Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,847
- 15,252
Ukifika mkoani Kilimanjaro utaona ni jinsi gani kizazi hiki kinavyoenda kubadili kabisa aina ya kilimo cha kahawa kilichozoeleka tangu enzi ya mkoloni.
Vijiji vichache nilivyotembelea katika wilaya ya Hai na wilaya ya moshi vijijini nimejionea wanavijiji wengi wakiwa wameondosha kabisa zao la kahawa shambani na kuweka aina Moja tu ya mazao ambayo ni ndizi kama zao la biashara,
Na baadhi ya wanakijiji wachache wakiondoa zao la ndizi pamoja na kahawa na Kupanda matunda mbalimbali kama vile mapapai, machungwa, parachichi, embe nk. kwa ajili ya biashara.
Sababu mojawapo walizotaja kuwa ni kutokana mfumo wa Maisha ya sasa, maisha ya zamani ni tofauti na sasa, kwa kuwa kilogram moja ya kahawa haitoshi hata kununua nyama lakini akiuza ndizi mkungu mmoja ni afadhali kuliko kilo ya Kahawa.
Soko la ndizi ndani ya Nchi ni kubwa kwa sasa kutokana na kuwa magari ya mizigo kutoka Dar es Salaam na Mkoa kama Iringa hufika hadi huku vijijini ndani kabisa kutafuta ndizi hasa ndizi aina ya malindi ambazo zinapendwa na Wengi.
Unafuu wa gharama katika kutunza shamba la ndizi ni afadhali kuliko utunzaji wa kahawa ambao gharama zake ni kubwa ikiwa ni pamoja na kupiga dawa mara Kwa mara, na hata uvunaji wa kahawa ni msimu mmoja kwa mwaka kulinganisha na ndizi.
Baadhi ya wakulima waliopanda Matunda tofauti tofauti kwa kuondoa kahawa na ndizi wamedai kuwa achia mbali soko la ndani idadi kubwa ya wakenya hufuata mzigo wenyewe tena Ukiwa shambani kwa hiyo mkulima hasumbuki kutafuta masoko.
Elimu, kupata elimu kwa vijana kumesaidia sana mabadiliko haya ya Kilimo ambayo wengi wanaona ni kizuri zaidi kuliko aina. Ya. Kilimo kilicho kuwepo hapo kabla ambapo kahawa, ndizi matunda nk vyote vililimwa kwa pamoja katika shamba moja na hivyo kupelekea mavuno machache
Wakulima wengi wameanza kuchukua hatua katika aina hii mpya ya kilimo chenye tija kwa mkulima