KILIMANJARO: Ugonjwa wa Kipindupindu walipuka, watu 26 walazwa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Mkuu wa Mkoa Anna Mghwira amesema Wagonjwa 26 wamelazwa katika hospitali ya TPC huku eneo hilo likitengwa mahususi kwa kuhudumia wagonjwa hao

Wagonjwa wengi wanatoka Wilayani Simanjiro huku ikielezwa kuwa mlipuko huo ni miongoni mwa athari zilizotokana na mafuriko katika maeneo mengi ya bonde la mto Pangani

Maeneo yaliyoathirika zaidi kwa mkoa wa Kilimanjaro ni Chemchem, Kirungu, Mikocheni, Kahe na New land huku kwa upande wa Mkoa wa Manyara ni eneo lote la Msitu wa Tembo

Aidha, ni nadra sana kwa Kilimanjaro kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na usafi uliopo katika mkoa huo
 
nilishtuka kilimanjaro mji wa moshi unaongoza kwa usafiii.... halafu kipindupinduuu....yabidi kata/tarafa/vijiji viige sera ya usafiii ya MJI WA MOSHI
 
Mkuu umepanick
ktk post,wagonjwa ni wa simAnjiro, ila wanatibiwa Kilimanjaro
Kilimanjaro sii wAchafu ka kAgera ndio maana moshi inaongoza usafi daily
pole kwa mhemko
mwaguma
Hahaha nilijua.lazima unipige misumari, vipi usharudi TZ?? Au bado unakula dunia?
 
Watu pakikucha tu unakuta wamejazana kwenye vibanda umiza vya mbege, mbege ni tatizo uandaaji wake una ukakasi. wanatumia maji ya mfereji si salama
 
Back
Top Bottom