Kilimo bora cha mahindi

Mrkingcamel

Member
Jul 27, 2021
16
12
UTANGULIZI
Mahindi ni zao muhimu la chakula, na ni aina ya nafaka inayotumiwa zaidi kama chakula,uhususani katika matifa ya Afrika, na yamekuwa yakitumika zaidi na nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara. Ni chakula cha matumizi ya nyumbani kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa asilimia 50. Ni chanzo muhimu cha madini na kuongeza nguvu mwilini, protini, madini ya chuma (iron) vitamini na madini mengine asilia.Waafrika
hutumia mahindi kwa njia mbalimbali (uji, ugali na pombe). Na mahindi ya kuchoma.
Kila sehemu ya mmea wa mahindi ina thamani kiuchumi : punje, majani, shina na magunzi huweza kutoa kiasi kikubwa cha bidhaa nyinginezo zilizo chakula na zisizokuwa chakula.
Vile vile mahindi ni chakula muhimu cha mifugo (ng’ombe) na huhifadhiwa kama silage. Pia mabaki ya mimea na nafaka hutumika viwandani kutengeneza wanga na mafuta.
Mahindi ni mimea ambayo hustahimili mabadiliko ya hali ya hewa tofauti tofauti na huweza kumea katika maeneo mengi tofauti hapa nnchini. Kuna aina nyingi za mahindi yanayotofautiana katika muda wa kukomaa, mavuno na ustahimilivu wa hali ya hewa .

HALI YA HEWA NA UDONGO

Mmea huu unahitaji kiwango cha joto cha kila siku cha nyuzi joto 20º ili umee vyema. Joto la juu sana kwa mazao mazuri ni kama nyuzi joto 30º.

Mahindi hustawi katika maeneo mbalimbali hapa nchini kuanzia 0-3000 m kutoka usawa wa bahari kulingana na aina ya mbegu na hali ya hewa ya eneo husika.

Mahindi huwa yanaathirika sana na ukosefu wa unyevu wakati wa kutoa maua na matunda. Pia yanahitaji maji ya kutosha wakati wa kupanda. Katika nchi za joto jingi (tropiki), mahindi hufanya vyema katika mvua ya kiwango cha milimita 600 hadi 900 wakati wa kukua.

Mahindi yanaweza kukuzwa kwenye aina nyingi za udongo lakini hukua vyema zaidi katika udongo wa kichanga au tifutifu usiotuamisha maji mengi, ulio na hewa ya kutosha na ulio na rutuba na madini ya kutosha. Pia h ustawi vizuri katika udongo wenye uchachu wa kiwango cha pH 6-6.5.

Pia ikumbukwe kuwa mahindi ni moja ya zao ambalo huathirika sana na hali ya chumvi katika maji na udongo.

KUTAYARISHA SHAMBA

[https://4]
Shamba la mahindi linahitajika kutayarishwa mapema mapema sana mwanzoni mwa msimu wa mvua au hata kabla mvua kuanza.
Shamba linaweza kuandaliwa kwa aina tofauti tofauti kulinganisha na eneo na aina ya udongo. Shamba linaweza kulimwa kwa trekta au kwa jembe la mkono kwa kina kisichopungua 15 cm ili kuruhusu mizizi kupenya vizuri na udongo kuhifadhi maji kwa wingi. Kama shamba liaasili ya kutuamisha maji matuta yaandaliwe vizuri shambani. Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.
Vilevile kama shamba lina asili ya mmomonyoko wa udongo, basi ni vyema tahathari ichukuliwe katika uhifadhi wa udongo na unyevunyevu ardhini kwa kuweka matandazo shambani (mulching).

FAIDA ZA KUANDAA SHAMBA MAPEMA

Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote.
 Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
 Hupunguza magugu.
 Hupunguza wadudu waharibifu na kuharibu mazalio yao.
 Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
 Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au
yatakuwa kidogo.
 Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi na yatastawi vizuri.

WAKATI WA KUPANDA

Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki,Kama mvua hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako.
 Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba
mwishoni.
 Morogoro,Pwani, DSM, Tanga na Maeneo Jirani Mwezi Januari, February na March Mwanzoni katikati
 Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni
 Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni.
Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni
mkubwa. Kwa mashamba makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvua
kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua. Isiwe mapema zaidi kwani mbegu
zitaharibiwa na joto katika na wadudu, panya, ndege na wanyama wengineo.

KUCHAGUA MBEGU BORA

Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
 Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
 Huzaa mazao mengi.
 Hustahimili magonjwa.

AINA ZA MBEGU

 Mbegu aina ya chotara(hybrid)
 Aina ya ndugu moja(synthetic)
 Mbegu aina ya composite
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia
50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta moja.8( Gunia 25

MAPENDEKEZO YA MBEGUZA KUPANDA

Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa ZAMSEED, SEEDCO ,PANNAR, MERU n.k

KUPANDA

Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikizidi
 Kuna uwezekano wa mazao kupungua.
 Mimea kuwa dhoofu
 Mimea mingi kutozaa au kuwa na matunda madogomadogo.
 Kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kusambaa kwa magonjwa kiurahisi
Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa mavuno kupungua
jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi na kiwango cha mbegu sahihi kilichoshauriwa na mtaalamu hapo chini.

KIASI CHA KUPANDA

 Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja., (Hii hutegemea na aina ya mbegu)

NAFASI ZA KUPANDA.

MASHINE YA KUPANDIA

Unaweza kupanda mhindi katika nafasi mbalimbali kulingana na mahitji yako, hali ya hewa na rutuba ya udongo. lakini zifuatazo ni nafasi pendekezwa na hutumika sehemu nyingi hapa nchini kwetu.
 75cm x 30cm mfano:- mstari kwa mstari 75cm na mche kwa mche 30cm hii ni kwa mbegu moja kwa kila shina na kufanya uwe na idadi ya mimea zaidi ya 44000 kwa hekta.
 75cm x 60cm mfano;- mstari kwa mstari 75cm na mche kwa mche 60cm hii ni kwa mbegu mbili kwa kila shina na kufanya uwe na idadi ya mimea 44000 na zaidi kwa hekta.
 75cm x 25cm mfano:- mstari kwa mstari 75cm na mche kwa mche 25cm hii ni kwa mbegu moja kwa kila shina na kufanya uwe na idadi ya mimea zaidi ya 53000 kwa hekta.
 90cm x 50cm Hii ni nzuri kwa sehemu kame na kwa wanaopanda mazao mchanganyiko au kilimo mseto.
Mahindi yanaweza kuchanganywa na mazao mengine ya kutambaa kama kunde, maharage, maboga, karanga nk.

MATUMIZI YA MBOLEA

 Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwa mbolea pamoja na matunzo mengine ya kilimo bora.
 Angalizo: Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.

KUNA AINA MBILI KUU ZA MBOLEA

 Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hua na
virutubisho vya kutosha ambavyo havijulikani vipo kwa kipimo kiasi gani.
 Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na vipimo hujulikana, hii
inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa kipindi gani.

KWA MFANO:
Mbolea inayotumiwa na wakulima wadogo mara yingi huwa haitoshi. Mahindi ya kiwango cha juu yaweza tu kufikia kiwango cha juu cha Uzalishaji iwapo yatapewa lishe na madini ya kutosha. Mahindi ya tani 2 kwa hekta na tani 5 kwa hekta hutumia karibu kilo 60 N, kilo 10 za P205 na kilo 70 K20 kutoka katika udongo. Mahindi hunyonya Nitrogen pole pole katika miezi ya kwanza baada ya kupanda, lakini huongezeka hadi kiwango cha juu kabisa
wakati wa kutoa maua na kukuza tunda (gunzi). Mahindi huhitaji nitrogen kwa kiwango cha juu na ukosefu huwa ndio kizingiti. Kiwango cha juu cha nitrogen kinahitajika mara tatu; kwanza wakati wa kupanda, pili, wakati ambapo mmea umefikia sentimita 50 za urefu na tatu, wakati matunda ya mahindi yanaanza kutoa zile nyuzi nyuzi nyororo (silking). Udongo mwingi huwa na madini ya phosphorous (P205) na potassium (K20) lakini sio kiwango kinachotosheleza mahitaji haswa ya mbegu za mahindi zinapochipua. Nyunyuzia P205 karibu na mbegu ili ziote kwa haraka. K20 hutumika kwa kiwango kikubwa lakini hitaji la mimea hubainika baada ya upimaji wa hali ya udongo kujua kiasi cha mahitaji (soil test). (ndo maana twasisitiza mbolea za viwandani sio lazima iwe ya kemikali).
 
Samahani mkuu ni nina maswali Kede Kede kama ni mtaalamu wa kilimo naomba nikuulize
 
Asante kwa nyuzi kali kama hii.
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom