Kilimanjaro Na Tanga Kuwa Na Uranium Na Mafuta

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,219
2,000
Moshi. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga,
imeonyesha kuwa na matumani ya kuwa na
utajiri mkubwa wa mafuta.
Mkoa wa Kilimanjaro pia umeonekana kuwa
na dalili za kuwa na madini ya urani na
kuufanya mkoa huo wenye mlima mrefu
kuliko yote Afrika, kuwa na uwezekano wa
kuwa na utajiri wenye manufaa makubwa
kwa Tanzania.
Wakuu wa mikoa hiyo, jana walithibitisha
kuwa tafiti zilizofanyika kwa nyakati tofauti,
zimethibitisha matumaini ya utajiri huo.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama
alisema katika mkoa wake mafuta
yamegundulika katika Bonde Pangani katika
vijiji vya wilaya za Moshi Vijijini, Mwanga na
Same.
“Ni kweli kuna watu wanafanya utafiti wa
mafuta pale Chekereni Moshi Vijijini kuna
mwelekeo wa kupatikana kwa mfuta katika
bonde lote hilo kuanzia Same hadi Moshi
Vijijini,” alisema Gama.
Gama alisema ishara za kuwepo kwa mafuta
ndizo zilizosukuma kuanza kwa utafiti huo.
“Tusubiri tuone yakipatikana itakuwa ni
neema kwa Kilimanjaro na taifa,” alisema.
Wakati mkuu wa mkoa akisema hivyo,
Mbunge wa Mwanga ambaye pia ni Waziri wa
Maji, Profesa Jumanne Maghembe, naye
alithibitisha kuwepo kwa dalili za kupatikana
kwa mafuta katika ukanda huo.
“Ni kweli walianzia utafiti wao pale Ziwa
Chala na Ziwa Jipe halafu wakaenda hadi
Kijiji cha Butu mpaka Mkomazi pale jimboni
kwangu na kuna dalili za kuwapo kwa
mafuta,” alisema Profesa Maghembe.
Profesa Maghembe alisema taarifa za
wataalamu wa miamba pia zinaonyesha
kugunduliwa kwa madini ya Urani katika
milima ya Kijiji cha Kivisini.
“Hii ni neema kwa kweli kwa sababu
rasilimali zote hizi mbili zikigunduliwa hapa
kwetu ni manufaa makubwa ya kiuchumi si
kwa mkoa tu lakini kwa taifa zima hili si
jambo dogo,” alisema waziri.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa
alisema dalili za kuwepo kwa mafuta katika
ukanda wa bahari ya mkoa wake, zimeanza
kuonyesha matumaini na utafiti kwamba
unatarajia kukamilika mwaka ujao.
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,850
2,000
Huu ndo muda wa J Nassari kutangaza kuwe na taifa LA kaskazini:) ukabila mbaya sana limjazalo rohoni MTU ndo limtokalo mdomoni
 
samaki2011

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
1,775
0
Ili tuwe matajiri kutokana na rasilimali zetu ni sharti ccm watoke kwenye system otherwise mambo ni yale yale. CCM wamefilisi madini kila eneo la tanzania, wanyama pori, na sasa ivi wameingia kwenye gesi. Lazima mabadiliko ya haraka yafanyike.
 
mirisho pm

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
3,445
2,000
sitaki kusikia laana kama hiyo imegunduliwa moshi, sitaiki kabisa..... hizo ni laana....
 
MANI

Platinum Member
Feb 22, 2010
7,287
2,000
Ili tuwe matajiri kutokana na rasilimali zetu ni sharti ccm watoke kwenye system otherwise mambo ni yale yale. CCM wamefilisi madini kila eneo la tanzania, wanyama pori, na sasa ivi wameingia kwenye gesi. Lazima mabadiliko ya haraka yafanyike.

Kabisa mkuu kwani dhahabu inaisha na sijui tumepata nini kimaendeleo zaidi ya kuachiwa mashimo ambayo sijui tutayafukiaje.
 
ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Huu ndo muda wa J Nassari kutangaza kuwe na taifa LA kaskazini:) ukabila mbaya sana limjazalo rohoni MTU ndo limtokalo mdomoni
Pamoja na kwamba ukabila ni mbaya na umekujaa...Nakuhakikishia kuwa wachaga, wapare, wadigo, wasambaa, wazigua hawatakubali kuwa mafala kama wasukuma ambao dhahabu na almasi zao zinaenda kujenga ulaya... Bora kaskazini ijitenge kuliko kuendelea kuwa na watawala wenye kwenda kuficha matrilioni uswis...Btw Wamakonde na wamakua wanastahili pongezi wanahitaji misaada ya wapenda maendeleo wote wa nchi hii...
 
mbota

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
834
500
Baada utafiti huo Mungu awapige upofu wachina hawa ambao wamegeuka kuwa wahujumu uchumi wa watanzania
 
Jan 1, 2014
19
0
Mimi natafuta mchumba mwenye sifa zifuatazo:- 1. Awe na elimu ya kuanzia kidato cha sita 2.Awe mcha Mungu 3. Awe tayali kuishi nchi yoyote kati ya nchi za East Africa .
 
babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,219
2,000
Pamoja na kwamba ukabila ni mbaya na umekujaa...Nakuhakikishia kuwa wachaga, wapare, wadigo, wasambaa, wazigua hawatakubali kuwa mafala kama wasukuma ambao dhahabu na almasi zao zinaenda kujenga ulaya... Bora kaskazini ijitenge kuliko kuendelea kuwa na watawala wenye kwenda kuficha matrilioni uswis...Btw Wamakonde na wamakua wanastahili pongezi wanahitaji misaada ya wapenda maendeleo wote wa nchi hii...

Mkuu hiyo kitu imegundulika kwa Wajanja sasa cjui itakuaje maana cpati pcha.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Kabisa mkuu kwani dhahabu inaisha na sijui tumepata nini kimaendeleo zaidi ya kuachiwa mashimo ambayo sijui tutayafukiaje.

Mimi bado sijatoa siri yangu ya moyoni, nilipokuwa mdogo kabla sijaanza kwenda shule ya msingi, baba alikuwa na ng'ombe nikawa wakati fulani nawasindikiza waendao kuchungu, kuna sehemu bonge fulani karibu na kijito kulikuwa kunatoka mafuta ardhini na mengi yakawa yanaelea juu ya maji, dalili kwamba hapo kuna mafuta tu ni chini ya mapangano ya milima. Ipo siku nitavujisha siri kwa chombo kinachoaminika kwa manufaa ya taifa.
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,664
2,000
Itakuwa vipi iwapo uranium itapatikana ndani ya mlima wenyewe wa Kilimanjaro; utafumuliwa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom