Kilimanjaro: Mwekezaji alima bangi na kuichakata na kupeleka nje ya nchi

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
93,061
2,000
Mwekezaji wa kigeni raia wa Poland Bw. Damian Sankowisik amekamatwa na mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini eneo la Njiapanda Mashariki wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya kukutwa akizalisha mazao ya bangi na kuchakata kupeleka nje ya nchi.

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.

Screenshot_20200209-162953.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,475
2,000
Mmawia,

Kwa Tanzania kosa ni kuvuta bangi, kuuza bangi na kukutwa na bangi, lakini kule kwetu bangi inajiotea tuu yenyewe, tunakula kama mboga.

Kimataifa bangi inafanyiwa industrial reprocessing kutengeneza medical marijuana inayotumika as prescription medicines for pain relief kwa chronic pain, na pia wana extract mafuta ni dawa.

TIC wana wawekezaji 5 lined up for this. Sheria tuu ndio kikwazo.
P
 

Baraja

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
745
1,000
Kenya walikuwa wakisafirisha kilo tele za miraa kwenda ng'ambo mpaka pale walipowekewa vizingiti na mabeberu. Hii kitu soko liko wazi mnoo na lina pesa nzuri mnoo! Hii mijitu bado haioni fursa tu!?

Niuseme ukweli tu, ikihalalishwa, wavutaji watakuwa wachache mnoo, sababu wengi watajikita katika uzalishaji mkubwa, bado tumezubaa!
 

MjuviKitambo

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
702
1,000
Hii kitu haina shida sana na ni biashara nzuri tu. Inalimwa, unauzwa, na inavutwa wazi wazi tunashuhudia wala haina tatizo.
Iruhusiwe kulimwa large scale na small scale . Mimi pia nitalima small scale. Nb situmii bangi lakini sina tatizo na wanaotumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom