Kilimo cha Alizeti (Sunflower): Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

Kwa upande wa hali ya hewa ukanda huo zao hili linaweza kustawi. Kama Mzenga zao hilo halijawahi limwa nakushauri jaribia kwanza ulime eneo dogo maana hali ya hewa na udongo vinaweza kuwa toshelevu kwa zao lakini kukawa na matatizo mengine tusiyoyajua, kwa mfano uwepo wa wanyama kama panya, ndege na nyani (ngedere) hawa huwa ni kikwazo sana! Kwa vyovyote vile hata kama una nguvu na uwezo msimu wa kwanza jaribu ufanye kama kujaribia! Vinginevyo mazingira ya mzenga ni mazuri tu.

Wakuu naombeni mnisaidie kitu kimoja,je kuna anaejua gunia moja la alizeti linatoa lita ngapi za mafuta!asanteni
 
Wakuu naombeni mnisaidie kitu kimoja,je kuna anaejua gunia moja la alizeti linatoa lita ngapi za mafuta!asanteni
Gunia moja la alizeti ni huwa ni jepesi mfano wa pamba, huchezea karibu na kilo 55, na wingi wa mafuta hutegemea na aina ya alizeti na mazingira iliyotunzwa shambani pia inategemea ufanisi ya mashine ya kukamulia! Gunia moja la alizeti mara nyingi tarajia mkamuo wa lita 20 hadi 25. Alizeti aina za Hybrid zinaweza kufika lita 30! Lakini unajua kuwa faida ya Alizeti iko kwenye kuuza mashudu?? Usiishie kupigia hesabu ya mafuta tu, mashudu ni BONUS!

Wengine mnaweza kusahihisha au kuongezea zaidi!

 
Gunia moja la alizeti ni huwa ni jepesi mfano wa pamba, huchezea karibu na kilo 55, na wingi wa mafuta hutegemea na aina ya alizeti na mazingira iliyotunzwa shambani pia inategemea ufanisi ya mashine ya kukamulia! Gunia moja la alizeti mara nyingi tarajia mkamuo wa lita 20 hadi 25. Alizeti aina za Hybrid zinaweza kufika lita 30! Lakini unajua kuwa faida ya Alizeti iko kwenye kuuza mashudu?? Usiishie kupigia hesabu ya mafuta tu, mashudu ni BONUS!

Wengine mnaweza kusahihisha au kuongezea zaidi!




Mkuu Kubota; i salute you,yaani upo deep kweli kweli na masuala haya,ukweli unatoa darasa la kutosha hapa jukwaani,ni kweli kabisa hata mimi niliuliza sana juu ya gunia la alizeti linatoa ujazo gani wa mafuta nikaambiwa kama ulivyotaja wewe yaani 20 to 25,nikaambiwa pia kua mara nyingi mashineni uwa wanaweza kukushauri wakukamulie bure na uwaachie mashudu,ila nikashauriwa pia ni bora uingie gharama ya kulipia kukamua kuliko kuachia mashudu,maana mashudu yanalipa mara mbili ya bei ya kukamulia!kifupi nilichogundua alizeti inalipa zaidi kama ukikamua na kuuza mafuta na mashudu mwenyewe,kuliko kuuza alizeti kama mbegu!vipi kuhusu zao la ufuta?je una idea nalo mkuu?
 
Chonde chonde kaka ukibahatika kupata mchanganuo tushirikishe na sisi.

Wadau nimejaribu kumpata mdau mmoja na amenipa mchanganuo wa juu juu kuhusu gharama za zao ili!kwanza kwa mkoa wa Morogoro kama hauna shamba lako mwenyewe itakubidi kukodisha,na kwa heka moja ya kukodi ni kati ya 15,000/= mpaka 25,000/=, Pili kuna gharama za kuandaa shamba,kupalilia,kununua mbegu,kutunza shamba na kuvuna gharama zake roughly ni kama 110,000 hv kwa heka moja,ukipeleka zao lako kukamua mashineni ni 150/= kwa kilo na gunia moja lina kilo kati ya 55 mpaka 60,ukiamua kukamua tu na kuwaachia mashudu wenye mashine basi wanakukamulia bure,sijajua mashudu inauzwa kiasi gani kwa kilo,labda wadau wengine waje kutusaidia,na anasema kua mara nyingi gunia moja la alizeti utoa 35kg mpaka 40kg za mashudu!si vibaya wadau wengne wakija kutusaidia juu ya uhakika wa soko la mafuta ya alizeti na bei zake pia
 
Wadau kitu chochote unapoamua kuingia unatakiwa uingie ukiwa hauna shaka,ukishakua unawaza mara hv,mara vile hauwezi fanya jambo ilo kwa ufanisi,wathubutu(risk takers) ndio always wanaofanikiwa katika mambo yao!kilimo hakimtupi mtu,kikubwa ni ufuatiliaji na matunzo,kilimo cha alizeti hakina complications sana kama baadhi ya mazao,kilimo hiki hakihitaji mvua sana,so ni wazi kua ni rahisi sana kujua wakati muafaka wa kupanda alizeti,mavuno ya alizeti mara nyingi utegemeana na aina ya mbegu,udongo wa eneo husika na matunzo hasa wadudu waharibifu kama ngedere,panya etc,ila kwa heka moja ya alizeti kwa mkulima anayejua nini anafanya,msimu ukiwa mbaya sana atavuna gunia 8 kiwango cha chini,ila mara nyingi uwa inacheza 12 mpaka 15,na wakati mwingine waweza pata hata guni 17,alizeti ni kilimo kizuri kwa wale wenye nia hasa ya kupata kipato na kuwekeza zaidi kwenye kilimo,maana alizeti demand yake ni kubwa mno ndani na nje ya nchi,ni vizuri sana kufanya kitu ukiwa na long term target!nchi ni tajiri hii,tuwekezeni kwenye kilimo vijana wenzangu
 
Nimeyapata haya maoni kwa wadau fulani humu JF :

Mimi tangu nilipotembelea maonyesho ya kilimo kwa mara kwanza miaka miwili iliyopita nimegundua ni kwa kiasi gani tumekuwa na mtazamo hasi wa kudharau kilimo na wakati mwingine tukikimbilia kazi za ofisini kwa woga wetu wa maisha!

Tuko pamoja naomba tushirikiane kwa hilo TUPO wengi ktk hii safari ya Malila.
imagine kijiji kina wakulima wenye upeo wa kutumia internet,research on market and prices via intaneti
 
ninavyo jua Alzeti inastawi maeneo mengi yanayo limwa Mahindi na ni maeneo yasiyokuwa na Baridi sana make alzeti na Baridi havipatani na kwa uzalishaji inategemeana na aina ya Mbegu make ni kama mahindi kuna aina za kutosha za alzeti
 
Mzinga

Wewe katika mada hii ndiye muhusika mkubwa kabisa .... naomba utusaidie sana katika kutuelekeza .... nitakuwa na maswli kadhaa hivi ... naomba usichoke

naomba unijulishe aina ya mashine hiyo ya kichina uliyoitaja yaani (105) ni model gani, brannd gani .... ina motor ya KW ngapi .... na ni ya capacity ya ukamuaji wa tani ngapi kwa siku .... pia je mashine hii ina filter inbuilt au ipo tofauti?

nitashukuru kwa info

ahsante

Mzinga mkuu ebu njoo utupe data tunahitaji maelezo yako uku...
 
Last edited by a moderator:
Mashine zinapatikana sido na kwa wahindi. Nimemnunulia mjombangu mashine moja kwa milioni nane pamoja na filter ina mabomba kumi na mbili. Igembe Nsabo nisaidie, Unauza lita ishirini za mafuta kwa bei gani. Nadhani bei ya shilingi 2,500 kwa lita itakupa shilingi elfu hamsini kwa lita 20. Naogopa kidogo, Kuhusu kulima wengi wanalima kwa njia za asili. Ukilima kitaalam, utapata tani nne za alizeti kwa ekari moja. Huende ukishirikisha wataalaam utalima kwa faida. Mimi nimefanya utafiti wa kilimo cha mpungu cha umwagiliaji. Ekari moja gharama yote ni shs 300,000. Mavuno ni magunia 40 minimum. Una uhakika wa kuuza shs 2,500,000 kwa ekari moja. Kilimo ni ukombozi ni vizuri tunaopenda kilimo tulime sehemu moja ili kupunguza gharama. Tuchangie gharama za mtaalam, gharama za kusafirisha pembejeo na hata usafiri wetu wa kwenda na kurudi shamba.

Safi sana

Hapo kwenye mpunga nimependa!
 
Ktk hili la kutafuta mashine, naomba ikiwezekana kila aliye karibu na mashine hizi ajaribu kupata aina za mashine zilizopo hapo. Kutokea hapo tunaweza kupata aina za mashine zinazopendwa zaidi( hatimaye tutapata sifa/siri ya hizo mashine).

Nipendekeze kitu hapa, kama una-plan ya kuingia ktk usindikaji wa mazao kama alizeti/ufuta, ni vizuri kujua proper location za siku zijazo hasa kwa sisi tulio hapa Dar.

Naamini Chalinze/Mdaula/Moro surbubs/Lugoba/Mlandizi ni maeneo mwafaka ili kuwa karibu na wakulima.

Hivi ufuta unalimwa hapo maeneo ya Chalinze mkoa wa pwani? unastawi?
 
Habari zetu wakuu ningependa kuuliza juu ya kilimo cha alizeti je ukiwekeza katika kilimo hiki kinalipa?
Na vipi kuhusu masoko yake? Msaada wa mawazo kuhusu kilimo hiki wakuu
 
mimi sifahamu chochote kuhusu kilimo cha alizeti,ninachofahamu ni kwamba MUZAR OIL walitoa tangazo kwamba wana uwezo wa kununua alizeti yote inayolimwa na wakulima wa nchi hii.Kazi ni kwako
 
Unataka kuwekeza mkoa gani? Kwa ufahamu wangu mimi alizeti ni zao bora sana ukiachana na swala la soko hata wewe mwenyewe unaweza ukazalisha mafuta kama kwa Dsm bei ya sasa dumu la lita tano ni elfu kumi na saba wewe wekeza kwa speed zote zao la alizeti ni zuri sana
 
Habari zetu wakuu ningependa kuuliza juu ya kilimo cha alizeti je ukiwekeza katika kilimo hiki kinalipa?
Na vipi kuhusu masoko yake? Msaada wa mawazo kuhusu kilimo hiki wakuu

Ni biashara nzuri sana, japokuwa inapendeza kama unalima in large scale. Soko lake lipo kubwa sana tena siku hizi watu wengi wanaanza kuyatumia, jipange karibu kwenye gemu, njoo moro tulime mkuu
 
kwenye hali zote za hewa linastawi, iringa , mbeya , morogoro, njombe. Hizi sehemu tajwa zote niza hali ya baridi na joto, hivyo mkuu wewe wa tabora jipange tu hata huko wawezalima alizeti.
 
kwenye hali zote za hewa linastawi, iringa , mbeya , morogoro, njombe. Hizi sehemu tajwa zote niza hali ya baridi na joto, hivyo mkuu wewe wa tabora jipange tu hata huko wawezalima alizeti.
Ahsante mkuu wangu, je zao hilo lahitaji pembejeo pia kama vile mbolea, madawa kupulizia ama nawezaje kulimudu?
 
Back
Top Bottom