Kilimo cha Bamia: Fahamu kuhusu mbegu bora, mazingira sahihi ya kulima, magonjwa na namna ya kuyakabili

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
1589091493453.png

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU KILIMO HIKI:
Mwenye kufahamu ufanisi wa hiki kilimo atujuze mambo yafuatayo:
1) Mbegu bora zinapatikana wapi?
2) Zinachukua muda gani kukomaa?
3) Masoko yake yako wapi?
4) Bei ya kuuza inakwendaje?

Asanteni.
===
Habarini Wakuu,

Baada ya kuona nina kila sababu ya kuongeza kipato changu, nimefikiri na kugundua nahitaji kuwekeza katika kilimo cha bamia kwa sasa.

Na kwa kuwa JF ina watu makini na hodari katika nyanja mbalimbali basi mtanisaidia kimbinu,ushauri na maarifa ili kufanikisha hii plan yangu.

Kwa kuanzia nina eneo la ekari 2 na visima viwili vyenye maji ya kutosha nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.

Kimsingi nimekamilisha maandalizi mengi ya awali kwa ajili ya kuanza kilimo cha umwagiliaji,kwani pamoja na kuwa na maji ya kutosha lakini pia nimenunua pump na nina mbolea ya samadi tayari.

Yote kwa yote naomba mnijuze,

~ni aina gani ya mbegu inafaa zaidi na inayotumia muda mfupi toka kupanda hadi mavuno na yenye soko zuri.

~changamoto zipi nijiandae kukabiliana nazo katika kilimo hiki.

~dawa zipi zinahitajika magonjwa na wadudu wakianza kushambulia mimea.

Ni hayo tu,natumai kupata mawazo yenu wakuu ili nijue kipi napaswa kufanya.
---
Habari wana JF,

Ningependa kufahamishwa kuhusu kilimo cha bamia ,mbegu bora ,dawa, muda kupanda hadi kuivuna.

Asanteni
---
Wapendwa ndugu zangu, salaamu kwenu.

Naombeni msaada wa mawazo na uzoefu wenu kuhusu kilimo cha Bamia.

a) Ni mbegu aina gani iliyo bora? na nikanunue wapi penye mbegu origino?

b) Kuhusu spacing ya kupandia... wanasema ni sentimita 30 shimo kwa shimo, sentimita 60 msitari kwa msitari. Je kuna madhara gani kama nisipozingatia iyo spacing? i.e nichimbe mashimo ya karibu karibu zaidi.

c) Kuhusu magonjwa... kuanzia kupanda/kuotesha mpaka mavuno, je nitumie dawa/sumu zipi kuzuia/kukinga (prevention) mmea usipatwe kabisa na ugonjwa wowote?

d) Kuhusu mbolea ya kienyeji (ya kuku) ama za kisasa, nitumie mbolea ipi? na kwanini?

e) Je, nifanye mbinu zipi au nifanye mambo gani ili Bamia izae sana (maua kwa wingi) na nivune kwa muda mrefu (mmea usizeeke mapema) ?

N.B: Eneo la kulima lipo Dar.

Natanguliza shukrani za dhati. Mungu awabariki.
===
UFAFANUZI WA JUMLA WA KILIMO HIKI
Bamia ni zao la Jamii ya mbogamboga linalotambulika kitaalamu kama Abelmoschus esculentus (OKRA) lenye asili ya Afrika ya magharibi. Kwa sasa zao hili linalimwa katika nchi nyingi hasa sehemu za joto. Baadhi ya maeneo yanayolima zao la bamia kwa Tanzania ni pamoja na ukanda wote wa nchi ya Tanzania,Kutoka mita 0-1500 kutoka usawa wa bahari

Zaidi ya hapo unaweza kulima lakini halivumilii hali ya baridi kali. Pia bamia hufanya vizuri zaidi katika maeneo yenye udongo wenye unyevu wa kutosha na joto la wastani wa nyuzi joto 25 - 30 C.

Mvua hadi kiasi cha milimita 1000 cha mvua kwa mwaka.tu asili yake ni africa nchini Ethiopia ambapo kwa sasa linalimwa katika nchi nyingi.bamia ni moja kati ya mazao ambayo yanafaida sana ndani ya mwili kama kusafisha utumbo mpana husaidia kulainisha choo huongeza uroto kwa wale wenye upungufu wa uroto kwenye maungio pia ina vitamin C ambayo husaidia kulainisha ngozi na macho kuona

AINA ZA UDONGO
Kuna aina kuu tatu za udongo,
• Kichanga (Sand soil) –
una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.
• Tifutifu (Loam soil) –
unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.
• Mfinyanzi (Clay soil) –
unahifadhi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.

Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:
- Tindikali ya udongo
- Kiasi cha mboji
- Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium.

Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa. Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH)

PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita.

Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0). Ila bamia Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katikakipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0.

MAANDALIZI YA SHAMBA LA BAMIA
Taarisha shamba lako mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita. Baada ya kuvuna, udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi na masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.

Magonjwa kama yale ya majani hayatatokea yatakuwa kidogo. Hupunguza magugu.Hupunguza wadudu waharibifu .Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na MIMEA kutastawi vizuri. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:

1. Jembe la mkono - wengi wanatumia
2. Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
3. Power tillers
4. Trekta

ZINGATIA
Tunashauliwa kupanda bamia katika matuta ili kusaidia mizizi kukua vizuri na udongo kuhifadhi maji. Wakati wa kiangazi, tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo ili kufanya maji yaweze kukaa kwenye udongo na wakati wa masika matuta yainuliwe kidogo toka kwenye usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasituame. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.

AINA ZA BAMIA
Kuna aina za bamia zinazo patikana kama vile:

1. Clemson spineless
Ain ya bamia hii inatabia ya kukua urefu wa mita 1 hadi 1.5 na kuzaa bamia za kijani zenye urefu karibu sm 15. Huchukua siku 55 hadi 58 kuanza kuvuna.

2. Emerald green
bamia hii ina tabia ya kukua hadi urefu wa m 1.5 na kuzaa bamia za kijani zenye urefu wa sm 18 hadi 20. Huchukua siku 58 hadi 60 kuanza kuvuna.

3. White velvet
bamia hii inatabia ya kukua urefu wa m 1.5 hadi 1.8 na kuzaa bamia ndefu, nyembamba, zilizochongoka na zenye urefu wa sm 15 hadi 18.

UANDAAJI WA MBEGU
Andaa mbegu mapema kwa kawaida inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji kwenye bustani. Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za bamia zinazoweza kupandwa na kutoa mavuno bora kama vile Lady’s Finger, Quim Bombo, Asutem, Mkulima-Clemson Spineless, Labadi Dwarf.

UPANDAJI WA BAMIA
Mbegu za bamia mara nyingi husumbua kidogo kuota kama patakuwa na hali ya baridi katika udongo.Hivyo ili ziote vizuri tunashauriwa kabla ya kuzipanda shambani ziloweke katika maji ya uvuguvugu kwa masaa 24 au ziloweke kwa dakika 30 katika ethly alcohol and acetone.

panda mbegu zako katika mashimo uliyoyachimba katika udongo wenye unyevu kwa kina cha sentimeta 2 -3 katika nafasi ya sentimeta 60-90 kati ya mstari na msatari na sentimeta 25-50 Kati ya shina na shina utahitajika katika kila shimo uweke mbolea kwa ajili ya ukuaji mzuri wa Bamia zako.

kutumia mbolea ya kuku au ng'ombe amabayo ni bora zaidi kwani ya kuku huisha kazi yake mapema zaidi katika udongo.Panda Mbegu mbili kwa kila shimo na zikisha ota ngolea uache shina moja kwa kila shimo.

kiasi cha kilo 1.5 - 2.5 hutosha kwa ekari moja ambapo wingi wa mbegu itategemea uwezo wa mbegu kuota na aina ya bamia.Kama mbegu zako uwezo wake wa kuota ni mdogo mbegu zitatumika nyingi na kama unapanda bamia fupi au bamia zenye mbegu kubwa mbegu itatumika nyingi pia.

Mbegu za bamia zinaweza kuchukua siku 8 - 10 kupanda hadi kuota.Pia bamia unaweza kupanda mbegu katika kitalu baadaye zikifikisha sentimeta 10-15 unazing'oa na kwenda kupanda shambani ila njia nzuri ni kupanda moja kwa moja shambani

PALIZI
Katika kilimo cha bamia ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda.nashauri kwamba katika kilimo cha cha bamia shamba lipaliliwe mara 1-2, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono kwa kung’olea au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (HERBCIDES).

MFUMO WAUMWAGILIAJI
Hali ya unyevunyevu ni mdogo katika shamba itahitajika uwe unamwagilia shamba lako kila baada ya siku 10 au pungufu kulingana na hali ya unyevu katika shamba lako.Kiasi cha wastani wa milimita 350 za maji katika siku 10 zinahitajika kwa ukuaji wa bamia ili uweze kupata mavuno yaliyo bora na mengi.na kama umepanda mbegu katika kipindi cha ukame zimwagilie kila siku kuhakikisha udongo wako unakuwa na unyevu wa kutosha ili uwezesha mbegu zako kuota.

MBOLEA
Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja kwenye mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.

Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati na potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium, boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa asili, yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua kutokana na kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.

Aina za mbolea
Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:
1. Mbolea za asili (organic fertilizers)
2. Mbolea za viwandani (inorganic or industrial fertilizers)

Mbolea Za Asili (Organic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili ni kama vile:
i. Mbolea vunde: inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana na mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.
ii. Samadi: kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na ndege.
iii. Mbolea za kijani: hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde ambayo hukatuliwa na kuchanganywa na udongo.
iv. Majivu: ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa wingi, fosfati, chokaa na magnesium.
v. Matandazo (mulch): ambayo baadaye yakioza huwa mbolea.
Mbolea Za Viwandani (Inorganic Fertilizers)

Hizi ni mbolea zinazotengenezwa viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa lengo maalum la kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho vinavyohitajika na mimea.

RATIBA YA MBOLEA KATIKA ZAO LA BAMIA

HATUA YA KWANZA
(Tunashauri Kapadia kwa Samadi kama ikiwepo)
NPK 15.9.20 +TE(yaramila winner) Gramu 10 kupanda bila kuweka samadi
Yara mila winner Gram 5 pamoja na samadi kwa shina / shina moja
Tenganisha kwa kuweka tabaka la udongo usio na mbolea kwa sentimita mbili kati ya mbengu na udongo uliyochanywa na mbolea
Epuka mbegu kugusana na mbolea inaweza kuungua na kushindwa kuota

HATUA YA PILI(A) KUWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KATIKA UDONGO
NITROBAR (CAN)

Weka mbolea ya kukuzia ya nitrobar wiki tatu baada ya mche kuota au mche wenye majani matatu(3)baada ya utokaji .
Weka mbolea ya ujazo wa kifuniko cha soda /kijiko kimoja kidogo cha chai sawa na gramu tano katika kila shina la mche mmoja
Weka mbolea kwa umbali wa kiasi cha sentimita 5 kutoka mzunguko wa shina alafu fukia zingatia kuweka mbolea hii mapema kabla ya kutoa maua.

HATUA YA PILI (B) KUWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KUPITIA MAJANI(BUSTA) BAMIA
MULT-K AND SUPERGRO/NPK+TE foliar –pulizia mbolea hii kwa miche ikiwa na majani matatu hadi manne ya kuchipua
Changanya MULT-K maganda matatu ya kibiriti katika maji ya lita 20 puliza juu ya majani ya mche

Rudia tena baada ya siku kumi na nne (14) zingatia kutumia mbolea,
Mbolea hii ni mtiririko wa mbolea ya kukuzia sambamba na nitrobar izingatie kutumia kabla ya maua.

WADUDU NA MAGONJWA YA BAMIA

1)WADUDU

A) Mdudu mafuta (aphids)
Hufyonza majimaji katika majani na bamia changa hivyo kusababisha bamia kutokuwa vizuri na bora.
Kinga na tiba
Tumia dawa za wadudu kama vile ABAMECTIN, NIMEBECIDIN FARMER GULD, ACTARA,n.k

B) MIilibagi (Mealy bug)
Ni wadudu wanaoganda katika majani,matawi na bamia wakifyonza maji maji ya mimea
Kuzuia na Kinga-Tumia dawa za wadudu kama vile selecron 720,Nimebecidin,multimectin,Dudu all,ninja nk n.k

c)Funza(Boll worm)
Hawa ni funza amabao hutoboa na kuharibu Bamia

Kinga na tiba
Kwa maeneo yanayoshambuliwa sana na wadudu,Puliza dawa za wadudu mara tuu bamia ziwekapo ua na zikiwa ndogo,Puliza asubuhi sana au jioni sana ili kuwakwepa wadudu wachavushaji wasije kufa na dawa wakati unapuliza.Puliza dawa kama vile Nimebedicin,albamectin n.k kuua wadudu hawa

d) Funga funga(Leaf roller)
hufunga majani kwa kuyavilingisha na kukaa na kula majani hayo.
kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin,dudu all n.k

e) Inzi weupe (whitefly)
Ni waenezaji wakubwa wa magonjwa ya virusi, wadudu hawa hufyonza majimaji katika majani ya mimea na hujificha sana chini ya majani wakati wa jua kali
kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin,dudu all,actara, n.k

f) Vinundu katika Mizizi(Root –knot nematodes)
Ni wadudu wadogo kama minyoo midogo ambao hula katika mizizi midogo na kusababisha uvimbe na mimea kusinyaa.

kinga na tiba
tumia dawa kama vile NIMEBECIDIN (kwa kiasi kikubwa Chini ya shina La mmea), DAZOMET (BASAMID),CARBOFURAN(FURADAN) kuua wadudu hawa.Hizi ni dawa za ardhini.

2) MAGONJWA YA BAMIA
Bamia hushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama vile;

a) Ubwiri unga (Powdery mildew)
Ni ugonjwa unaosababishwa na fangasi(ukungu).ugonjwa ambao hufanya mmea kuwa na madoa au unga unga unga wa rangi ya kijivu katika majani na baadaye hunyauka na kufa na kupukutika majani.

TIBA NA KINGA
Liweke shamba lako katika hali ya usafi na Puliza dawa za ukungu zenye salfa kama vile copper sulphate, na siku za upuliziaji itategemea muda wa kulima bamia masika hupulizwa mara kwa mara na kiangazi hupulizwa mara chache.
b)Ugonjwa wa kujikunja na kudumaa majani (Leaf curl)
ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ni ugonjwa ambao huambatana na kujikunja kwa majani machanga na kuwa magumu na mmea kudumaa kukua

KUZUIA NA KINGA
-panda mbegu kinzani na ugonjwa huu,tumia madawa ya ukungu kama vile Copper sulphate, au puliza sulpha au copper (BONIDE).Pia tumia dawa za wadudu kuua wadudu kama nzi weupe ambao kwa kiasi kikubwa hueneza ugonjwa huu.

c) Ugonjwa wa manjano (Mosaic)
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi amabapo mmea ulioshambuliwa huwa na majani yenye umbo na ukubwa wa kawaida lakini yenye kijani kikavu au majani yenye rangi ya njano ambapo baadaye mmea hudumaa kukua.KUMBUKA rangi ya njano ya majani inaweza kusababishwa pia na ukosefu wa nitrojeni katika mmea hasa kama maji yatakuwa mengi ardhini katka udongo

KUZIA NA KINGA
kukinga na kuzuia ugonjwa huu hakikisha unapanda mbegu kinzani na ugonjwa huu.zui wadudu katika shamba lako kwani wanaweza kueneza ugonjwa huu shambani kwako.Jiadhari na uvutaji au ubebaji wa sigara/tumbakukatika shamba la bamia wakati unatembea au unafanya kazi katika shamba la bamia.Ng'oa mashina yaliyoathirika mapema na uyachome moto mbali na shamba.lima kilimo cha mzunguko wa mazao tofauti na jamii ya bamia.

10. JINSI YA KUVUNA BAMIA
Bamia huwa tayari kuanza kuvunwa mwezi 1 tangu kupandwa na huckukua siku 6 kuvunwa baada ya kuanguka.

kama matunzo ni mazuri kila ua katika mabamia litatowa bamia.chuma vizuri bamia kutoka katika mbamia bila kuacha athari kubwa katika mche wa mbamia.

Hivyo kwa uvunaji mzuri unaweza kutumia mkasi mkali katika kukata vikonyo vya bamia.chuma bamia kubwa na ndogo ziache ziendelee kukua, ila inakubidi uwe mwangalifu ili bamia zisije kukomaa shambani kwani hukomaa kwa haraka zaidi na zilizokomaa hazina soko zuri na hazipendwi na walaji kwani huwa gumu na nyuzinyuzi nyingi.

Katika matunzo mazuri unaweza kuendelea kuchuma bamia kutoka katika mibamia kwa muda wa miezi miezi 2 na zaidi.

MAVUNO
wingi wa mavuno hutegemea matunzo na aina ya mbegu za bamia,muda wa upandaji na kukua-baridi ikiwa kali mavuno yake hupungua na mara za uchumaji wa bamia-kadri zinavyochumwa mara nyingi ndivyozinavyozidi kuzaa na zile zinazozachumwa kwa muda mrefu ndizo zenye manufaa kwa mkulima , japokuwa kwa wastani bamia huvunwa kiasi cha tani 3 - 10 kwa ekari

11.UHIFADHI WA BAMIA
Bamia ni kama mazao mengine ya mbogamboga haistahimili kukaa muda mrefu bila kuliwa na kadri inavyokaa muda mrefu baada ya kuvunwa ndipo hupoteza ubora wake.Kama kuna soko hakikisha unazivuna na kuzipeleka sokoni.

Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo.

BAADHI YA MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
KILIMO BORA CHA BAMIA NA KANGETAKILIMO

KILIMO BORA CHA BAMIA NA KANGETAKILIMO

Agro Project Tz
KILIMO CHA BAMIA

Bamia ni zao la Jamii ya mbogamboga linalotambulika kitaalamu kama Abelmoschus esculentus (OKRA) lenye asili ya Afrika ya magharibi. Kwa sasa zao hili linalimwa katika nchi nyingi hasa sehemu za joto. Baadhi ya maeneo yanayolima zao la bamia kwa Tanzania ni pamoja na ukanda wote wa nchi ya Tanzania,Kutoka mita 0-1500 kutoka usawa wa bahari zaidi ya hapo unaweza kulima lakini halivumilii hali ya baridi kali.Pia bamia hufanya vizuri zaidi katika maeneo yenye udongo wenye unyevu wa kutosha na joto la wastani wa nyuzi joto 25 - 30 C.

Mvua hadi kiasi cha milimita 1000 cha mvua kwa mwaka.tu asili yake ni africa nchini Ethiopia ambapo kwa sasa linalimwa katika nchi nyingi.bamia ni moja kati ya mazao ambayo yanafaida sana ndani ya mwili kama kusafisha utumbo mpana husaidia kulainisha choo huongeza uroto kwa wale wenye upungufu wa uroto kwenye maungio pia ina vitamin C ambayo husaidia kulainisha ngozi na macho kuona

AINA ZA UDONGO
Kuna aina kuu tatu za udongo,
• Kichanga (Sand soil) –
una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.
• Tifutifu (Loam soil) –
unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.
• Mfinyanzi (Clay soil) –
unahifadhi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.

Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:
Ø Tindikali ya udongo
Ø Kiasi cha mboji
Ø Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium.
Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa. Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH)
PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0)

.Ila bamia Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katikakipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0

AINA YA UDONGO UNAOFAA KWA ZAO LABAMIA
BAMIA hustawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia halinaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya

MAANDALIZI YA SHAMBA LA BAMIA

Taarisha shamba lako mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita. Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi na masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.Magonjwa kama yale ya majani hayatatokea yatakuwa kidogo. Hupunguza magugu.Hupunguza wadudu waharibifu .Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na MIMEA kutastawi vizuri. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
1. Jembe la mkono - wengi wanatumia
2. Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
3. Power tillers
4. trekta

ZINGATIA
Tunashauliwa kupanda bamia katika matuta ili kusaidia mizizi kukua vizuri na udongo kuhifadhi maji. Wakati wa kiangazi, tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo ili kufanya maji yaweze kukaa kwenye udongo na wakati wa masika matuta yainuliwe kidogo toka kwenye usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasituame. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.

AINA ZA BAMIA
Kuna aina za bamia zinazo patikana kama vile

1. Clemson spineless
.
Ain ya bamia hii inatabia ya kukua urefu wa mita 1 hadi 1.5 na kuzaa bamia za kijani zenye urefu karibu sm 15. Huchukua siku 55 hadi 58 kuanza kuvuna.
2. Emerald green.
bamia hii ina tabia ya kukua hadi urefu wa m 1.5 na kuzaa bamia za kijani zenye urefu wa sm 18 hadi 20. Huchukua siku 58 hadi 60 kuanza kuvuna.
3. White velvet.
bamia hii inatabia ya kukua urefu wa m 1.5 hadi 1.8 na kuzaa bamia ndefu, nyembamba, zilizochongoka na zenye urefu wa sm 15 hadi 18.
UWANDAAJI WA MBEGU
Andaa mbegu mapema kwa kawaida inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji kwenye bustani. Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za bamia zinazoweza kupandwa na kutoa mavuno bora kama vile Lady’s Finger, Quim Bombo, Asutem, Mkulima-Clemson Spineless, Labadi Dwarf.

UPANDAJI WA BAMIA

Mbegu za bamia mara nyingi husumbua kidogo kuota kama patakuwa na hali ya baridi katika udongo.Hivyo ili ziote vizuri tunashauriwa kabla ya kuzipanda shambani ziloweke katika maji ya uvuguvugu kwa masaa 24 au ziloweke kwa dakika 30 katika ethly alcohol and acetone,.
panda mbegu zako katika mashimo uliyoyachimba katika udongo wenye unyevu kwa kina cha sentimeta 2 -3 katika nafasi ya sentimeta 60-90 kati ya mstari na msatari na sentimeta 25-50 Kati ya shina na shina utahitajika katika kila shimo uweke mbolea kwa ajili ya ukuaji mzuri wa Bamia zako
kutumia mbolea ya kuku au ng'ombe amabayo ni bora zaidi kwani ya kuku huisha kazi yake mapema zaidi katika udongo.Panda Mbegu mbili kwa kila shimo na zikisha ota ngolea uache shina moja kwa kila shimo.kiasi cha kilo 1.5 - 2.5 hutosha kwa ekari moja ambapo wingi wa mbegu itategemea uwezo wa mbegu kuota na aina ya bamia.Kama mbegu zako uwezo wake wa kuota ni mdogo mbegu zitatumika nyingi na kama unapanda bamia fupi au bamia zenye mbegu kubwa mbegu itatumika nyingi pia.Mbegu za bamia zinaweza kuchukua siku 8 - 10 kupanda hadi kuota.Pia bamia unaweza kupanda mbegu katika kitalu baadaye zikifikisha sentimeta 10-15 unazing'oa na kwenda kupanda shambani ila njia nzuri ni kupanda moja kwa moja shambani

PALIZI
Katika kilimo cha bamia ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda.nashauri kwamba katika kilimo cha cha bamia shamba lipaliliwe mara 1-2, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono kwa kung’olea au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (HERBCIDES).

MFUMO WAUMWAGILIAJI
Hali ya unyevunyevu ni mdogo katika shamba itahitajika uwe unamwagilia shamba lako kila baada ya siku 10 au pungufu kulingana na hali ya unyevu katika shamba lako.Kiasi cha wastani wa milimita 350 za maji katika siku 10 zinahitajika kwa ukuaji wa bamia ili uweze kupata mavuno yaliyo bora na mengi.na kama umepanda mbegu katika kipindi cha ukame zimwagilie kila siku kuhakikisha udongo wako unakuwa na unyevu wa kutosha ili kuwezesha mbegu zako kuota.

MBOLEA
Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja kwenye mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.
Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati na potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium, boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa asili, yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua kutokana na kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.

Aina za mbolea
Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:
1. Mbolea za asili (organic fertilizers)
2. Mbolea za viwandani (inorganic or industrial fertilizers)

Mbolea Za Asili (Organic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili ni kama vile:
i. Mbolea vunde: inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana na mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.
ii. Samadi: kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na ndege.
iii. Mbolea za kijani: hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde ambayo hukatuliwa na kuchanganywa na udongo.
iv. Majivu: ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa wingi, fosfati, chokaa na magnesium.
v. Matandazo (mulch): ambayo baadaye yakioza huwa mbolea.

Mbolea Za Viwandani (Inorganic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotengenezwa viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa lengo maalum la kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho vinavyohitajika na mimea.

RATIBA YA MBOLEA KATIKA ZAO LA BAMIA
HATUA YA KWANZA

(Tunashauri Kapadia kwa Samadi kama ikiwepo)
NPK 15.9.20 +TE(yaramila winner) Gramu 10 kupanda bila kuweka samadi
Yara mila winner Gram 5 pamoja na samadi kwa shina / shina moja
Tenganisha kwa kuweka tabaka la udongo usio na mbolea kwa sentimita mbili kati ya mbengu na udongo uliyochanywa na mbolea
Epuka mbegu kugusana na mbolea inaweza kuungua na kushindwa kuota

HATUA YA PILI(A) KUWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KATIKA UDONGO
NITROBAR (CAN)
Weka mbolea ya kukuzia ya nitrobar wiki tatu baada ya mche kuota au mche wenye majani matatu(3)baada ya utokaji .
Weka mbolea ya ujazo wa kifuniko cha soda /kijiko kimoja kidogo cha chai sawa na gramu tano katika kila shina la mche mmoja
Weka mbolea kwa umbali wa kiasi cha sentimita 5 kutoka mzunguko wa shina alafu fukia zingatia kuweka mbolea hii mapema kabla ya kutoa maua

HATUA YA PILI (B) KUWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KUPITIA MAJANI(BUSTA) BAMIA
MULT-K AND SUPERGRO/NPK+TE foliar –pulizia mbolea hii kwa miche ikiwa na majani matatu hadi manne ya kuchipua
Changanya MULT-K maganda matatu ya kibiriti katika maji ya lita 20 puliza juu ya majani ya mche
Rudia tena baada ya siku kumi na nne (14) zingatia kutumia mbolea,
Mbolea hii ni mtiririko wa mbolea ya kukuzia sambamba na nitrobar izingatie kutumia kabla ya maua
HATUA YA TATU KUWEKA MBOLEA YA UZALISHAJI WA MATUNDA YA
Maua na matunda yatakapotunga wiki ya sita na nane weka tena npk 15.9.20+ TE(yaramila winner) gram 10 kwa shina (kijiko cha chakula)
Weka mbolea au umbali wa nchi 6 mzunguko wa shina unaweza kuongeza gram 5 hadi 10 baada ya siku ya 21 kama kuna viashirio vya upungufu wa rutuba shambani kwa kuangalia ubora matunda na muonekano wa majani ya matikiti
WADUDU NA MAGONJWA YA BAMIA
1)WADUDU

A) Mdudu mafuta (aphids)
Hufyonza majimaji katika majani na bamia changa hivyo kusababisha bamia kutokuwa vizuri na bora.

Kinga na tiba
Tumia dawa za wadudu kama vile ABAMECTIN, NIMEBECIDIN FARMER GULD, ACTARA,n.k

B) MIilibagi (Mealy bug)
Ni wadudu wanaoganda katika majani,matawi na bamia wakifyonza maji maji ya mimea

Kuzuia na Kinga-Tumia dawa za wadudu kama vile selecron 720,Nimebecidin,multimectin,Dudu all,ninja nk n.k

c)Funza(Boll worm)
Hawa ni funza amabao hutoboa na kuharibu Bamia

Kinga na tiba
Kwa maeneo yanayoshambuliwa sana na wadudu,Puliza dawa za wadudu mara tuu bamia ziwekapo ua na zikiwa ndogo,Puliza asubuhi sana au jioni sana ili kuwakwepa wadudu wachavushaji wasije kufa na dawa wakati unapuliza.Puliza dawa kama vile Nimebedicin,albamectin n.k kuua wadudu hawa

d) Funga funga(Leaf roller)
hufunga majani kwa kuyavilingisha na kukaa na kula majani hayo.

kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin,dudu all n.k

e) Inzi weupe (whitefly)
Ni waenezaji wakubwa wa magonjwa ya virusi, wadudu hawa hufyonza majimaji katika majani ya mimea na hujificha sana chini ya majani wakati wa jua kali.

kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin,dudu all,actara, n.k

f) Vinundu katika Mizizi(Root –knot nematodes)
Ni wadudu wadogo kama minyoo midogo ambao hula katika mizizi midogo na kusababisha uvimbe na mimea kusinyaa.

kinga na tiba
tumia dawa kama vile NIMEBECIDIN (kwa kiasi kikubwa Chini ya shina La mmea), DAZOMET (BASAMID),CARBOFURAN(FURADAN) kuua wadudu hawa.Hizi ni dawa za ardhini.

2) MAGONJWA YA BAMIA
Bamia hushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama vile;

a) Ubwiri unga (Powdery mildew)
Ni ugonjwa unaosababishwa na fangasi(ukungu).ugonjwa ambao hufanya mmea kuwa na madoa au unga unga unga wa rangi ya kijivu katika majani na baadaye hunyauka na kufa na kupukutika majani.

TIBA NA KINGA
Liweke shamba lako katika hali ya usafi na Puliza dawa za ukungu zenye salfa kama vile copper sulphate, na siku za upuliziaji itategemea muda wa kulima bamia masika hupulizwa mara kwa mara na kiangazi hupulizwa mara chache.

b)Ugonjwa wa kujikunja na kudumaa majani (Leaf curl)
ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ni ugonjwa ambao huambatana na kujikunja kwa majani machanga na kuwa magumu na mmea kudumaa kukua.

KUZUIA NA KINGA
-panda mbegu kinzani na ugonjwa huu,tumia madawa ya ukungu kama vile Copper sulphate, au puliza sulpha au copper (BONIDE).Pia tumia dawa za wadudu kuua wadudu kama nzi weupe ambao kwa kiasi kikubwa hueneza ugonjwa huu.

c) Ugonjwa wa manjano(Mosaic)
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi amabapo mmea ulioshambuliwa huwa na majani yenye umbo na ukubwa wa kawaida lakini yenye kijani kikavu au majani yenye rangi ya njano ambapo baadaye mmea hudumaa kukua.KUMBUKA rangi ya njano ya majani inaweza kusababishwa pia na ukosefu wa nitrojeni katika mmea hasa kama maji yatakuwa mengi ardhini katka udongo.

KUZIA NA KINGA
kukinga na kuzuia ugonjwa huu hakikisha unapanda mbegu kinzani na ugonjwa huu.zui wadudu katika shamba lako kwani wanaweza kueneza
ugonjwa huu shambani kwako.Jiadhari na uvutaji au ubebaji wa sigara/tumbakukatika shamba la bamia wakati unatembea au unafanya kazi katika shamba la bamia.Ng'oa mashina yaliyoathirika mapema na uyachome moto mbali na shamba.lima kilimo cha mzunguko wa mazao tofauti na jamii ya bamia.

10. JINSI YA KUVUNA BAMIA
Bamia huwa tayari kuanza kuvunwa mwezi 1 tangu kupandwa na huckukua siku 6 kuvunwa baada ya kuanguka.kama matunzo ni mazuri kila ua katika mabamia litatowa bamia.chuma vizuri bamia kutoka katika mbamia bila kuacha athari kubwa katika mche wa mbamia.
Hivyo kwa uvunaji mzuri unaweza kutumia mkasi mkali katika kukata vikonyo vya bamia.chuma bamia kubwa na ndogo ziache ziendelee kukua,ila inakubidi uwe mwangalifu ili bamia zisije kukomaa shambani kwani hukomaa kwa haraka zaidi na zilizokomaa hazina soko zuri na hazipendwi na walaji kwani huwa gumu na nyuzinyuzi nyingi.
Katika matunzo mazuri unaweza kuendelea kuchuma bamia kutoka katika mibamia kwa muda wa miezi miezi 2 na zaidi.

MAVUNO
wingi wa mavuno hutegemea matunzo na aina ya mbegu za bamia,muda wa upandaji na kukua-baridi ikiwa kali mavuno yake hupungua na mara za uchumaji wa bamia-kadri zinavyochumwa mara nyingi ndivyozinavyozidi kuzaa na zile zinazozachumwa kwa muda mrefu ndizo zenye manufaa kwa mkulima , japokuwa kwa wastani bamia huvunwa kiasi cha tani 3 - 10 kwa ekari

11.UHIFADHI WA BAMIA

Bamia ni kama mazao mengine ya mbogamboga haistahimili kukaa muda mrefu bila kuliwa na kadri inavyokaa muda mrefu baada ya kuvunwa ndipo hupoteza ubora wake.Kama kuna soko hakikisha unazivuna na kuzipeleka sokoni.
Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo

TEMBELEA MAKALA ZANGU KWENYE MTANDAO KANGETAKILIMO

· Kilimo cha mihongo na mazao yote ya nafaka kama ufuta mbaazi ,choroko,mahindi ,karanga,nk
· Kilimo cha vitunguu,pilipli,nyanya na mazao yote ya mbogamboga
· Kilimo cha matunda kama mipesheni mipapai,michungwa,nk
· Ufugaji wa kuku wa kienyeji kisasa

===
Hongera ndugu kwa hatua kubwa uliopiga, mambo ya kuzingatia katika kilimo:-
1. Fanya uchunguzi juu ya soko la zao lolote kabla ya kulilima, hii itakusaidia kuangalia matazamio ya faida. Wengi huwa tunakosea tunaanza kulima then tunakuja kutafuta soko usifanye kosa hilo.

2. Andaa pembeje za kilimo unachotaka kukifanya (mbegu, madawa) na pesa ya dharula. Mimi ningekushauri ununue mbegu za kampuni hizi mbili PV Holland na Royal na ulime nusu heka kampuni moja na nusu nyingine kampuni nyingine. Sababu kubwa ya kukwambia hivi hii itakusaidia na kukupa uhakika ni aina gani ni nzuri na bora kuliko nyingine, ninamaana hapa wewe mwenyewe utajua mbegu gani inawahi kuzaa mapema, mbegu gani haishambuliwi na magonjwa na nimbegu gani utaichuma kwa muda mrefu wakati wa kuvuna, hii muhimu sana kuweka kumbukumbu ya kuandika siku ulipopanda.

3. Ingia kwenye kilimo sasa sana uwe unachunguz a mazao yako mara kwa mara maranyingi dawa hupuliziwa kila baada ya wiki 2, inategemea na geographia ya eneo husika.

4. Naamini ukizingatia hayo utafanya vizuri utakapo lima awamu yapili kwasababu utakuwa umepata uzoefu wa kilimo na changamoto ulizopitia. Bamia kupanda hadi kuanza mavuno ni siku 45 mpaka 60.

Nisikuchoshe na maelezo marefu mimi pia najifunza naamini wapo wengine wajuzi zaidi watajazia au kurekebisha pale nilipokosea.

Nakutakia kila lakheri na mafanikio.

Sent from my LG-H635 using JamiiForums mobile app
---
UTANGULIZI
Bamia ni zao la mbogamboga linalolimwa sana sehemu za joto, kwa lugha ya kigeni inaitwa Okra. Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda yanayotokana na mmea. Zao hili linafaida sana kiafya, baadhi ya watu hutumia bamia kutengenezea mrenda. Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

ASILI YAKE
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limeenea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines. Zao hili kwa sasa hulimwa maeneo mengi.

HALI YA HEWA
Zao hili hustawi katika mita 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Lima shamba lako vizuri kwa kutumia trekta, jembe la ng’ombe, jembe la mkono au pawatila, hakikisha shamba linakuwa halina nyasi, changanya samadi au mboji na udongo ili kuongeza rutuba.

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Andaa mbegu mapema kwa kawaida inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji kwenye bustani.

UPANDAJI
Mbegu za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani au shamba, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).Aidha kuotesha ili kurahisisha uotaji mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja.

nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa zile aina zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.

MBOLEA
Katika zao hili inashauriwa kutumia mbolea za asili (samadi na mboji) au takataka ili kurutubisha ardhi na kupata mavuno mengi.

UPALILIAJI & UNYEVU
Shamba la bamia inatakiwa lipaliliwe kwa kuondoa nyasi na liwe safi ili kudhibiti magonjwa na wadudu, unyevu unahitajika ili kuongeza mavuno.

MAGONJWA &WADUDU

MAGONJWA

Zao la bamia pia hushambuliwa sana na ukungu uitwao ubwiri unga, pia hushambuliwa sana na utitiri mwekundu na aphids. Kwa hiyo kila wiki dawa ya ukungu na sumu ya wadudu ipuliziwe kwenye mimea ili kuweza kukua katika ustawi uliobora zaidi, pia ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo.

WADUDU
Mosaic Virus– Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoa madoa na huumuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

UVUNAJI
•Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
•Kiasi cha kilo 8000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.
•Hakikisha unavuna bamia na kikonyo chake, kisu kinaweza kutumika kwa kuvuna.

SOKO
Nchini Tanzania soko la bamia lipo. Inakadiriwa kuwa ifikapo kipindi cha masika bei ya bamia sokoni huwa juu. Hivyo mkulima atakayekuwa na mavuno ya bamia wakati wa masika anatarajiwa kuuza kwa bei ya juu kwa kuwa kipindi hicho zao hili huwa adimu katika soko.Ukilima eneo lenye ukubwa wa ekari 3 faida yake huwa kubwa zaidi kwani debe kidogoo cha lita 10 huwa 5000-6000 fedha za kitanzania.Ukilima kipindi cha kiangazi ambapo zao hilo huwa jingi sokoni hukadiriwa kidoo cha lita 20 huuzwa 3000-4000 fedha za kitanzania.

TIP: FAIDA ZA BAMIA KWENYE MWILI WA BINADAMU
Bamia ni miongoni mwa mboga za majani ambazo kwa kisayansi huitwa, ‘Abelmoschus Esculentus’.

Vitamini A itokanayo na bamia husaidia kuupa mwili wako kinga ya kupigana na maradhi. Kwa wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara kutaimairisha mwanga katika macho yako.

Wingi wa vitamini A huzuia maradhi yatokanayo na virusi kama mafua.

Uteute uliomo katika bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Watu wenye ngozi laini na zinazoteleza wana kiwango kikubwa cha ute ambacho husaidia kujenga ngozi.

Ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu na saratani za mdomo. Bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.

SOURCE:www.kilimotanzania.tk
---
View attachment 1500524Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine. Bamia huliwa kama matunda au hupikwa kama mboga pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine.
Mambo ya kuzingatia katika kilimo cha bamia

- Hakikisha unatumia mbegu bora

- Panda kwa nafasi

- Mwagilia maji ya kutosha kulingana na hali ya hewa

- Palilia shamba vizuri

- Dhibiti magonjwa na wadudu waharibifu kwa wakati

- Vuna kwa wakati unaotakiwa

Jinsi yakupanda

Mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja. Nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa aina ya bamia zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.

Namna ya Umwagiliaji

Kama unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.

Palizi

Hakikisha shamba ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona yamejitokeza ili kuongeza uzaaji wa bamia.

Wadudu waharibifu

Wadudu wanaoshambulia zao hili la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba na
utitiri mwekundu. Dhibiti wadudu hawa kwa kufuata njia zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo Kwenye eneo lako.
Magonjwa

Bamia hushambuliwa na magonjwa kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka huathiri zao la bamia hivyo ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo eneo ulipo.

Uvunaji wa bamia
View attachment 1500525

- Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.

- Unashauriwa kutumia kisu kuvunia na uhakikishe unavuna bamia na kikonyo chake ili kupunguza kuharibika kwa bamia

- Kiasi cha kilo 8,000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.

Soko la bamia

Soko la bamia ni kubwa sokoni mahitaji ni makubwa kuliko uzalishaji, unasubiri nini kuanza na kilimo hiki ujipatie kipato.
 
Mkuu hongera kwa aidia nzuri sana,

ninavyo fahamu kuhusu bamia kwa sasa soko lake ni kuuza kwenye masoko yandani kama kariakoo na kwingineko.

Ila kama utaweza kupaki freshi unaweza kju export kwenye soko la ulaya kuna demand ila kumeet standardzao c kitu cha mchezo.
 
bamia kwa siku hizi limekuwamoja ya mazao yenye faida kwa mkulima
mbegu zipo kwenye maduka ya pembejeo
zipo zinazokomaa kwa siku 45 na kuendelea
soko ni njenje kwa mijini
kipimo chake ni plastiki ya lita 20 na lita 10
bei inategemea na uwingi wake sokoni
lakinni haina hasara ya kutisha
 
Wakuu magonjwa yanayoishambulia bamia ni yapi na dawa zake. Afu pia nmesikia kuwa aina za bamia znapendelewa kutokana na eneo, kwa mfano Dodoma bamia zenye mgongo zinapendelewa sana kuna ukweli juu ya hili!?
 
bamia kwa siku hizi limekuwamoja ya mazao yenye faida kwa mkulima
mbegu zipo kwenye maduka ya pembejeo
zipo zinazokomaa kwa siku 45 na kuendelea
soko ni njenje kwa mijini
kipimo chake ni plastiki ya lita 20 na lita 10
bei inategemea na uwingi wake sokoni
lakinni haina hasara ya kutisha

bamia uzuri wake unachuma kipindi kirefu mno
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Habari wana JF,

Ningependa kufahamishwa kuhusu kilimo cha bamia ,mbegu bora ,dawa, muda kupanda hadi kuivuna.

Asanteni
 
Habari wana JF,

Ningependa kufahamishwa kuhusu kilimo cha bamia ,mbegu bora ,dawa, muda kupanda hadi kuivuna.

Asanteni

Na wewe ni mgeni JF? uliza swali ktk thread ya kilimo utajibiwa, au unafurahia kuanzisha thread yako?
 
Jamani tunaomba input zenu katika hili.

cc Malila

Asante,

Moja ya vitu niliyojifunza ktk kilimo ni kuto dharau mazao yasiyo na majina, kama vile bamia,ulezi,uwele,mbaazi na magimbi. Nilisafiri na jamaa mmoja, yy anauza ulezi tu,na anapiga ela kimya kimya.

Nirudi kwenye bamia soko la bamia ni la ndani zaidi na la uhakika. Kadri ulimwengu unavorudi kwenye organic materials,ndivyo ambavyo masoko ya vitu local yanavyopanda
 
Nililima Bamia kiangazi, za kumwagilia kwa pump!! Bei niliyopata nilipoanza ilikuwa 4000 ilishuka hadi 3000 kwa debe moja la ujazo wa lita 20.

Ustawi wa bamia ulikuwa wa kawaida nilikuwa natoa ndoo 13 kwa eneo la robotatu eka mavuno ni mara mbili kwa wiki. Naamini kwa ekari moja nigevuna debe 20. Kunastori watu huvuna debe 30 au zaidi kwa eka mimi hizo sikuziona.

Huwa zinashambuliwa sana na ukungu uitwao ubwiri unga, pia hushambuliwa sana na utitiri mwekundu na aphids. Kwa hiyo kila wiki dawa ya ukungu na sumu ya wadudu, ulipe mpiga dawa, petrol ya kumwagilia na malipo ya mmwagiliaji, wachumaji kila debe 1000/=.

Ili uone pesa ya bamia lima masika, lima eneo kubwa kama ekari kuanzia 3. Kumbuka eneo unalovuna debe 1 bamia eneo kama hilo ungevuna debe 10 za nyanya. bei ya bamia iikifikia chini ya 4000/= debe hailipi !!!!!
 
Back
Top Bottom