Kilimanjaro Stars yaadhibiwa vibaya na Uganda Cranes

erfan

Member
Nov 20, 2011
70
17
Timu ya Kilimanjaro Stars imeaga mashindano ya Cecafa Tusker Chalenji baada ya Uganda Cranes kuiadhibu 3-1.
Kilimanjaro Stars walianza kwa kishindo kufuatia bao la kuongoza liliofungwa na Mrisho Ngasa na kuwafanya mpaka kinamalizika kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa Uganda kulishambulia lango la Kilimanjaro Stars na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa kapteni wa Andrew Mwesiga kwa kichwa kufuatia mpira wa kona.
Baada ya kumalizika dakika 90 zikaongezwa dakika 30 ndipo Waganda walipomaliza kazi kufuatia goli la pili lilowekwa kimiani na Emmanuel Okwi kwa kichwa baada ya kupata krosi toka upande wa kulia.
Goli la tatu limefungwa na Isaac Isinde kwa njia ya penati baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa na Juma Nyoso wakati akienda kumsalimia Juma Kaseja.
Kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars itakutana Sudan katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ambapo katika mechi ya mapema Rwanda ilitinfa fainali baada ya kuifunga Sudan kwa mabao 2-1.
Fainali inatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi ya desemba 10.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom