Kilimo bora cha Bamia za kisasa na Kangetakilimo

kangetakilimo

kangetakilimo

Tahadhari ni TAPELI
Joined
Jan 21, 2018
Messages
3
Points
45
kangetakilimo

kangetakilimo

Tahadhari ni TAPELI
Joined Jan 21, 2018
3 45

KILIMO BORA CHA BAMIA NA KANGETAKILIMO
KILIMO BORA CHA BAMIA NA KANGETAKILIMOAgro Project Tz
KILIMO CHA BAMIA

Bamia ni zao la Jamii ya mbogamboga linalotambulika kitaalamu kama Abelmoschus esculentus (OKRA) lenye asili ya Afrika ya magharibi. Kwa sasa zao hili linalimwa katika nchi nyingi hasa sehemu za joto. Baadhi ya maeneo yanayolima zao la bamia kwa Tanzania ni pamoja na ukanda wote wa nchi ya Tanzania,Kutoka mita 0-1500 kutoka usawa wa bahari zaidi ya hapo unaweza kulima lakini halivumilii hali ya baridi kali.Pia bamia hufanya vizuri zaidi katika maeneo yenye udongo wenye unyevu wa kutosha na joto la wastani wa nyuzi joto 25 - 30 C.Mvua hadi kiasi cha milimita 1000 cha mvua kwa mwaka.tu asili yake ni africa nchini Ethiopia ambapo kwa sasa linalimwa katika nchi nyingi.bamia ni moja kati ya mazao ambayo yanafaida sana ndani ya mwili kama kusafisha utumbo mpana husaidia kulainisha choo huongeza uroto kwa wale wenye upungufu wa uroto kwenye maungio pia ina vitamin C ambayo husaidia kulainisha ngozi na macho kuona

AINA ZA UDONGO
Kuna aina kuu tatu za udongo,
• Kichanga (Sand soil) –
una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.
• Tifutifu (Loam soil) –
unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa.
• Mfinyanzi (Clay soil) –
unahifadhi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.


Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni:
Ø Tindikali ya udongo
Ø Kiasi cha mboji
Ø Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium.
Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa. Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH)
PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0)

.Ila bamia Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katikakipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0


AINA YA UDONGO UNAOFAA KWA ZAO LABAMIA
BAMIA hustawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia halinaweza kulimwa katika udongo wenye asili yaMAANDALIZI YA SHAMBA LA BAMIA
Taarisha shamba lako mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita. Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi na masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.Magonjwa kama yale ya majani hayatatokea yatakuwa kidogo. Hupunguza magugu.Hupunguza wadudu waharibifu .Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na MIMEA kutastawi vizuri. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
1. Jembe la mkono - wengi wanatumia
2. Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
3. Power tillers
4. trekta

ZINGATIA
Tunashauliwa kupanda bamia katika matuta ili kusaidia mizizi kukua vizuri na udongo kuhifadhi maji. Wakati wa kiangazi, tengeneza matuta yaliyodidimia kidogo ili kufanya maji yaweze kukaa kwenye udongo na wakati wa masika matuta yainuliwe kidogo toka kwenye usawa wa ardhi ili kuzuia maji yasituame. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.

AINA ZA BAMIA
Kuna aina za bamia zinazo patikana kama vile1. Clemson spineless.
Ain ya bamia hii inatabia ya kukua urefu wa mita 1 hadi 1.5 na kuzaa bamia za kijani zenye urefu karibu sm 15. Huchukua siku 55 hadi 58 kuanza kuvuna.
2. Emerald green.
bamia hii ina tabia ya kukua hadi urefu wa m 1.5 na kuzaa bamia za kijani zenye urefu wa sm 18 hadi 20. Huchukua siku 58 hadi 60 kuanza kuvuna.
3. White velvet.
bamia hii inatabia ya kukua urefu wa m 1.5 hadi 1.8 na kuzaa bamia ndefu, nyembamba, zilizochongoka na zenye urefu wa sm 15 hadi 18.
UWANDAAJI WA MBEGU
Andaa mbegu mapema kwa kawaida inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji kwenye bustani. Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za bamia zinazoweza kupandwa na kutoa mavuno bora kama vile Lady’s Finger, Quim Bombo, Asutem, Mkulima-Clemson Spineless, Labadi Dwarf.

UPANDAJI WA BAMIA

Mbegu za bamia mara nyingi husumbua kidogo kuota kama patakuwa na hali ya baridi katika udongo.Hivyo ili ziote vizuri tunashauriwa kabla ya kuzipanda shambani ziloweke katika maji ya uvuguvugu kwa masaa 24 au ziloweke kwa dakika 30 katika ethly alcohol and acetone,.
panda mbegu zako katika mashimo uliyoyachimba katika udongo wenye unyevu kwa kina cha sentimeta 2 -3 katika nafasi ya sentimeta 60-90 kati ya mstari na msatari na sentimeta 25-50 Kati ya shina na shina utahitajika katika kila shimo uweke mbolea kwa ajili ya ukuaji mzuri wa Bamia zako
kutumia mbolea ya kuku au ng'ombe amabayo ni bora zaidi kwani ya kuku huisha kazi yake mapema zaidi katika udongo.Panda Mbegu mbili kwa kila shimo na zikisha ota ngolea uache shina moja kwa kila shimo.kiasi cha kilo 1.5 - 2.5 hutosha kwa ekari moja ambapo wingi wa mbegu itategemea uwezo wa mbegu kuota na aina ya bamia.Kama mbegu zako uwezo wake wa kuota ni mdogo mbegu zitatumika nyingi na kama unapanda bamia fupi au bamia zenye mbegu kubwa mbegu itatumika nyingi pia.Mbegu za bamia zinaweza kuchukua siku 8 - 10 kupanda hadi kuota.Pia bamia unaweza kupanda mbegu katika kitalu baadaye zikifikisha sentimeta 10-15 unazing'oa na kwenda kupanda shambani ila njia nzuri ni kupanda moja kwa moja shambani

PALIZI
Katika kilimo cha bamia ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda.nashauri kwamba katika kilimo cha cha bamia shamba lipaliliwe mara 1-2, kufuatana na hali ya magugu katika shamba.Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono kwa kung’olea au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (HERBCIDES).

MFUMO WAUMWAGILIAJI
Hali ya unyevunyevu ni mdogo katika shamba itahitajika uwe unamwagilia shamba lako kila baada ya siku 10 au pungufu kulingana na hali ya unyevu katika shamba lako.Kiasi cha wastani wa milimita 350 za maji katika siku 10 zinahitajika kwa ukuaji wa bamia ili uweze kupata mavuno yaliyo bora na mengi.na kama umepanda mbegu katika kipindi cha ukame zimwagilie kila siku kuhakikisha udongo wako unakuwa na unyevu wa kutosha ili kuwezesha mbegu zako kuota.

MBOLEA
Mbolea ni chakula cha mimea, ambayo ni mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali vinavyoongezwa kwenye udongo au vinavyowekwa moja kwa moja kwenye mimea ili kuongeza ukuaji na uzalishaji wa mimea.
Virutubisho hivyo ni pamoja na madini muhimu kama vile naitrojeni, fosfati na potashi. Madini mengine ni pamoja na salfa, chokaa (calcium), magnesium, boroni, shaba, chuma, manganese, molybedenum na zinki. Haya madini kwa asili, yanapatikana katika udongo kwa viwango tofauti. Yanapopungua kutokana na kilimo, inabidi yaongezwe kwa kutia mbolea.

Aina za mbolea
Kuna aina mbili kuu za mbolea ambazo ni:
1. Mbolea za asili (organic fertilizers)
2. Mbolea za viwandani (inorganic or industrial fertilizers)

Mbolea Za Asili (Organic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotokana na wanyama na mimea. Mbolea za asili ni kama vile:
i. Mbolea vunde: inajulikana pia kama biwi au compost. Hutokana na mchanganyiko wa manyasi au mabaki ya mbao na samadi na majivu.
ii. Samadi: kutoka kinyesi cha wanyama kama mifugo na ndege.
iii. Mbolea za kijani: hutokana na kupanda mimea aina ya mikunde ambayo hukatuliwa na kuchanganywa na udongo.
iv. Majivu: ni mbolea ya asili yenye madini aina ya potashi kwa wingi, fosfati, chokaa na magnesium.
v. Matandazo (mulch): ambayo baadaye yakioza huwa mbolea.

Mbolea Za Viwandani (Inorganic Fertilizers)
Hizi ni mbolea zinazotengenezwa viwandani kwa kutumia virutubisho mbalimbali kwa kufuata viwango maalum vilivyowekwa ili kukidhi mahitaji ya mimea. Mbolea hizi zinatengenezwa kwa lengo maalum la kupata aina na kiasi fulani cha kirutubisho/ virutubisho vinavyohitajika na mimea.

RATIBA YA MBOLEA KATIKA ZAO LA BAMIA
HATUA YA KWANZA

(Tunashauri Kapadia kwa Samadi kama ikiwepo)
NPK 15.9.20 +TE(yaramila winner) Gramu 10 kupanda bila kuweka samadi
Yara mila winner Gram 5 pamoja na samadi kwa shina / shina moja
Tenganisha kwa kuweka tabaka la udongo usio na mbolea kwa sentimita mbili kati ya mbengu na udongo uliyochanywa na mbolea
Epuka mbegu kugusana na mbolea inaweza kuungua na kushindwa kuota


HATUA YA PILI(A) KUWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KATIKA UDONGO
NITROBAR (CAN)
Weka mbolea ya kukuzia ya nitrobar wiki tatu baada ya mche kuota au mche wenye majani matatu(3)baada ya utokaji .
Weka mbolea ya ujazo wa kifuniko cha soda /kijiko kimoja kidogo cha chai sawa na gramu tano katika kila shina la mche mmoja
Weka mbolea kwa umbali wa kiasi cha sentimita 5 kutoka mzunguko wa shina alafu fukia zingatia kuweka mbolea hii mapema kabla ya kutoa maua


HATUA YA PILI (B) KUWEKA MBOLEA YA KUKUZIA KUPITIA MAJANI(BUSTA) BAMIA
MULT-K AND SUPERGRO/NPK+TE foliar –pulizia mbolea hii kwa miche ikiwa na majani matatu hadi manne ya kuchipua
Changanya MULT-K maganda matatu ya kibiriti katika maji ya lita 20 puliza juu ya majani ya mche
Rudia tena baada ya siku kumi na nne (14) zingatia kutumia mbolea,
Mbolea hii ni mtiririko wa mbolea ya kukuzia sambamba na nitrobar izingatie kutumia kabla ya maua
HATUA YA TATU KUWEKA MBOLEA YA UZALISHAJI WA MATUNDA YA
Maua na matunda yatakapotunga wiki ya sita na nane weka tena npk 15.9.20+ TE(yaramila winner) gram 10 kwa shina (kijiko cha chakula)
Weka mbolea au umbali wa nchi 6 mzunguko wa shina unaweza kuongeza gram 5 hadi 10 baada ya siku ya 21 kama kuna viashirio vya upungufu wa rutuba shambani kwa kuangalia ubora matunda na muonekano wa majani ya matikiti
WADUDU NA MAGONJWA YA BAMIA
1)WADUDU

A) Mdudu mafuta (aphids)
Hufyonza majimaji katika majani na bamia changa hivyo kusababisha bamia kutokuwa vizuri na bora.
Kinga na tiba
Tumia dawa za wadudu kama vile ABAMECTIN, NIMEBECIDIN FARMER GULD, ACTARA,n.k
B) MIilibagi (Mealy bug)
Ni wadudu wanaoganda katika majani,matawi na bamia wakifyonza maji maji ya mimea


Kuzuia na Kinga-Tumia dawa za wadudu kama vile selecron 720,Nimebecidin,multimectin,Dudu all,ninja nk n.k

c)Funza(Boll worm)
Hawa ni funza amabao hutoboa na kuharibu Bamia


Kinga na tiba
Kwa maeneo yanayoshambuliwa sana na wadudu,Puliza dawa za wadudu mara tuu bamia ziwekapo ua na zikiwa ndogo,Puliza asubuhi sana au jioni sana ili kuwakwepa wadudu wachavushaji wasije kufa na dawa wakati unapuliza.Puliza dawa kama vile Nimebedicin,albamectin n.k kuua wadudu hawa


d) Funga funga(Leaf roller)
hufunga majani kwa kuyavilingisha na kukaa na kula majani hayo.kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin,dudu all n.k


e) Inzi weupe (whitefly)
Ni waenezaji wakubwa wa magonjwa ya virusi, wadudu hawa hufyonza majimaji katika majani ya mimea na hujificha sana chini ya majani wakati wa jua kali.
kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin,dudu all,actara, n.k

f) Vinundu katika Mizizi(Root –knot nematodes)
Ni wadudu wadogo kama minyoo midogo ambao hula katika mizizi midogo na kusababisha uvimbe na mimea kusinyaa.kinga na tiba
tumia dawa kama vile NIMEBECIDIN (kwa kiasi kikubwa Chini ya shina La mmea), DAZOMET (BASAMID),CARBOFURAN(FURADAN) kuua wadudu hawa.Hizi ni dawa za ardhini.

2) MAGONJWA YA BAMIA
Bamia hushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama vile;

a) Ubwiri unga (Powdery mildew)
Ni ugonjwa unaosababishwa na fangasi(ukungu).ugonjwa ambao hufanya mmea kuwa na madoa au unga unga unga wa rangi ya kijivu katika majani na baadaye hunyauka na kufa na kupukutika majani.

TIBA NA KINGA
Liweke shamba lako katika hali ya usafi na Puliza dawa za ukungu zenye salfa kama vile copper sulphate, na siku za upuliziaji itategemea muda wa kulima bamia masika hupulizwa mara kwa mara na kiangazi hupulizwa mara chache.


b)Ugonjwa wa kujikunja na kudumaa majani (Leaf curl)
ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ni ugonjwa ambao huambatana na kujikunja kwa majani machanga na kuwa magumu na mmea kudumaa kukua.KUZUIA NA KINGA
-panda mbegu kinzani na ugonjwa huu,tumia madawa ya ukungu kama vile Copper sulphate, au puliza sulpha au copper (BONIDE).Pia tumia dawa za wadudu kuua wadudu kama nzi weupe ambao kwa kiasi kikubwa hueneza ugonjwa huu.


c) Ugonjwa wa manjano(Mosaic)
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi amabapo mmea ulioshambuliwa huwa na majani yenye umbo na ukubwa wa kawaida lakini yenye kijani kikavu au majani yenye rangi ya njano ambapo baadaye mmea hudumaa kukua.KUMBUKA rangi ya njano ya majani inaweza kusababishwa pia na ukosefu wa nitrojeni katika mmea hasa kama maji yatakuwa mengi ardhini katka udongo.


KUZIA NA KINGA
kukinga na kuzuia ugonjwa huu hakikisha unapanda mbegu kinzani na ugonjwa huu.zui wadudu katika shamba lako kwani wanaweza kueneza
ugonjwa huu shambani kwako.Jiadhari na uvutaji au ubebaji wa sigara/tumbakukatika shamba la bamia wakati unatembea au unafanya kazi katika shamba la bamia.Ng'oa mashina yaliyoathirika mapema na uyachome moto mbali na shamba.lima kilimo cha mzunguko wa mazao tofauti na jamii ya bamia.

10. JINSI YA KUVUNA BAMIA
Bamia huwa tayari kuanza kuvunwa mwezi 1 tangu kupandwa na huckukua siku 6 kuvunwa baada ya kuanguka.kama matunzo ni mazuri kila ua katika mabamia litatowa bamia.chuma vizuri bamia kutoka katika mbamia bila kuacha athari kubwa katika mche wa mbamia.
Hivyo kwa uvunaji mzuri unaweza kutumia mkasi mkali katika kukata vikonyo vya bamia.chuma bamia kubwa na ndogo ziache ziendelee kukua,ila inakubidi uwe mwangalifu ili bamia zisije kukomaa shambani kwani hukomaa kwa haraka zaidi na zilizokomaa hazina soko zuri na hazipendwi na walaji kwani huwa gumu na nyuzinyuzi nyingi.
Katika matunzo mazuri unaweza kuendelea kuchuma bamia kutoka katika mibamia kwa muda wa miezi miezi 2 na zaidi.

MAVUNO
wingi wa mavuno hutegemea matunzo na aina ya mbegu za bamia,muda wa upandaji na kukua-baridi ikiwa kali mavuno yake hupungua na mara za uchumaji wa bamia-kadri zinavyochumwa mara nyingi ndivyozinavyozidi kuzaa na zile zinazozachumwa kwa muda mrefu ndizo zenye manufaa kwa mkulima , japokuwa kwa wastani bamia huvunwa kiasi cha tani 3 - 10 kwa ekari


11.UHIFADHI WA BAMIA

Bamia ni kama mazao mengine ya mbogamboga haistahimili kukaa muda mrefu bila kuliwa na kadri inavyokaa muda mrefu baada ya kuvunwa ndipo hupoteza ubora wake.Kama kuna soko hakikisha unazivuna na kuzipeleka sokoni.
Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo

TEMBELEA MAKALA ZANGU KWENYE MTANDAO KANGETAKILIMO
· Kilimo cha mihongo na mazao yote ya nafaka kama ufuta mbaazi ,choroko,mahindi ,karanga,nk
· Kilimo cha vitunguu,pilipli,nyanya na mazao yote ya mbogamboga
· Kilimo cha matunda kama mipesheni mipapai,michungwa,nk
· Ufugaji wa kuku wa kienyeji kisasa


 
Last edited by a moderator:
jozzeva

jozzeva

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2012
Messages
2,064
Points
2,000
jozzeva

jozzeva

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2012
2,064 2,000
Shukrani kwa elimu mkuu.
 
kichakaa man

kichakaa man

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Messages
3,067
Points
2,000
kichakaa man

kichakaa man

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2011
3,067 2,000
Aiseee asante kwa somo zuri
 
Come27

Come27

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2012
Messages
4,943
Points
2,000
Come27

Come27

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2012
4,943 2,000
Tunashukuru Kwa darasa hili la kilimo. Alafu hayo masomo mengine na yenyewe ungeyatagi apo chini tusome kuliko kuanza kutafuta. Ila shukrani sana ndugu. Tunaomba kama moderator utaweza ukayatagi hayo masomo mengine tukajifunza ndugu.
Jamiii Forum darasa langu na shule yangu
 
Last edited:
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
9,030
Points
2,000
Tutor B

Tutor B

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
9,030 2,000
Vipi kuhusu yale mabamia makubwa yana shida gani? Yanastawi vizuri lakini naona sokoni watu hawayachangamkii.
 
Mwamba028

Mwamba028

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2013
Messages
3,993
Points
2,000
Mwamba028

Mwamba028

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2013
3,993 2,000
Kilimo sio lelemama

Ahsante mtoa mada kwa maelezo yaliyojitosheleza
 
A

antimatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2017
Messages
1,921
Points
2,000
A

antimatter

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2017
1,921 2,000
Thanks.. Vinundu kny mizizi unajuaje kama vipo ili utie dawa?? Unachimba kuangalia au unaweka dawa tu?
 
miminimkulimaakachekasana

miminimkulimaakachekasana

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2017
Messages
1,853
Points
2,000
miminimkulimaakachekasana

miminimkulimaakachekasana

JF-Expert Member
Joined May 29, 2017
1,853 2,000
clemson spineless ziko bomba
 
successor

successor

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2012
Messages
3,028
Points
2,000
successor

successor

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2012
3,028 2,000
Hili somo limekuja muda muafaka. Shukrani mkuu.
 
kangetakilimo

kangetakilimo

Tahadhari ni TAPELI
Joined
Jan 21, 2018
Messages
3
Points
45
kangetakilimo

kangetakilimo

Tahadhari ni TAPELI
Joined Jan 21, 2018
3 45
Tunashukuru Kwa darasa hili la kilimo. Alafu hayo masomo mengine na yenyewe ungeyatagi apo chini tusome kuliko kuanza kutafuta. Ila shukrani sana ndugu. Tunaomba kama moderator utaweza ukayatagi hayo masomo mengine tukajifunza ndugu.
Jamiii Forum darasa langu na shule yangu
asnate sana ntajitahidi zaidi
 
M

mapenz matam

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
212
Points
250
M

mapenz matam

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2012
212 250
Asante sana kwa somo zuri kaka
 
kivyako

kivyako

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2012
Messages
14,116
Points
2,000
kivyako

kivyako

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2012
14,116 2,000
Asante kwa shamba darasa
 
TATA MKURIA

TATA MKURIA

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2015
Messages
205
Points
250
TATA MKURIA

TATA MKURIA

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2015
205 250
Mkuu...
God bless you! Nitakutafuta kwenye cm kwa ushaur zaid. Ila nauliza huku Mwanza City hamjafikiria kufika? Au tayari mpo niwacheki katika ofisi zenu.
Asante
 

Forum statistics

Threads 1,334,772
Members 512,099
Posts 32,486,481
Top