Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,796
- 11,959
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), unapenda kutoa taarifa ya hali ya ukamatwaji wa waandishi na watanzania wanaotumia mitandao ya kijamii katika kutoa taarifa kwa umma.
Mwaka 2018 Kanuni za Maudhui Mtandaoni zilitungwa na kuanza kutumika. THRDC kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu pamoja na Baraza la Habari Tanzania tulifungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Mtwara kupinga kanuni hizo kutokana na ukweli pekee kwamba zinakiuka uhuru wa kujieleza pamoja na haki ya kutumia mitandao bila masharti na gharama yoyote. Kesi hiyo bado inaendelea mahakamni mpaka sasa.
Tangu kutungwa kwa Kanuni hizo, waandishi wengi wamekamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za kuendesha au kumiliki akaunti mbalimbali mtandaoni bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Kukamatwa kwa waandishi hao jana ni muendelezo wa utekelezaji wa Kanuni hizi ambazo tangu kutungwa kwake tumezipigia kelele kuwa hazifai kwasababu zinaminya uhuru wa kujieleza kinyume na Katiba.
Waandishi hao na mmiliki huyo wa YouTube akaunti walikamatwa jana siku ya Jumapili tarehe 05 Aprili 2020 kwa tuhuma za kumiliki blog bila ya kuzisajili. Waandishi hao ni: Tumsifu Kombe na Johnson Jabir. Mmiliki wa YouTube akaunti bado jina lake halijafahamika.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Kilimanjaro Bw. Nakajumo James ni kwamba: Jana jumapili jioni waandishi hao walikamatwa na askari wa jeshi la polisi aliyejitambulisha kuwa anatokea Dar es Salaam. Waandishi hao walipelekwa kituo cha polisi kati mjini Moshi. Askari huyo alionyesha pia picha za waandishi wengine kadhaa ambao wapo kwenye orodha ya kukamatwa kutokana na tuhuma za kumiliki blog bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umemuagiza wakili wake Emmanuel Makiya kufuatilia haki za waandishi hao ili haki iweze kutendeka. Mtandao utaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu kushikiliwa kwa waandishi hao.
Wito wa Mtandao
1. Jeshi la Polisi linapaswa kuzingatia haki za watuhumiwa hao ikiwemo kuwaachia huru au kuwafikisha mahakamani ndani ya masaa 24 kwa mujibu wa kifungu cha 64 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20
2. Mtandao unatoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni, watumiaji wa mtandaoni, watunga sheria na wadau wote wa haki nchini kuendelea kupinga Kanuni hizi ambazo kimsingi zipo kinyume na misingi ya haki ya uhuru wa watu kujieleza kwa kutumia njia yoyote ile ambayo wao wameichagua ikiwemo kutumia mitandao. Ikumbukwe kuwa mitandao ya kijamii ipo bure kwa kila mtu duniani kutumia na wenye mitandao hii hawajahi kudai wanaotumia walipie chochote.
Imetolewa
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
Aprili 06, 2020