Kilimo cha Alizeti (Sunflower): Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

Mkuu naomba na mimi nitoe mchango wangu kwa kwa kile ninachojua kwenye hili zao.Binafsi nina mashine ya kukamulia alizeti 118 ni ya kichina hii mashine kwani kipindi zimetoka hizi mashine ndo zilikuwa chaguo la wafanyabiashara wengi sana waalizeti.

Lakini kilochokuja kutukumba wengi wetu ni ughali wa spea za mashine yenyewe na hata gear box zikaanza kutusumbua sana.

Sasa tukaje na solution ya kubadilisha gear box tukaweka mapaja ya trekta ili kutatua tatizo.Hilo zoezi wengi tulifanikiwa licha ya gharama ya zoezi zima kuwa kubwa sana.

Kikajitokeza tatizo jingine hasa hasa kwa wateja wanaotaka kukamuliwa wakawa wanailalamikia hii mashine kwamba sio nzuri inawakata sana kwenye mafuta.Ijapokuwa kukata kwa mafuta kuna sababu nyingi achilia mbali mashine yenyewe.

Sasa kwa sisi wafanyabiashara ambao tunawakamulia vile vile wenye mbegu zao ikawa ni tatizo jengine.Watu wakaja na mashine 105 kwamba ndo nzuri na hai kati mafuta na ndo wengi wakamuaji wakawa wanataka mashine 105 ili wakamulie hapo na ndo inayotumika mpaka sasa hivi kwa wakamuaji wengi.

Hii ndo historia fupi ya hizi mashine za alizeti kuhusiana na mashine za SIDO kwa kweli sijawahi kuziona na sidhani kama zinauwezo sana wakufanya kazi kubwa sana kama hizi za kichina.

Huu ndo mchango wangu kwa upande wa mashine.Nitarudi kuzungumzia bei ya alizeti na soko lake.
 
Wakuu TEMDO arusha wanahizo mashine/wanacontact za wauzaji/wanatoa ushauri wa kitalamu wa aina gani ya mashine ni nzuri hasa hizo za INDIA, kwa sasa siko Arusha ila kwa alie Arusha anaweza kwenda kuwa ona TEMDO wako NJIRO ila nikirudi Arusha nitaenda kuwacheki na nitawaletea FEED BACK
 
Mkuu naomba na mimi nitoe mchango wangu kwa kwa kile ninachojua kwenye hili zao.Binafsi nina mashine ya kukamulia alizeti 118 ni ya kichina hii mashine kwani kipindi zimetoka hizi mashine ndo zilikuwa chaguo la wafanyabiashara wengi sana waalizeti.

Lakini kilochokuja kutukumba wengi wetu ni ughali wa spea za mashine yenyewe na hata gear box zikaanza kutusumbua sana.

Sasa tukaje na solution ya kubadilisha gear box tukaweka mapaja ya trekta ili kutatua tatizo.Hilo zoezi wengi tulifanikiwa licha ya gharama ya zoezi zima kuwa kubwa sana.

Kikajitokeza tatizo jingine hasa hasa kwa wateja wanaotaka kukamuliwa wakawa wanailalamikia hii mashine kwamba sio nzuri inawakata sana kwenye mafuta.Ijapokuwa kukata kwa mafuta kuna sababu nyingi achilia mbali mashine yenyewe.

Sasa kwa sisi wafanyabiashara ambao tunawakamulia vile vile wenye mbegu zao ikawa ni tatizo jengine.Watu wakaja na mashine 105 kwamba ndo nzuri na hai kati mafuta na ndo wengi wakamuaji wakawa wanataka mashine 105 ili wakamulie hapo na ndo inayotumika mpaka sasa hivi kwa wakamuaji wengi.

Hii ndo historia fupi ya hizi mashine za alizeti kuhusiana na mashine za SIDO kwa kweli sijawahi kuziona na sidhani kama zinauwezo sana wakufanya kazi kubwa sana kama hizi za kichina.

Huu ndo mchango wangu kwa upande wa mashine.Nitarudi kuzungumzia bei ya alizeti na soko lake.

Mzinga

Wewe katika mada hii ndiye muhusika mkubwa kabisa,naomba utusaidie sana katika kutuelekeza nitakuwa na maswli kadhaa hivi.Naomba usichoke

Naomba unijulishe aina ya mashine hiyo ya kichina uliyoitaja yaani (105) ni model gani, brannd gani ,ina motor ya KW ngapi .... na ni ya capacity ya ukamuaji wa tani ngapi kwa siku pia je mashine hii ina filter inbuilt au ipo tofauti?

Nitashukuru kwa info.

Ahsante.
 
Na kuna hii kampuni ya Kenya nao wanakuwa na Mashine nzuri sana za Kukamua alzeti na zinalenji kwenye milioni 4 ikiwa complete, wacheki na sales@marinakenya.com
Binafsi nashukuru sana Mkuu, nimekuwa interested sana na hii biashara. Kule kwetu kuna alizeti za kutosha na msimu wake ni huu. Nafikiri huu sio wakti wa kulala na kusubiri wajomba
 
Wadau habari!nakuja hapa jamvini kwa mara nyingine tena kuomba ushauri wenu juu ya jambo ambalo liko kichwani mwangu!mimi niliamua kujiajiri baada ya muda mwingi wa kusaka ajira bila mafanikio!nimejaribu vitu kadhaha wa kadhaha vingine vimefanikiwa vingine vimegoma,nilichokua naomba ushauri kwa siku ya leo ni juu ya wazo langu la kilimo cha alizeti mkoani Morogoro!nilikua naomba ushauri kwa wale wenye kujua juu ya ilo,1: Je Alizeti katika mkoa wa Morogoro yaweza stawi vizuri katika maeneo kama Gairo,Dumila,Kilosa na Mikese? 2: Je ni wakati gani mzuri wa kupanda alizeti? 3: Je ni kiwango gani cha mvua chahitajika ili kuweza stawisha Alizeti? 5: Na mwisho je heka moja ya Alizeti inaweza toa gunia ngapi za alizeti!natanguliza shukrani wadau,maana nina amini ukiomba ushauri hapa JF basi utaondoka na wingi wa manufaa!asanteni
 
Mkuu kwa alizeti sehemu hizo zoe ulizotaja inastawi,na mbegu nzuri ni records kuhusu wakati wa kupanda,wakati mzuri ni pale masika inapoelekea mwishoni,maana alizeti ahiitaji mvua nyingi,na kuhusu heka moja kutoa gunia ngapi,hapo sina uhakika,labda waje wadau wengine watupe somo
 
Ni kweli mheshimiwa Kapuku: tarehe ya kupanda lazima ujue alizeti yako huchukua siku ngapi hadi kuvuna ili upande iweze kukomaa wakati kipindi cha mvua kimeshaisha. Alizeti ikikomaa huku mvua bado inanyesha vichwa vyake huoza.

Kuna imani kwamba alizeti iliyochelewa kupandwa huwa na mafuta mengi! Yawezekana ikawa na mafuta mengi kwa gunia moja lakini mavuno kwa shamba zima yakawa kidogo kiasi kwamba wingi wa mafuta kwenye hayo mavuno kidogo hauwezi kuzidi alizeti yenye mafuta kiasi lakini yenye mavuno makubwa.

Pamoja na kwamba alizeti inastahimili ukame lakini inahitaji mvua za kutosha pale zinapoweza kupatikana! Cha kuepuka ni isije ikakomaa huku mvua bado zinaendelea! Morogoro Mvua za kupandia alizeti ni za mwezi February mwishoni na mwezi wa March mwanzoni! Ukitaka alizeti yenye mafuta mengi panda mwezi wa April lakini utapata mavuno kidogo! Alizeti iliyositawi wastani wa mavuno ni magunia 15 ingawa wakulima wengi wanaishia gunia 8 hadi 10 tu kwa ekari moja.

Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro walishaachana na mbegu ya aina ya Record siku nyingi, kuna alizeti fupi toka Kenya zinazaa sana na zina mafuta mengi. Pia kuna alizeti Hybrid nazo ni fupi na mambo yake ni makubwa! Kama umepania kujichimbia kwenye kilimo cha alizeti anzia na Record lakini ukipata fursa ya kuwasiliana na mikoa ya Kaskazini ulizia mbegu za kutoka Kenya utaona vitu vyake! Tanzania utafiti wetu unasua sua sana kiasi kwamba toka iwepo mbegu ya Record hawajatoa mbegu nyingine, Record imepitwa na muda, haina mavuno makubwa wala haina mafuta mengi kama mbegu maarufu ambazo zinapatikana mikoa ya Kaskazini!

Pia lazima ikumbukwe kuwa alizeti hukubali sana inapowekewa mbolea za kukuzia (Nitrogen) kama Urea, CAN, SA nk kulingana na aina yako ya udongo. Kwa hiyo kama ikitokea unaona zao lako halieleweki ujue rutuba haitoshi! Hebu fanya jaribio kidogo sehemu ndogo weka mbolea uone matokeo yake! Nchi zilizoendelea hawalimi mazao haya bila mbolea ili wapate kipato kikubwa! Pamoja na imani kwamba Morogoro ni nchi yenye rutuba zipo sehemu zingine ni choka mbaya tu unakuta mtu anavuna vichwa vya alizeti kama kichwa cha tochi ya Tiger mwee!! Wekeni mbolea!!
 
Mkuu Kubota asante sana!yaani umekata kiu yangu yote ya juu ya zao ili la alizeti!nashukuru sana!kwa kuanzia naona nianze na heka nne niangalie upepo wake!swali moja la mwisho kwako mkuu wangu Kubota je,unaweza kua na mchanganuo wa heka moja ya alizeti tokea uanze kutayarisha shamba,kupanda,kutunza mpaka kuja kuvuna roughly inaweza kugharimu kama kiasi gani kwa heka?asante sana mkuu
 
Kuhusu mchanganuo niko nje na eneo la uzalishaji kwa muda mrefu na bei zitakuwa zimebadilika, waheshimiwa JF tusaidiane kwa hili waungwana!
 
Ndugu yangu Kubota,vp juu ya kilimo hiki kufanyika mkoani Tanga?kinawezekana kufanyika kwa tija kweli?
 
Tanga inamazingira mazuri kabisa ya kulima Alizeti! Alizeti inastawi maeneo ya joto mfano wake Morogoro hadi maeneo ya baridi mfano wake Iringa! Kichocheo kikubwa cha kulima zao la alizeti imekuwa ni uwepo wa soko na hasa mashine za kukamua mafuta! Alizeti inapouzwa kama punje haina kipato kikubwa na ndiyo maana sehemu ambazo si rahisi kupata mashine za kukamulia mafuta kilimo cha zao hili huwa hakipo.
 
Asante sana ndugu Kubota kwa msaada wako mkubwa,itabidi nikakodi mashamba tu Morogoro,maana nilitaka kulimia Tanga,ila angepatikana mtu wa kutupa mchanganuo tu wa kua heka moja yaweza gharimu kiasi gani kuanzia kulima mpaka kuvuna angekua ametusaidia kweli wadau,ni nzuri kua na mawazo ya kujikwamua kimaisha zaidi ya kuwaza kuajiriwa tu!asante sana Kubota
 
Mkuu kuna mdau alinigusia kua ukiwa na Tsh 150,000/= kwa Morogoro una uwezo wa kulima mpaka kuvuna heka moja ukijumlisha na vibarua,ila sijawa na uhakika sana,labda wadau wengine waje kutupa ukweli kuliko kuingia kichwa kichwa!
 
Chonde chonde kaka ukibahatika kupata mchanganuo tushirikishe na sisi.
 
Haina shaka mkuu wangu,nikipata mchanganuo tu nitauweka hapa ili wengine wenye kuvutiwa waweze kujiingiza kwy kilimo,i believe kilimo ukikifanya kwa tija kinakupa maisha bora sana!!
 
Chonde chonde kaka ukibahatika kupata mchanganuo tushirikishe na sisi.

Mheshimiwa Kubota naomba niambie kama ardhi ya mzenga kisarawe kama inafaa kwa kilimo cha alizeti. Maana sina uzoefu wa kutosha, ila ardhi yake inaonekana ina rutuba.
 
Last edited by a moderator:

Kwa upande wa hali ya hewa ukanda huo zao hili linaweza kustawi. Kama Mzenga zao hilo halijawahi limwa nakushauri jaribia kwanza ulime eneo dogo maana hali ya hewa na udongo vinaweza kuwa toshelevu kwa zao lakini kukawa na matatizo mengine tusiyoyajua, kwa mfano uwepo wa wanyama kama panya, ndege na nyani (ngedere) hawa huwa ni kikwazo sana! Kwa vyovyote vile hata kama una nguvu na uwezo msimu wa kwanza jaribu ufanye kama kujaribia! Vinginevyo mazingira ya mzenga ni mazuri tu.
 
Nashukuru sana mkuu Kubota nitajaribu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom