Kilimanjaro: Wanawake wa Kimasai wamlilia Rais Samia kumsamehe Sabaya, Wamtumia mtoto mchanga kama chagizo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,638
218,071
Hii ndio Taarifa mpya ambayo imetufikia hivi punde kutoka huko Mahakamani Moshi Mkoani Kilimanjaro , ambapo leo Mtuhumiwa wa unyang'anyi wa kutumia silaha za moto Ole Sabaya amefikishwa Mahakamani .

Wanawake wa Kimasai kutoka Hai wamemuombea Msamaha Ole Sabaya kwa Rais wa Nchi Samia Suluhu , kwa kutumia mtoto mchanga ambaye bado hakukatika kitovu aliyekuwa analia sana , huku wao wakiomba msamaha kwa pamoja (Bila shaka ni mambo ya kimila).

Kilichonifurahisha ni kwa Wamama hao wa Kimasai KUKIRI WAZI KWAMBA SABAYA ALIFANYA MAKOSA MENGI , lakini wanamuomba Mh Rais amsamehe na kumkanya ili aishi maisha mema hapo baadaye kama binadamu wengine.

Chanzo: Mwananchi
 
Sijui kama wana hofu ya kweli au nao wanatumwa kutuchezea mchezo ili mwisho wa siku Sabaya akiachiwa huru ionekane ni huruma ya Samia ndio imemtoa gerezani.

Binafsi kwa namna mambo yanavyoendelea kwenye kesi za Sabaya sioni ugumu wowote uliopo mbele yake, anashinda kesi kila siku, hao wanawake sijui wanalilia kitu gani, nahisi wametumwa tu.
 
sioni ugumu wowote uliopo mbele yake, anashinda kesi kila siku
kwa hiyo hapo atatoka kifue mbele kwamba ameshinda kesi au mbeleko ndo imetabaruku?
afu Mbwa mmoja anataka kulinganisha mwenendo wa kesi ya Sabaya na Mbowe, khaa!!!
 
Sabaya ni mwanaume anapambana kuzipangua Moja baada ya nyingine Kuna gaidi mmoja wa kichaga mpaka wakuu wa dino walimuombea ndiyo akatoka sabaya Hana hatia kesi ya mchongo hiyo kutoka kwa Wala rushwa na magendo wa hai
 
Sabaya ni mwanaume anapambana kuzipangua Moja baada ya nyingine Kuna gaidi mmoja wa kichaga mpaka wakuu wa dino walimuombea ndiyo akatoka sabaya Hana hatia kesi ya mchongo hiyo kutoka kwa Wala rushwa na magendo wa hai
Aibu yao ndio imemtoa jela,toka lini wakawa na upendo huo.
Akaunti zake zishafunguliwa soon atapewa bilicanas yake tukaukumbuke ujana pale
 
Huu utaratibu wa kuombea msamaha watuhumiwa utakuja kutujazia majambazi na majizi ya fedha za umma kwa wingi nchini.

Imagine unakwapua fedha ya serikali/kufanya uhalifu ukuwa na uhakika wa kuombewa msamaha na kina Mama na ukaachiwa huru!

Mama nae aache mahakama ifanye kazi yake, kama hana hatia mahakama itasema.
 
Back
Top Bottom