Kilimanjaro stars thread!!

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
Kili Stars kazi moja muhimu leo Send to a friend Thursday, 09 December 2010 21:48 0diggsdigg

kocha%20poulsen.jpg
Michael Momburi
KILIMANJARO Stars leo ina kazi mbili muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Chalenji dhidi ya bingwa mtetezi, Uganda Cranes.

Kwanza, inatakiwa kulipa kisasi na kumaliza uteja dhidi ya Waganda hao na pili ni kuwapa zawadi mashabiki wake kwa kushinda mchezo huo na kucheza fainali Jumapili.
Uganda Cranes ambao ndio mabingwa watetezi waliotwaa kombe hilo mfululizo kwa misimu miwili iliyopita, inakumbana na Kili Stars ikiwa ni mara ya pili kwenye michuano ya Chalenji tangu mwaka 2000.

Katika mchezo wa kwanza jijini Kampala, Uganda, Waganda hao walishinda kwa mabao 2-1 na mwaka jana nchini Kenya wakashinda tena kwa mabao 2-0.

Katika michuano ya msimu huu, Uganda Cranes iliyokuwa Kundi C imekuwa ikitumia mifumo ya 4-5-1 au 4-4-2 na imeshinda mechi mbili dhidi Harambee Stars ya Kenya 2-1 na Ethiopia 2-1 na kutoka suluhu na Malawi 0-0 kwenye hatua ya makundi ambapo kwenye robo fainali iliitoa Zanzibar kwa mikwaju ya penalti 5-3.

Kili Stars chini ya kocha Jan Poulsen, 64, ikitumia mifumo ya uchezaji kama ya ile ya Uganda, imeshinda mechi mbili kwenye hatua ya makundi ambako ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na Zambia, ikazinduka na kuichapa Somalia mabao 3-0, kisha ikaikung'uta Burundi mabao 2-0 na katika hatua ya robo fainali ikaifunga Rwanda bao 1-0.

Kwa vyovyote vile, mchezo wa leo unatazamiwa kuwa na kasi ya aina yake huku Poulsen akitambia morali waliyo nayo wachezaji wake ambayo inampa uhakika wa kufuta rekodi ya Uganda kutamba kwenye michuano hiyo ya Cecafa.

"Uganda ni timu ngumu ambayo haijapoteza mchezo, lakini wachezaji wangu wana morali ya kutosha na nguvu za kuwasimamisha, hatuhofii timu yoyote ile kwenye mashindano haya, tunaingia uwanjani kuikabili Uganda tukisaka ushindi na nafasi ya kucheza fainali,"alisema Poulsen.

"Ninao majeruhi wawili ambao hawatacheza, Mohammed Banka ameumia na Henry Joseph anayesumbuliwa na malaria, lakini wapo wachezaji wengi zaidi tunaoweza kuwatumia kuziba nafasi zao.

"Lakini, tutaangalia wachezaji wataamkaje, tunaomba kuungwa mkono na mashabiki wetu na hatutawaangusha, tutajitoa kwa nguvu zote,"alisisitiza kocha huyo katika mazoezi ya jana asubuhi kwenye Uwanja wa Karume.

Naye nahodha wa Kili Stars, Shadrack Nsajigwa alisema: "Tunaijua Uganda, tumecheza nayo mara nyingi tutaikabili vilivyo ili kuhakikisha tunasonga mbele,wachezaji wana morali na uchu wa ushindi."

Kulingana na mwenendo wa mazoezi, kikosi cha kwanza cha Kili Stars huenda kikawa; Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa, Stephen Mwasika, Kelvin Yondani, Juma Nyosso, Shabaan Nditi, Mrisho Ngassa, Jabir Aziz, John Boko, Nurdin Bakari na Idrissa Rajab.

Kocha wa Uganda, Bobby Williamson, raia wa Scotland alisisitiza jana asubuhi mazoezini: "Najua Tanzania ina sapoti kubwa ya mashabiki, ni kikosi chenye wachezaji wenye morali ya kupambana bila kukata tamaa, tumewaona kwenye mechi zao zote wachezaji wote wanajuana nadhani itakuwa mechi nzuri sana kwa mashabiki kuangalia."

"Tunasisitiza kwamba sisi (Uganda) hatuogopi, hatujawahi kuogopa na hatutaogopa timu yoyote ile, tuna uwezo wa kumfunga yoyote kwenye ukanda huu,"alisisitiza kocha huyo huku nahodha wake ambaye ni beki wa kati, Andy Mwesigwa akisema: "Tutafanya kazi, Mungu ataamua."

Mechi hiyo itachezwa saa 10.00 jioni, ikitanguliwa na nusu fainali ya kwanza baina ya Ivory Coast na Ethiopia ambayo makocha wote wamekiri kuwa itakuwa ni patashika kwa vile wachezaji wote wanafanana kwa mambo mengi, ikiwemo, umri na staili za uchezaji

Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom