo sokoni kwa sasa ni kati ya Tshs 280,000 hadi 320,000 kwa ekari moja ukiondoa garama ya kununua mashine (chain saw), vifaa vya kazi ikiwamo mapanga, tupa,na buti, kupiga mashimo, miche na kupanda.

Ila usiogope bro karibu sana.

KUANDAA SHAMBA, MBEGU, JINSI YA KUPANDA NA WADUDU WALETAO MAGONJWA

UTANGULIZI
Korosho ni zao la biashara ambalo chimbuko lake ni Ureno na baadae mnamo karne ya 16 ndipo lilipofika Afrika, katika nchi ya mozamboque na baadae likafika Kenya na Tanzania.

Tanzania zao la korosho ulimwa na kustawi vizuri katika pwani yote ya bahari ya Hindi kuanzia Mtwara mpaka Tanga, pia ipo mikoa mipya kamaTabora, Singida, Dodoma, Songwe, Rukwa huko kote zao la korosho linastawi vizuri mvua na Udongo.

Korosho hustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua 840mm - 1250 mm wastani wa mvua kwa mwaka, na pia hukua vizuri kwenye maeneo 0- 500 m kutoka usawa wa bahari.

Kutokana na kwamba samadi sehemu nyingi ni adimu, mbolea za viwandani zinafaa kutumika katika kupandia, husaidia kukuza haraka japo ukipanda bila mbolea miti inaota na utavuna kama kawaida ila tofauti ya kutumia mbolea husaidia kukua kwa haraka.

Mikorosho haihitaji maji kilasiku ukuaji hautakuwa mzuri ,kwa kipindi cha kiangazi umwagiliaji mzuri ni ndoo ya lita kumi kwa kila shimo kwa wiki moja inatosha sana,ila kama utakuwa una miche iliyofikia upana wa peni na ukapanda kipindi cha mvua na mche ukapata mvua kwa miezi 4-5 inatosha sana kuendelea kukua wenyewe.

Pia kama ni kipindi cha kiangazi unaweza kuzungushia mche na majani makavu kwa kuhifadhi unyevu. Korosho hukua vizuri kwenye maeneo yenye PH 5.6 udongo wa kichanga (sandy) na pia udongo mfinyazi kichanga.

MAANDALIZI YA SHAMBA
Korosho kama mazao mengine shamba linatakiwa kusafishwa, kusawazishwa nakutifuliwa vizuri kwaajili ya kupanda korosho.

Katika mashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya ngombe ukachanganya na udongo mapema ili kuongeza rutuba.

2242735_IMG-20191201-WA0082.jpeg

JINSI YA KUPANDA
Ni muhimu sana kuchagua mbegu bora kwakua mbegu utakayoipanda ndio itakuonyesha kiasi gani utavuna,

Baada ya kununua mbegu unachukua maji na chumvi 100g ya chumvi unaweka katika maji kiasi cha lita 5 unakoroga vizuri na unachukua mbegu zako unaweka kwenye maji hayo zile zitakazo zama ndio mbegu zenye uwezekano mkubwa wa kiota.

Kitaalamu hekari moja inatakiwa ichukue miche 25-27 ambapo ni space ya mita 12 urefu na 12 upana kwa mbegu za kienyeji. Kwa kilimo cha kisasa nikimaanisha mbegu bora za kisasa na kwa mpango wa upandaji bila kuchanganya na mazao mengine hekari moja inakaa mpaka miti 100 na mkorosho uliostawi vizuri unatoa kuanzia kilo 10-20.

Kwa hiyo unauhakika wa kuvuna kuanzia tani moja ya korosho kila heka ambayao tani moja sio chini ya milioni 3

Mikorosho ile ya kubebesha ya muda mfupi inaanza kutoa Korosho kuanzia miaka mitatu, Huwa wanasema miaka miwili au mmoja ni kweli ila unakuwa hauna nguvu, unashauriwa kutoa mau yote ili uweze kutengeneza matawi na kuwa na nguvu.

AINA ZA UPANDAJI MBEGU
Kupanda moja kwa moja. Hii ni njia mambayo ni hatarishi sana na inaitaji umakini kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa mbegu kufa. ukitumia njia hii unatakiwa kupanda mbegu tatu 3 katika shimo moja na baada ya miezi mi 3 - 4 ng’oa mimea na bakiza mmoja wenye afya na muonekano mzuri.

Njia ya kitaru

Hii ni njia ya pili na ni nzuri kwa sababu unakua huru kuchagua mche ambao umestawi na ulio na muonekano mzuri , unatakiwa kuamishia miche shambani ikiwa na umri wa wiki 6 na zingatia kuchagua mche wenye afya na baadae unatakiwa kupunguza majani urefu wa sm60- 90 kutoka kwenye ardhi na pia ondoa majani yote ambayo yanaonekana kuadhiliwa na magonjwa au wadudu.

MAGONJWA NA WADUDU

MAGONJWA

  • Anthracnose
  • Powdery mildew
Hayo ni baadhi ya magonjwa yanayo athiri sana korosho

WADUDU
  • Cashew stem girdler
  • Cashew weevil
  • Coconut bug
  • Heliotropes bug

KUZUIA NA TIBA
Ili kuweza kuzuia maagonjwa na wadudu unatakiwa kuzingatia yafuatayo:

Palilia mapema

Weka shamba katika hali ya usafi

Tumia mbinu ya kuchanganya mazao kwa korosho unaweza kuchanya pamba au maharagwe hiyo inasaidia kukimbiza wadudu wengine ambao wanakua hawapatani na mazao hayo

Tumia pesticide kutibu magonjwa na insecticide kuuwa wadudu wahalibifu.

Uwekezaji

Wengi wananunua mashamba yenye mikorosho then wanaindeleza kwa kupanda niche mipya,ambapo ikianza kuzaa kwa wingi ndipo hukata ya zamani.Ila kipindi hiki kuuziwa shamba la mikorosho ni shughuli ni sawa na kuuza kitalu cha madini.

images-1.jpeg

JINSI YA KUBEBESHA MICHE YA MIKOROSHO (GRAFTING)


Kwanza niwapongeze wadau wote mnaofatilia Kilimo cha korosho. "Thesis, kimpupu, "Mshuza2,, SUKAH, Gu Jike , ankai, Shark, Mndengereko One, Na wengine

Nime Post video 4 zinazoonyesha jinsi ya kubebesha miche ya mikorosho (grafting).Ukiangalia kwa vitendo inatosha,Kama una swali niulize.









LUMUMBA
 
Hii kitu hii!

Wameacha kukopa, kulipwa hela nusu, nyingine mpaka wakauze mzigo india? Mikorosho mizuri mbegu za india, inakua mifupi kama miembe ya kisasa, inazaa baada ya miaka 3, mazao yanaongezeka kadri ya matunzo na muda.
 
Heshima kwenu wakuu

Kutokana na bei ya korosho kukaa vizur nimepata wazo la kupanda mikorosho maeneo ya Rufiji.

Kwa anayejua idadi ya niche ya mikorosho kwa heka moja anisaidie na distance kati ya mche na mche ni mita ngapi?

Na pia nitumie mbegu gani nzuri ambayo hutoa mazao mengi mazuri.

Asante
 
Habari wajasiriamali.

Ni kijana mwenzenu ambaye ni mkulima wa korosho mkoani Mtwara wilaya ya Tandahimba. Kesho naenda kutembelea na kufanya farmer works na kurudi home.

Nitawajulisha nikifika. Inshaaalah

great thinker
 
Hiki tunaita kilimo cha SIMU!! Yaani unalima kwa simu, unapalilia kwa simu, unaweka mbolea kwa simu na unavuna kwa simu!! Kuwa makini mkuu kilimo ni uti uti wa mgongo wa taifa, hakiitaji ulelemama!!
Kulima sio lazima uwepo kila siku eneo la field.Huu ni mwaka wangu wa pili kulima hili zao. Last year nilipata mafinikio mazuri tu.

great thinker
 
Kulima sio lazima uwepo kila siku eneo la field. Huu ni mwaka wangu wa pili kulima hili zao. Last year nilipata mafinikio mazuri tu.

great thinker
Kwani linalimwa Mara 2 Mkuu? Ukilima mara moja si basi.
 
Hiki tunaita kilimo cha SIMU!! Yaani unalima kwa simu, unapalilia kwa simu, unaweka mbolea kwa simu na unavuna kwa simu!! Kuwa makini mkuu kilimo ni uti uti wa mgongo wa taifa, hakiitaji ulelemama!!
Mkuu umenikumbusha kipindi flani niliwahi lima kwa simu basi jamaa yangu ananambia twende tufike tushuhudie mie namwambia namwamini jamaa.

Nikampa mkwanja wa debe 4 animwagie mpunga heka 4 si akachukua mbegu zake (za hovyo ndo kamwagia) kuja kwenda umeota mbali na alilima hovyo majani yamejaa.

Basi namwomba ushauri jamaa yangu tufanyaje ananijibu twende town tumrushie jamaa mkwanja atamaliza kila kitu. Nilikuwa nakasirika sana. Tangu hapo lazima nifike sehemu nijionee.
 
Mkuu umenikumbusha kipindi flani niliwahi lima kwa simu basi jamaa yangu ananambia twende tufike tushuhudie mie namwambia namwamini jamaa.

Nikampa mkwanja wa debe 4 animwagie mpunga heka 4 si akachukua mbegu zake (za hovyo ndo kamwagia) kuja kwenda umeota mbali na alilima hovyo majani yamejaa.

Basi namwomba ushauri jamaa yangu tufanyaje ananijibu twende town tumrushie jamaa mkwanja atamaliza kila kitu. nilikuwa nakasirika sana. tangu hapo lazima nifike sehemu nijionee

Pole sana mkuu vipi uliacha au still unaendelea na kilimo.

great thinker
 
Mkuu umenikumbusha kipindi flani niliwahi lima kwa simu basi jamaa yangu ananambia twende tufike tushuhudie mie namwambia namwamini jamaa

Nikampa mkwanja wa debe 4 animwagie mpunga heka 4 si akachukua mbegu zake (za hovyo ndo kamwagia) kuja kwenda umeota mbali na alilima hovyo majani yamejaa.

Basi namwomba ushauri jamaa yangu tufanyaje ananijibu twende town tumrushie jamaa mkwanja atamaliza kila kitu. nilikuwa nakasirika sana. tangu hapo lazima nifike sehemu nijionee
Ilishanitokea hata mimi mkuu sina hamu na kilimo cha simu!!
 
Back
Top Bottom