Kilimo cha fenesi, changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo

mullaX

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
312
97
1600612024996.png

1479452007765.png


Hatua za kufuata unapotaka kulima fenesi
Mmea wa fenesi unaweza kustahimili viwango vya juu vya joto na baridi. Mfenesi uliokomaa unaweza kustahimili joto la hadi digrii 48 na baridi ya hadi digrii 0. Baadhi ya mifenesi hukua hadi urefu wa futi 100, lakini pia kuna aina zingine ambazo hukua hadi urefu wa futi 10-20.

Mti huu unaweza kuzaa matunda kwa zaidi ya miaka 100. Ni mmea wa kipekee kwani kati ya matunda yote duniani, ndio unazaa matunda yenye uzani wa juu zaidi wa kilo 50.

Kwa nini upande mifenesi?

Huu ni uwekezaji wa muda mrefu labda kwa maisha yako yote. Sehemu zote za mmea huu zina manufaa tele. Pia ni mti unaoweza kumpa mkulima kivuli nyumbani na kuwapa ndege makao. Mfenesi mmoja unatosha kuwapa matunda kijiji kizima huku pia ukikupa hela.
Miche ya mfenesi inaweza kutengenezwa kutokana na vipandikizi lakini mbinu hii imewapiga chenga wakulima wengi. Hivyo, mbinu ya kukuza kutokana na mbegu huwafaa wakulima wengi. Unatakiwa kuteua mbegu kubwa kutokana na fenesi lililoiva vizuri na kuziosha kwa maji yenye kiwango kidogo cha joto.

Sasa unaweza kupanda mbegu hizo katika kitalu kisha kuhamisha miche shambani. Unaweza pia kununua miche kutoka kwa wapanzi wa miche, ila watapatikana katika maeneo ya Pwani ya Kenya na pia kaunti ya Kakamega hasa mjini Mumias.
Iwapo uko mbali na maeneo haya unaweza kumtuma mtu akununulie fenesi lililoiva vizuri ili baadaye upande mbegu zake na kukuza miche yako mwenyewe.

Chagua eneo pana lililo wazi na linalopata jua kwa wingi, ondoa magugu na uchimbe shimo. Ili kuhakikisha maji yanapenyeza bila matatizo, changanya mbolea ya kawaida, majani, changarawe na mchanga wa shamba lako na kutia mle shimoni.

Sasa unaweza kupanda mche mmoja wenye afya nzuri ndani ya lile shimo. Nyunyizia maji na ufunikwe kwa nyasi ili kuzima unyevunyevu kuyeyuka kwa hewa.

Kama unapanda mche uliopandikizwa, usifunike majani yake ya juu maanake mmea utaoza kutoka ndani na kukauka. Tenganisha mimea kwa mita 10 kwa 10.

Umwagiliaji na uwekaji mbolea
Mfenesi hukua vizuri katika maeneo yenye joto ambayo hupata mvua ya kutosha. Hii inmaanisha utahitajika kuunyunyizia maji kila mara sababu unahitaji mazingira yenye unyevunyevu na mchanga laini. Hata hivyo, epuka kunyunyizia maji kupita kiasi hasa katika miaka yake miwili tangu kupanda.

Mara moja kwa mwaka, hasa mwanzoni wa mwezi Julai au Agosti, ongeza mbolea ya zizini kwa mmea ili kuupa nguvu. Unaweza kutia fatalaiza iliyosawzishwa, mara mbili kwa mwaka. Ukifikisha miaka mitatu, unaweza kutia fatalaiza ya kiwango cha 8:3:9.

Weka nyasi kuzingira mmea wakati baridi imekaribia kufikia kiwango cha digrii 0 ili kulinda mizizi ndidi ya baridi hiyo. Mara kwa mara ondoa matawi ya ziada kuhakikisha urefu wake umesalia kuwa futi 20.

Wakati mmea umezidisha urefu wa futi 12, kata upande wa juu wa shina lake hadi futi 8 ili kuuwezesha kupata matawi mengi. Mfenesi hukomaa baada ya miaka 3-6. Katika wakati huu, mfenesi ukichanua maua ya kwanza, yaondoe ili uendelee kukua.

Mara moja kwa mwezi ondoa magugu yaliyo karibu na mmea kwani yataanza kutumia madini muhimu yanayohitajika na mmea huu.

Funika eneo la mizizi kwa nyasi wakati wa kiangazi ili kuhifadhi unyevunyevu na kuepuka magugu kumea.

Kati ya miaka 3-6 baada ya kupanda (kutegemea na utunzaji na mazingira uliyopanda) mfenesi huanza kuchanua maua na baada ya miezi 2-3, mafenesi madogo ya rangi ya kijani kibichi yanaweza kuchumwa kutumika na wapishi.

Matunda yaliyokomaa huwa tayari kuvuna baada ya miezi 4-5 tangu maua yachanue. Wakati huo mafenesi huwa na harufu ya kupendeza na ngozi yake hubadilika kutoka kijani kibichi kuwa manjano.

Mfenesi huzaa matunda nyakati zote za mwaka ila katika maeneo mengi duniani, linavunwa sana katika msimu wa kiangazi
Baadhi ya wadudu wana mazoea ya kuvamia mfenesi na kuyatoboa mashimo yakiwa mtini huku pia nao ndege wakifurahia maji yake matamu na kuharibu matunda.

Wadudu wanaotoboa mashimo huathiri sehemu zote za mmea, lakini ukiwapulizia dawa ya kujitengezea nyumbani isiyo na kemikali huweza kuwaua na kuwazuia. Pia kuufunika mmea wakati matunda yamekomaa kutasaidia kukinga matunda dhidi ya ndege hatari.

Mdau anaetaka kujua kilimo cha fenesi
Habari wadau, kuna tunda moja maarufu maeneo ya kanda za pwani linaitwa FENESI. Hivi tunda hili linaitwaje kwa Kiingereza na asili yake wapi hasa? Yaan lililetwa na wakoloni au namna gani?


Michango ya wadau kuhusu kilimo cha fenesi

Unaweza ukawa mmoja kama mm ambaye nilikuwa nahisi/najua kuwa tunda la fenesi halina faida lolote wala wazungu/wanasayansi hawalifahamu basi tunajidanganya.

Leo nimejikuta tu nafanya research za tunda hili kwakuwa nowadays zimejaa mjini na zinaliwa kweli, ndipo nilipoanza kugoogle nikakuta faida na hata hilo jina la lugha ya malkia (jackfruit) na nchi zilizoorodheshwa zinalimwa sana ni africa kwa ujumla southern america na india nahisi ni hali ya kigeografia zaidi.

Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.

Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutubisho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuzi.

Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu. Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha.

Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya potassium yanayosaidia kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.

Wataalamu wa mambo ya afya wamezitaja faida nyingine za tunda hili kuwa ni pamoja na:

Kinga: Fenesi ni chanzo kizuri cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.

Nishati: Ni tunda salama kiafya, halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake huchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.

Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.

Asthma: Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.

Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini.
 
The jackfruit (Artocarpus heterophyllus), also known as jack tree, jakfruit, or sometimes simply jack or jak)[6] is a species of tree in the Artocarpus genus of the mulberry family (Moraceae). It is native to parts of South and Southeast Asia, and is believed to have originated in the southwestern rain forests of India, in present-day Kerala, in Tamil Nadu (in Panruti), coastal Karnataka and Maharashtra.[7] The jackfruit tree is well suited to tropical lowlands, and its fruit is the largest tree-borne fruit,[8] reaching as much as 80 pounds (36 kg) in weight, 36 inches (90 cm) in length, and 20 inches (50 cm) in diameter.[9]

Sosi: WIkipedia
 
Kivipi mkuu, tia nyama kidogo!
Zinakuwa na unga unga fulani na kunukia unapozila baada ya kuchemshwa.

Kama hujawahi, jaribu utakuja niambia ila hakikisha zinaiva vinginevyo zikiwa hazijaiva vizuri unaweza umwa tumbo
 
The jackfruit (Artocarpus heterophyllus), also known as jack tree, jakfruit, or sometimes simply jack or jak)[6] is a species of tree in the Artocarpus genus of the mulberry family (Moraceae). It is native to parts of South and Southeast Asia, and is believed to have originated in the southwestern rain forests of India, in present-day Kerala, in Tamil Nadu (in Panruti), coastal Karnataka and Maharashtra.[7] The jackfruit tree is well suited to tropical lowlands, and its fruit is the largest tree-borne fruit,[8] reaching as much as 80 pounds (36 kg) in weight, 36 inches (90 cm) in length, and 20 inches (50 cm) in diameter.[9]

Sosi: WIkipedia

Asante sana na pia umekuwa muungwana kutuwekea source yako..wengine wangesema source ni wao wenyewe..
 
hiyo ni dalili ya njaa jamani vitu vingine hata kama sio sumu haviliwi we tangu lini mbegu za fenesi zikaliwa

Zinaliwa sana tu. Waulize Wazaramo, Wandenge, Wanyagatwa na baadhi ya watu wa Kilwa kandokando ya bahari.
 
Kiboko zaidi ni ukizichoma hizo mbegu. Ni tamu sana na laini kama kiazi ila kuwa mwangalifu wakati wa kuchoma zikiiva wakati mwingine hupasuka na kutoa sauti kama ya mlipuko, sasa kama ulikuwa unasonga ugali kwenye jiko la kuni ukaweka mbegu mbili tatu kwenye moto ili uendee kugonga mdogomdogo ikipasuka hata moja ugali wote lazima ujae majivu na michanga na kama mwoga unaweza toka nduki vilevile
 
Zinaliwa sana tu. Waulize Wazaramo, Wandenge, Wanyagatwa na baadhi ya watu wa Kilwa kandokando ya bahari.
Maeneo yote umetaja ya wavivu. mikoa ya kagera,kilimanjaro au mbeya hawawezi kula hayo makitu,we imagine muhaya mwanaume hali ndizi mbivu sembuse mbegu za fenesi ahahahaha
 
The jackfruit (Artocarpus heterophyllus), also known as jack tree, jakfruit, or sometimes simply jack or jak)[6] is a species of tree in the Artocarpus genus of the mulberry family (Moraceae). It is native to parts of South and Southeast Asia, and is believed to have originated in the southwestern rain forests of India, in present-day Kerala, in Tamil Nadu (in Panruti), coastal Karnataka and Maharashtra.[7] The jackfruit tree is well suited to tropical lowlands, and its fruit is the largest tree-borne fruit,[8] reaching as much as 80 pounds (36 kg) in weight, 36 inches (90 cm) in length, and 20 inches (50 cm) in diameter.[9]

Sosi: WIkipedia

Asante sana mkuu, mi mtu wa uswazi huku. Kuna jamaa alisema fenesi ni tunda la porini tu halina tofauti na ile mizizi wanayokula Wamakonde (wanaita ming'oko) yaani watu hula tu kwa kuforce kwa kufuata mazoea ila si chakula maalum. Akadai ndio maana halina jina Kiingerezani. Na elimu yangu yote sikupata kujua hasa laitwaje kwa Kiingereza. Umenifungua macho, asante sana.
"Kitu kama sikijui nitoe ushamba kwa sekunde kisha, I'm a Professional" fid Q-I'm a professional.
MullaX, Mbagala.
 
Back
Top Bottom