Kilimanjaro: Serikali yafunga migahawa isiyo na vyoo kwa muda usiyojulikana

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Serikali wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imeyafunga masoko mawili ya Longoi na Rundugai, kambi zote za vibarua wa mashamba ya vitunguu na migahawa isiyo na vyoo kwa muda usiyojulikana katika vijiji vya kata ya Rundugai ili kudhibiti maambukizi mapya ya ugonjwa wa kipindupindu katika wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya hiyo Bw Antony Mtaka amechukua hatua hiyo baada ya kulipuka kwa ugonjwa huo ambao ulikuwa haujaingia mkoani Kilimanjaro kwa muda mrefu ambao hadi jana wagonjwa 35 walikuwa wametibiwa katika zahanati ya kata ya Rundugai.

Bw Mtaka amesema, masoko na mighahawa hiyo imefungwa ili kuzuia maambukizi hayo kutokana na msongamano mkubwa katika maeneo hayo na matajiri wenye mashamba ya vitunguu wameagizwa kujenga vyoo kwa siku saba na nyumba za kudumu katika mashamba yao.

Mwenyekiti wa kijiji cha Chemka ambacho kimeathiriwa zaidi kutokana na shughuli za kilimo Bw Iddi Jacob amesema, ugonjwa huo umeletwa na watu kutoka vijiji vya wilaya ya Simanjiro ambao huwa wanakuja katika vijiji vya wilaya ya Hai kufanya kazi za vibarua mashambani.

Mganga mkuu wa wilaya hiyo Dr Paul Chaote amesema, kati ya wagonjwa 35 walioripotiwa wagonjwa 26 wametoka wilaya ya Simanjiro na kwamba hadi jana ni wagonjwa watatu tu walikuwa wamebaki katika zahanati ya kata ya Rundugai akiwemo mtoto mmoja na mwananchi kutoka Singida.


Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom