KILIMANJARO: Polisi linamtafuta Dominick Kweka (65) kwa kumbaka mtoto wa dada yake

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamtafuta mzee wa umri wa miaka 65 Dominick Kweka wa kijiji cha Kisereni wilayani Hai kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 16 ambaye ni mtoto wa dada yake (mjomba) na kumpa ujauzito ambao sasa una umri wa miezi sita.

Akizungumza na ITV kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro bw Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa juhudi za kumsaka zinaendelea ili afikishwe katika vyombo vya sheria.

Kamanda mutafungwa amesema, Jeshi la Polisi katika mkoa huo halitavumilia kuona vitendo vya ubakaji vikiendelea kutokea kwa watu wa aina hiyo ambao wanakatisha maandalizi ya maisha bora ya wanafunzi wasichana.

Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Nkuu amesema, mjomba wake huyo alimbaka nyumbani kwake wakati alipompelekea sola kwa ajili ya kuichaji ili apate nafasi nzuri ya kujisomea nyakati za usiku na ameiomba serikali aendelee na masomo baada ya kujifungua.

Baba mzazi wa msichana huyo Bw Kilasauko Nyuki ameiomba serikali imchukulie hatua kali za kisheria mzee huyo mwenye makazi katika kijiji hicho na majiji ya Arusha na Dar es Salaam ambaye inadaiwa ametoroka baada ya tukio hilo.

ITV ilitembelea katika kijiji cha Kisereni hadi nyumba ya mtuhumiwa na nyumbani kwa babu aliyekuwa akiishi msichana huyo mzee Kundambora kweka ambaye amesema hakuwa na mashaka na mtuhumiwa huyo kwa kuwa ni mtu wa nyumbani na kuiomba serikali isimuonee huruma kwa kuwa ni muuaji.

Chanzo: ITV
 
huko moshi vipi mmekula mdudu gani
 
Watu wengine sijui tamaa zao hizo ni za ndagu,ona sasa kiumbe hiki kinavyoishi kama digidigi na kikamatwe kipigwe mvua ya miaka 30 nikijulisha 65 aliyonayo ni sawa na 95.Simuoni akitoboa hiyo miaka ukiweka na Mateso ya nyapara.
 
Hv mzee wa miaka 65 anaweza kumzidi nguvu msichana wa miaka 16 mpaka akafanikiwa kumbaka bila mtoto kukubali. Au kwa kuwa siku ya hatari msichana anakuwa na hamu Sana alikubali mwenyewe.
 
Back
Top Bottom