Kilimanjaro: Vyama vya watumia maji vyasema Sabaya aliwapora mabilioni

Duniahadaa

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
336
677
Hai. Bodi saba za watumia maji wilayani Hai, Siha na Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro zimeibuka na tuhuma nzito kwamba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya aliwapora mali za mabilioni.

Bodi hizo zimeiomba Serikali kuingilia kati sakata hilo ili warejeshewe mali zenye thamani ya zaidi ya Sh1 bilioni, magari sita na Sh350 milioni ambazo zilikuwa chini ya bodi ya wadhamini ya mradi wa maji wa Water Service Facility (WSF).

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alipotafutwa na gazeti hili jana kuzungumzia sakata hilo alikiri kulifahamu na kueleza kuwa amepanga kufika katika wilaya hiyo hivi karibuni ili kulitolea uamuzi na hatua zaidi.

“Leo sitazungumza juu ya hilo japo nalifahamu, ila nimepanga hivi karibuni kufika huko kutolea uamuzi suala hilo kwa hiyo mje siku hiyo,” alisema Aweso.

Kwa sasa Sabaya yupo katika Gereza la Kisongo jijini Arusha na wenzake watano akikabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya wizi wa kutumia silaha, utakatishaji fedha, kuunda genge la kihalifu na kujihusisha na rushwa.

Malalamiko
Bodi hizo za watumia maji zinahudumia zaidi ya vijiji 156 vya wilaya ya Siha, Hai na Moshi vyenye zaidi ya watu 400,000 ambapo Mwenyekiti wa WSF, Julius Mollel alisema mali hizo ziliporwa na Sabaya na mpaka sasa hawajui zilipo.

Mollel, ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya watumia maji Magadini Makiwaru, alisema WSF ni chombo kilichoanzishwa kisheria mwaka 2011 kikiwa na lengo la kuunganisha nguvu ya bodi hizo saba ili kutoa huduma bora ya maji.

“Chombo hiki (WSF) kilianzishwa kwa makusudi na bodi hizi saba kwa ajili ya kuunganisha nguvu ya pamoja na kilisaidia kurudisha huduma ya maji kwa haraka pindi kulipotokea uharibifu wa miundombinu,” alisema Mollel.

Lakini Oktoba 2018, mwenyekiti huyo alisema “tulivamiwa na aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya bila kufuata utaratibu akatukamata akatuweka ndani kwa saa 48 bila kuhojiwa jambo lolote na mali za WSF zikachukuliwa.”

Katika mali zilizochukuliwa alisema yamo magari sita, fedha taslimu Sh357 milioni na vipuri na vifaa vya mabomba vyenye thamani ya zaidi ya Sh1 bilioni ambavyo hawajui vilikopelekwa wala utaratibu uliotumika kuvichukua.

“Uporaji huu haukuzingatia sheria na WFS ni chombo kilichoundwa kisheria, tunamuomba Rais wetu Samia Suluhu Hassan atusaidie. Kwa sasa tunapata shida kukarabati miundombinu iliyoharibika hususan kipindi cha mvua.

“Tulikamatwa kama wezi wakati hatukuwa wezi na hatujaiba kisha mali zetu zikapelekwa kusikojulikana na kuziacha bodi katika mazingira magumu.

“Kwa kuwa sikio la mama (Rais Samia Suluhu) ni jepesi kusikia na hapendi watu kuonewa, kwa njia isiyo halali, tunamwomba atusaidie mali hizi za wananchi wa Siha, Hai na Moshi Vijijini zirejeshwe ili ziwasaidie kuboresha huduma,” alisema Mollel.

Mwenyekiti wa Bodi ya Watumia Maji Lawate Fuka, Yohana Laizer alisema baada ya mali za WSF kuchukuliwa, walipewa miezi sita ya uangalizi lakini sasa ni zaidi ya miaka miwili hakuna kinachoendelea wala hatua zozote zilizochukuliwa.

“Tunamuomba Rais Samia Suluhu atusaidie maana tangu chombo hiki kimesimamishwa na mali zake kuchukuliwa hatujui zilipo na wala hatuoni chombo kinachofanya kazi kusimamia bodi hizi kwa niaba ya WSF. Serikali isaidie tufahamu mali zile na vifaa vilipo na kama WSF haiwezi kusimamia bodi hizi na mali zile basi tuambiwe zilipo na ni nani anawajibika nazo maana tangu zichukuliwe bodi zinataabika kuboresha miundombinu,” alisema.

Alieleza kuwa, kuchukuliwa kwa magari yale likiwemo la majitaka kumesababisha usumbufu kwa wananchi ambao walikuwa wakilipia Sh70,000 kwa uzoaji wa majitaka lakini sasa wanalazimika kutoa Sh200,000 kupata huduma hiyo.

Laizer alisema wamelalamika mara kadhaa kwenye mamlaka mbalimbali za Serikali na kuambiwa wasubiri suala hilo linashughulikiwa na hata taasisi za kiuchunguzi ambazo waliziomba ziwasaidie bado hazijawapa majibu nini kinaendelea.

Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe, pia amewahi kuzungumzia sakata hilo katika kikao cha ushauri cha mkoa hata bungeni, akiomba fedha na vifaa hivyo virejeshwe Hai, ili kushughulikia tatizo la maji.

chanzo: MWANANCHI, JULAI 10
 
Hapo hai mlikuwa mnaishi kwa kukimbizwa na mtu mmoja tena mshamba.Hadi kwenye maji?
Hakuna wazee hapo hai?
Hapakuwa na uongozi wa CCM?
Viongozi wa Dini na kamati za amani hawapo?

Hakika Mkuu wa Mkoa alikuwa wakuja

2800389_IMG_20210607_041822.jpg
 
Bahati sana haya mambo angeyafanya kule tarime

Au maeneneo ya bariadi, Sumbawanga au kigoma

Angekuwa marehemu hata kabula ya Magufuli
Ukweli mkuu, haya Mambo angekuwa kigoma angerambishwa kinyesi kuna mmoja alikuja na Moto wilaya ya kasulu alilazwa nje Mara mbili
 
Iko hivi: Ungefanyia huko kwingine Jiwe mwenyewe angeweza akakushughulikia. Ila kwa Hai inaweza kuwa ni maagizo kutoka juu. Na promotion inafuata.
 
Hai. Bodi saba za watumia maji wilayani Hai, Siha na Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro zimeibuka na tuhuma nzito kwamba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya aliwapora mali za mabilioni.

Bodi hizo zimeiomba Serikali kuingilia kati sakata hilo ili warejeshewe mali zenye thamani ya zaidi ya Sh1 bilioni, magari sita na Sh350 milioni ambazo zilikuwa chini ya bodi ya wadhamini ya mradi wa maji wa Water Service Facility (WSF).

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alipotafutwa na gazeti hili jana kuzungumzia sakata hilo alikiri kulifahamu na kueleza kuwa amepanga kufika katika wilaya hiyo hivi karibuni ili kulitolea uamuzi na hatua zaidi.

“Leo sitazungumza juu ya hilo japo nalifahamu, ila nimepanga hivi karibuni kufika huko kutolea uamuzi suala hilo kwa hiyo mje siku hiyo,” alisema Aweso.

Kwa sasa Sabaya yupo katika Gereza la Kisongo jijini Arusha na wenzake watano akikabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya wizi wa kutumia silaha, utakatishaji fedha, kuunda genge la kihalifu na kujihusisha na rushwa.

Malalamiko
Bodi hizo za watumia maji zinahudumia zaidi ya vijiji 156 vya wilaya ya Siha, Hai na Moshi vyenye zaidi ya watu 400,000 ambapo Mwenyekiti wa WSF, Julius Mollel alisema mali hizo ziliporwa na Sabaya na mpaka sasa hawajui zilipo.

Mollel, ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya watumia maji Magadini Makiwaru, alisema WSF ni chombo kilichoanzishwa kisheria mwaka 2011 kikiwa na lengo la kuunganisha nguvu ya bodi hizo saba ili kutoa huduma bora ya maji.

