Kilimanjaro Stars yashinda kombe la Challenge 2010

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
mpira umekwisha na kili stars wameshinda kwa goli moja ambalo limefungwa na Nsajigwa
Hureeeeeeeeeee Tanzania
 
sasa esa na kombe vinabaki hapahapa bongo. this is great...najua sasa tumepanda kiwango kwenye orodha ya fifa
 
Jk alikuwepo?maximo alikua hana jipya kama vile ccm haina jipya kwa watanganyika
 
Hatimaye tumeupata ushindi!pongezi kwa wachezaji wa kilimanjaro stars na watanzania wote wanaopenda michezo!nimeshangaa sijamuona JK!
 
Leo timu yetu ya taifa imeweza kuchukua Kombe la challenge hivyo basi ni wazi tuendelee kujipongeza kwa kuwauwa Tembo wa Ivory Coast. Nina maswali ya kujiuliza kwanini timu yetu tusiite Tanganyika Stars kuliko hilo la Kili Star? au nini cha kufanya tuite kili Stars?
 
Hongera tanzania,pia yamewashuka wale wambea waliosema jk ana gundu,jk ndie amehamasisha soka letu nakulipa msisimko hongera jk hòngera paulsen,hongera captain nsajigwa,hongera wachezaji wote wa stars
 
Hongereni watz. Maximo na fitna zake kwa kaseja ilikuw kikwazo kwa soka la bongo
Umeona mkuu!!! yaani kaseja ni lulu. juzi kapangua penati na ndio maana leo hii tunashangilia huu ushindi. angekuwepo maximo kaseja asingecheza, hivyo ile penati isingezuiliwa...afazali maximo hayupo..tutaendelea kushinda!!!
 
Hongera tanzania,pia yamewashuka wale wambea waliosema jk ana gundu,jk ndie amehamasisha soka letu nakulipa msisimko hongera jk hòngera paulsen,hongera captain nsajigwa,hongera wachezaji wote wa stars

inasemekana JK asingekuwepo tungeshinda kwa mabao mengi mno. watu wanasema hata huu ushindi tumeupata kwa taabu mno!!!
 
Kwanini tusipongezane Watanganyika ukisema watanzania inamaanisha na Zanzibar au umesahau na Zanzibar nao walitolewa
Hatimaye tumeupata ushindi!pongezi kwa wachezaji wa kilimanjaro stars na watanzania wote wanaopenda michezo!nimeshangaa sijamuona JK!
 
Back
Top Bottom