SoC01 Kilimo cha kimkakati ili kuondoa upungufu wa mafuta ya kula nchini

Stories of Change - 2021 Competition

malunde_mc

Member
Jul 19, 2021
9
5
Kilimo cha kimkakati ni aina ya kilimo kinacholimwa kwa lengo la kuzalisha mazao yanayotosheleza mahitaji ya nchi na kubaki ziada.

Kwa miaka mingi sasa kumekuwa na tatizo la upungufu wa mafuta ya kupikia nchini.Ili kuondokana na tatizo hilo nchi inatakiwa kuanzisha kilimo cha mazao yafuatayo ili kuondoa tatizo la upungufu wa mafuta ya kupikia ili kuondoa mfumko wa bei pale bidhaa hii inapokuwa adimu.

Alizeti-Kama serikali itawekeza katika upatikanaji wa mbegu bora za alizeti pamoja na pembejeo zinginezo wakulima watashawishika kuzalisha zao hili kwa ari.Zao la alizeti lingefanywa kuwa kilimo cha kimkakati kwa kanda ya kati pamoja na kanda ya ziwa ambako limekuwa likifanya vizuri pindi linapolimwa hivyo naishauri serikali kupitia wakala was mbegu na taasisi za utafiti was mbegu TARI zitafiti na kutoa mbegu bora zitakazostawi katika kanda mbalimbali hapa nchini.

Michikichi-Kama nchi itawekeza na kufanya zao la mawese lisaidie katika kupatikana kwa mafuta ya kupikia nchini .TARI wana jukumu la kuzalisha mbegu bora zitakazotoa mafuta mengi na zao hili liboreshewa input na hamasa itolewe katika kanda ya magharibi.Malaysia walikuja nchini kuchukua mbegu za michikichi leo ndiyo wamekuwa wazalishaji namba moja wa mafuta ya kupikia yatokanayo na mawese duniani wamefanikiwa kwa sababu nchi yao iliwekeza na kulifanya kuwa zao la kimkakati sisi tumebaki wasindikizaji tu.

Karanga-Zao jingine ambalo limepewa kisogo ni karanga miaka ya nyuma kulikuwa kunazalishwa mafuta ya kupikia yatokanayo na Katanga sijui uzalishaji huo uliishia wapi.Viongozi wakuu was nchi pamoja na wizara zote tatu Kilimo,Viwanda na Biashara kila moja inapaswa kufanya jambo kwa namna yake ili kurudisha mafuta ya kupikia ya karanga .

Pamba
-Ni zao linaloekekea kufa kabisa siioni tena Dhahabu Nyeupe iliyokuwa inazalisha kipindi kile tunakua miaka ya 90 na mwanzoni wa 2000.Zao hili lilikuwa linadhalisha mafuta pia lakini naona hakuna anaejali viongozi wapo kimya wakulima wamechoka kwa sababu mbegu si bora hazistawi kama zamani halafu bei wanayolipwa kwa kilo ni mbaya sana inatia kichefuchefu inafika kipindi wanakopwa hii si sawa tutaendelea kulalamika sana kuhusu upungufu wa mafuta ya kupikia .Serikali wekezeni kwenye kuzalisha mbegu bora za pamba bei ya soko iwe nzuri.

Nimeangazia mazao manne ambayo Serikali na sekta binafsi zikishikiana kuyafanya kuwa ya kimkakati tatizo la ukosefu wa mafuta ya kupikia litakuwa historia.Kama kutakuwa na mbegu bora na wakulima wakakopeshwa pembejeo au kuuziwa kwa being nafuu pamoja na kuwepo kwa masoko ya uhakika yenye being nzuri nchii hii haitatumia pesa za kigeni kuagiza mafuta ya kupikia.

Naomba kuwasilisha.
Wasaalamu,
Mathew Malunde.
Ushetu.
KILIMO CHA KIMKAKATI KITAONDOA TATIZO LA UPUNGUFU WA MAFUTA YA KUPIKIA NCHINI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom