Kilimarathon mmejishushia credibility kwa kumpa Haji Manara medali huku akipanda pikipiki

Architect E.M

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,211
1,360
Heshima kwenu wadau.

Nimesikitishwa na kitendo hichi na kinawashushia credibility sana. Medali maana yake mtu ameitolea jasho, amefanya mazoezi na kujiandaa na ashiriki mbio zote mwanzo mpaka mwisho kwa miguu yake bila kutumia chombo cha moto.

Iweje Manara apande pikipiki na picha zikazagaa mtandaoni na bado mkampa medali?

Hiyo inawaharibia credibility na inashusha hadhi ya ile medali kwamba kumbe hata nikipanda toyo ntaipata.

Si vyema na mlirekebishe hili tafadhali. Ikibidi manara anyang'anywe ile medali mliompatia.

Naomba kusilisha.

Ndimi mshiriki wa kili half marathon 2020.
 
Medali hazifanani,zipo wanaopewa walio shiriki just for funny.anapewa yeyote aliyeshiriki maana kachangia ,Kama sikosei,kundi ilo ata ukikombia ukaja kudandi baiskeli ,medali unapewa
 
Roho mbaya tu ungechukua boda nawewe. Ina maana zile medali wangepewa washindi kumi tu kila Category we ungefaidika nini!

Medali ziko za material tofauti tofauti, unaweza kuta zile za kupewa asante kwa kushiriki ndio aliyopewa Manara n wengine wote ambao wanafuata baada ya Top Ten.
 
sijaona kama manara kavunja sheria yoyote ya nchi hapo .
Maana hata kwenye tatu bora hayupo.
alikuwa bora liende wengi ni wasindikizaji tu . hawana madhara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sijaona kama manara kavunja sheria yoyote ya nchi hapo .
Maana hata kwenye tatu bora hayupo.
alikuwa bora liende wengi ni wasindikizaji tu . hawana madhara

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijasema manara kavunja sheria ya nchi. Soma uzi na uuelewe. Nimesema Kilimarathon wanajishushia credibility kwa kumpa mtu ambae hakukimbia medali... wameifanya medali soo cheap kwa kumoa mtu aliepanda bodaboda badala ya kukimbia kwa miguu yake afeel ile pain ya kutoka jasho na kuumwa misuli siku ya mbio bila kusahau kufanya mazoezi na kujiandaa wiki nyingi kabla ya mbio
 
Roho mbaya tu ungechukua boda nawewe. Ina maana zile medali wangepewa washindi kumi tu kila Category we ungefaidika nini!

Medali ziko za material tofauti tofauti, unaweza kuta zile za kupewa asante kwa kushiriki ndio aliyopewa Manara n wengine wote ambao wanafuata baada ya Top Ten.
Manara amepewa medali ya finisher wa 21kms.. lakini amefinish kwa kutumia pikipiki na si miguu yake.. kipi ambacho hujaelewa mkuu.?
 
Attachments

  • Screenshot_20200302-151334.jpg
    Screenshot_20200302-151334.jpg
    123.5 KB · Views: 1
Heshima kwenu wadau.

Nimesikitishwa na kitendo hichi na kinawashushia credibility sana. Medali maana yake mtu ameitolea jasho, amefanya mazoezi na kujiandaa na ashiriki mbio zote mwanzo mpaka mwisho kwa miguu yake bila kutumia chombo cha moto.

Iweje Manara apande pikipiki na picha zikazagaa mtandaoni na bado mkampa medali?

Hiyo inawaharibia credibility na inashusha hadhi ya ile medali kwamba kumbe hata nikipanda toyo ntaipata.

Si vyema na mlirekebishe hili tafadhali. Ikibidi manara anyang'anywe ile medali mliompatia.

Naomba kusilisha.

Ndimi mshiriki wa kili half marathon 2020.
Labda walimuweka kwenye makundi maalum mkuu

macson
 
  • Thanks
Reactions: Gef
Back
Top Bottom