Kilimanjaro mmetisha kwa shule za sekondari!

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,657
20,940
Nilikuwa naangalia matokeo ya form 4, nimeshangazwa na wingi wa shule za sekandari mkoani kilimanjaro. mkoa una watu 1.6m una sekondari za o-level 279!

Dar ya makonda ina watu 5m na shule za sekondari 230 tu! ukitoa 6 za mwisho zinabaki 224 tu. ili iifikie moshi inapaswa kuwa na si chini ya shule 847. makonda una kazi kubwa vinginevyo utakuwa na mkoa mbumbumbu.

Mwanza ya watu 2.7m ina shule 218 tu. wana kazi kubwa ya kujenga shule.

kagera ya watu 2.5m ina shule 150 tu hii ni aibu kubwa wahaya.

Mbeya kabla ya kugawanywa ilikuwa na watu 2.7m na shule 270. bado wana kazi kubwa kufikia Kilimanjaro ukiconsider idadi ya watu.

nafikiri tunahitaji mpango wa shule za kata awamu ya 2 hasa Dar es salaam. hongereni kilimanjaro japo sijui kama mnakidhi idadi inayotakiwa.
 
Asilimia kubwa ya shule za kilimanjaro wanafunzi wengi wanatoka mikoani kuja kusoma kilimanjaro. Mtoa mada unaongea kama hizo shule za kilimanjaro wanafunzi wake ni watu wa kilimanjaro tuu!!!!
 
Mikoa yote uliyotaja Wanafunzi wanatoka Dar es salaam wanaenda kusoma uko. Awo Wanafunzi waliotoka katika top ten wote ni wazaliwa wa Dar es salaam na ni wakazi wa Dar es salaam, ingawa wanasoma kule
mkuu ni watu wachache wenye uwezo huo wa kupeleka watoto mikoani. wengi wanategemea hizi shule za kata na dar ziko kiduchu sana. pia shule nyingi ni za kata, hazichukui wanafunzi wa bweni na nje ya mkoa.
 
Back
Top Bottom