Kilimo cha bustani njia rahisi ya kutatua ukata wa fedha katika familia

TEK

Senior Member
Jul 13, 2015
184
34
Habari zenu ndugu zangu, katika kutafakari nini cha kufanya nimejikuta napata wazo hili ambalo kimsingi kwa mtu ambaye atazingatia itamsaidia.

Hii ninazungumza kutokana na uzoefu nilionao katika maisha yangu. Mwaka 2016 ni mwaka ambao kwangu ulikuwa ni mgumu sana lakini kutokana na kilimo cha bustani ambacho nilianzisha wakati huo nilipata suluhu ya mambo mengi sana na hapa nimeona ni vema nilete na kwako kama ukivutiwa nami utapata kazi rahisi na nyepesi inayoweza kukufanya ujipatie fedha za kujikimu na familia.

Kilimo cha bustani ni kilimo hasa kinacholimwa wakati wa kiangazi kikitemea sana umwagiliaji. Kinafaa sana kwa watu wanaoishi katika mabonde na maeneo yenye maji yasiyotuama.

Unachotakiwa kuwa nacho ni mtaji kidogo wa kuanzia na hapa inategemeana na eneo ulilopo, nilipo mimi unahitaji kuwa na fedha kama laki na nusu hivi kwa kadirio la juu. Gharama hizi ni kwaajili ya kukodia shamba na kuanza hatua za awali kama kulima na mbegu.

Unachotakiwa kuzingatia ni kutumia nguvu nyingi zaidi kwako wewe mkulima kuliko kuajiri vibarua.

Mimi nilipoanza kulima bustani nilijitahidi sana kulima mwenyewe na kusimamia pia kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa. Mboga ni mradi ambao unahitaji muda mfupi sana tangu kuanza hadi mavuno.

Kila mtu anahitaji mboga hivyo ukilima mboga wateja kupata siyo tatizo sana isipokuwa kwa wale waliokaribu na taasisi kama vyuo, shule n.k tafuta masoko huko maana taasisi huwazinanunua mzigo mkubwa tena wanalipa kiasi kikubwa kwa mara moja.

Karibu tushirikiane kutatua matatizo yetu
 
Unalima mazao gani mkuu una muda gani vp kuhusu mafanikio uliyopata kutokana na hiyo bustani asante karibu ijibu
 
Back
Top Bottom