Kilimanjaro: Walimu wapandishwa kizimbani kwa kughushi nyaraka ili kupata mafao NSSF

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
TAKUKURU Mkoani humo imewafikisha Mahakamani Goldina Peter Minja, Rose Koshuma Msangi na Nicodemus Felician Kavishe. Goldina aliwasilisha nyaraka zenye maelezo ya uongo ya "Ukomo wa Ajira yako"

Rose aliwasilisha nyaraka zisizo za kweli ili alipwe mafao ilihali bado ni mtumishi, na Nicodemus alijipatia 26,001,383.85 za fao la kukosa ajira kwa njia za udanganyifu

==

MAHAKAMA ya Wilaya ya Same leo Juni 1 7, 2021 imemlkuta na Inatia aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mpinji, wilaya ya Same mkoani ilimanjaro kwa kosa la kijipatia shilingi rnillioni tatu kwa njia ya udangafiyifu toka kwa mfanyabiashara , kwa mjibu wa kifungu cha 302 kanuni za adhabu, kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Kesi hiyo ilikuwa imefunguliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupam ana na Rushwa (W) ya Same, mwaka 2020 na kupewa namba ya shauri la jinai C 51/2020 na ilikuwa inasikilizwa na Mheshimiwa Hakimu Judith Kamała am apo mahakama hiyo baada kujiridhisha na Ushahidi uliotołewa kwamba mshitakiwa Aston Elinazi

Mgonja alitenda kosa hilo ilimtia hatiani.

Kesi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na wakili wa TAKUKURU, Samwelİ Gabriel ambaye aliieleza mahakama ya kwamba katika kipindi cha mwaka 2018 ambapo mshitakiwa alikuwa Diwani alichukua fedha kwa njia za udangarıyifu toka kwa bi. şifa Aron kwa kumdanganya kuwa atampatia kibali cha kueııdesha biashara ya duka la dawa za binadamu huku akifahamu wazi kwamba yeye hana mamlaka ya kutoa kibali hicho.

Mshitakiwa amepelekwa jela kwa ajilİ ya kutumikia kifungo chake cha miaka mitano.

17/6/2021 ambapo washitakiwa watatu walifanya makasa nıbali mba[i kwa mujibu wa sheria ya kanuni za adhabu

Washitakiwa bao walifıkishwa mahakamani na kusomewa mashitaka na wakili wa TAKUKURU, Furahirıi Kibanga katika Mahakama ya Wilaya Moshi ambapo Kesi namba 239/2021 inamkabili Goldina Peter Millja (57) ilifunguliwa, na mshitakiwa anakabiliwa na makasa matıne, kosa la kwanza katika kipindi cha tarehe 30/8/2020 alighushi barua iliyokuwa na maelezo "ukomo wa ajira yaka” ikionyesha imeandikwa na Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Majengo huku akijua alilaıwa bado ni mtumishi wa Majengo sekondari, kosa lake la pili ni kutengeneza 'certificate of service' ikionyesha kuwa alikuwa mtumishi [angu 1994 hadi 2020 iliyosainiwa na makamu mkuu washule ya Majengo sekondari kosa la tatu ni la laıwasilisha nyaraka za kughushi kwenye mfuko wa jamii, NSSF zenye maelezo ya uongo ya ('Ukomo wa ajira yako” na kosa la nne kuwasilisha ' 'certifıcate of service" katika mfuko wa jaınİİ NSSF İkionyesha zimeandikwa na kusainiwa na Makamu IT)kuu wa shule ya sekondari ya Majengo.

Mshitakiwa mwingine aliyefunguliwa kesi namba CC337/2021 ni Rose Koshuma Msangi , ambaye kesi yake ipo mbele ya Mheshimiwa hakimu Masati wa mahakama ya wilaya ya Moshi, ambapo mshitakiwa alishitakiWa kwa makosa rnanne ambapo kosa la kwanza ni la kughushi "certificate of service" ilieleza kuwa alikuwa ni mtumishi wa majengo sekondari katika kipindi Cha mwaka 2006 hadi tarehe 30 Apriii 2020 kama mtumish wa ajira ya muda, kos•4 la pili, lilikuwa ni la kughushi barua yenye maelezo "mkataba wa ajira ya muda k isha" na wakati alikua bado anaendelea na ajira yake katika shule ya majengo n Rosa la tatil ni kuwasilisha nyaraka za uongo katika mfuko wa NSSF ili ali we mafao huku akijua bado ni mtumishi.

Kesi ya tatu, ambayo ipo mbele ya mheshimiwa Naomi Mwirind wa mahakama ya Wilaya ya Moshi, ambapo Inshitakiwa Nicodemus Feliciqn Kavishe (43) ambaye amefunguliwa kesi namba 238/2021, alisomewa mashitaka sita ambapo kosa la kwanza ni, kughushi barua ya kuachishwa kazi wakati kweli , kosa la pili ni la kuwasilisha katika mfuko wa NSSF barua ya kuachishwa kazi wakati siyo kweli , kosa la tatu ni la kughushi "certificate of service" kosa la nne ni kuwasilisha katika mfuko wa jamii NSSF nyaraka zenye maelezo Ya uongo . Kosa la tano ni kwa njia za udanganyifu aliweza kujipatia fao la kukosg ajira kiasi cha shilingi millioni 26,001,383.85 wakati bado ni mtumishi.

Mshitakiwa huyo, alnekosa dhamana na kupelekwa mahabusu ya magereza ya karanga hadi tarehe 25/6/2021 kesi hiyo itakapotajwa tena
 
TAKUKURU Mkoani humo imewafikisha Mahakamani Goldina Peter Minja, Rose Koshuma Msangi na Nicodemus Felician Kavishe. Goldina aliwasilisha nyaraka zenye maelezo ya uongo ya "Ukomo wa Ajira yako"

Rose aliwasilisha nyaraka zisizo za kweli ili alipwe mafao ilihali bado ni mtumishi, na Nicodemus alijipatia 26,001,383.85 za fao la kukosa ajira kwa njia za udanganyifu
Halafu wote ni wa ukanda ule. Dah
 
Sometime nikiona walioajiriwa wanavyoteseka naona hata mie nikiwa jobless ni sawa tu.
Yaani nachoomba nisije nikaajiriwa hela zangu zikaenda humo.

Kama wananipenda eti waje kunitunza ukubwani kwani mbunge wao hawampendi jamani.
Nashukuru nachopata tunamalizana hapo hapo so hata akili imeshkaa sawa.

Ila pia ili suala ningeshangaa mangi asingekuwemo Mana hao jamaa kwa kuiba kwa pen Nyerere akasome
 
Mil 26 mkuu.

Yaani mzee baba aligushi barua ya "Ukomo wa Ajira" ili aonekane amestaafu akala mzigo.
Akaendelea na ajira?? Shubamiti! Nadhani huyu mwalimu ni vyeti feki na wanafunzi wake watakuwa hawajawahi kufaulu masomo anayofundisha.

Kwanza 26M ni ndogo mno. Sidhani hata ka inanunua Harrier matako ya nyani!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Akaendelea na ajira?? Shubamiti! Nadhani huyu mwalimu ni vyeti feki na wanafunzi wake watakuwa hawajawahi kufaulu masomo anayofundisha.

Kwanza 26M ni ndogo mno. Sidhani hata ka inanunua Harrier matako ya nyani!

Everyday is Saturday............................... :cool:
Pesa yake inamtia jela, Sheria zingine za kikuda Sana

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Akaendelea na ajira?? Shubamiti! Nadhani huyu mwalimu ni vyeti feki na wanafunzi wake watakuwa hawajawahi kufaulu masomo anayofundisha.

Kwanza 26M ni ndogo mno. Sidhani hata ka inanunua Harrier matako ya nyani!

Everyday is Saturday............................... :cool:

Mkuu, hiyo pesa ni ndogo kwa mipango yako wewe. Lakini pengine kwa mahitaji ya mipango yake angetoboa!
 
Back
Top Bottom