“Chombo hiki (WSF) kilianzishwa kwa makusudi na bodi hizi saba kwa ajili ya kuunganisha nguvu ya pamoja na kilisaidia kurudisha huduma ya maji kwa haraka pindi kulipotokea uharibifu wa miundombinu,” alisema Mollel.

Lakini Oktoba 2018, mwenyekiti huyo alisema “tulivamiwa na aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya bila kufuata utaratibu akatukamata akatuweka ndani kwa saa 48 bila kuhojiwa jambo lolote na mali za WSF zikachukuliwa.”

Katika mali zilizochukuliwa alisema yamo magari sita, fedha taslimu Sh357 milioni na vipuri na vifaa vya mabomba vyenye thamani ya zaidi ya Sh1 bilioni ambavyo hawajui vilikopelekwa wala utaratibu uliotumika kuvichukua.

“Uporaji huu haukuzingatia sheria na WFS ni chombo kilichoundwa kisheria, tunamuomba Rais wetu Samia Suluhu Hassan atusaidie. Kwa sasa tunapata shida kukarabati miundombinu iliyoharibika hususan kipindi cha mvua.

“Tulikamatwa kama wezi wakati hatukuwa wezi na hatujaiba kisha mali zetu zikapelekwa kusikojulikana na kuziacha bodi katika mazingira magumu.

“Kwa kuwa sikio la mama (Rais Samia Suluhu) ni jepesi kusikia na hapendi watu kuonewa, kwa njia isiyo halali, tunamwomba atusaidie mali hizi za wananchi wa Siha, Hai na Moshi Vijijini zirejeshwe ili ziwasaidie kuboresha huduma,” alisema Mollel.

Mwenyekiti wa Bodi ya Watumia Maji Lawate Fuka, Yohana Laizer alisema baada ya mali za WSF kuchukuliwa, walipewa miezi sita ya uangalizi lakini sasa ni zaidi ya miaka miwili hakuna kinachoendelea wala hatua zozote zilizochukuliwa.

“Tunamuomba Rais Samia Suluhu atusaidie maana tangu chombo hiki kimesimamishwa na mali zake kuchukuliwa hatujui zilipo na wala hatuoni chombo kinachofanya kazi kusimamia bodi hizi kwa niaba ya WSF. Serikali isaidie tufahamu mali zile na vifaa vilipo na kama WSF haiwezi kusimamia bodi hizi na mali zile basi tuambiwe zilipo na ni nani anawajibika nazo maana tangu zichukuliwe bodi zinataabika kuboresha miundombinu,” alisema.

Alieleza kuwa, kuchukuliwa kwa magari yale likiwemo la majitaka kumesababisha usumbufu kwa wananchi ambao walikuwa wakilipia Sh70,000 kwa uzoaji wa majitaka lakini sasa wanalazimika kutoa Sh200,000 kupata huduma hiyo.

Laizer alisema wamelalamika mara kadhaa kwenye mamlaka mbalimbali za Serikali na kuambiwa wasubiri suala hilo linashughulikiwa na hata taasisi za kiuchunguzi ambazo waliziomba ziwasaidie bado hazijawapa majibu nini kinaendelea.

Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe, pia amewahi kuzungumzia sakata hilo katika kikao cha ushauri cha mkoa hata bungeni, akiomba fedha na vifaa hivyo virejeshwe Hai, ili kushughulikia tatizo la maji.

chanzo: MWANANCHI, JULAI 10
Wrong heading, exaggerated substance, we have very few things to write constructively. Jamhuri ya JF OYEEEEEE.
 
Hapo hai mlikuwa mnaishi kwa kukimbizwa na mtu mmoja tena mshamba. Hadi kwenye maji?

Hakuna wazee hapo Hai?

Hapakuwa na uongozi wa CCM?

Viongozi wa Dini na kamati za amani hawapo?

Hakika Mkuu wa Mkoa alikuwa wakuja
Sabaya hakua peke yake kwenye uporaji. Alilindwa na VIOMBO!
 
Back
Top Bottom