Kilimanjaro: Mkuu wa Mkoa aagiza huduma ya Chanjo kupelekwa kwenye Nyumba za ibada

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai amewaagiza wataalamu wa afya mkoani humo, kupeleka huduma ya chanjo ya Uviko 19 kwenye maeneo yote ya ibada, ili kuwezesha wananchi wote kufikiwa na huduma hiyo.

Mbali na hilo amewataka watumishi wote wa Umma kuonyesha mfano kwa jamii kwa kujitokeza kwa wingi kuchanja ili kutoa hamasa kwa wananchi na kuwawezesha wote kuhamasika na kuona umuhimu wa kupata chanjo.

Kagaigai ametoa maagizo hayo Septemba 30, 2021wakati akizungumza kwenye mkutano wa afya ya msingi ya mkoa na wadau kuhusu uhamasishaji na ushirikishwaji wa utekelezaji wa mpango wa Uviko 19 mkoani hapa.

“Naagiza kuanzia kesho Ijumaa wahudumu wapeleke huduma ya chanjo ya Uviko kwenye maeneo yote ya ibada, kesho mwende msikitini, Jumamosi mwende makanisani yanayosali siku hiyo na jumapili vivyo hivyo,” amesema Kagaigai.

Maagizo mengine aliyoyatoa Kagaigai ni kuelekeza wilaya ambazo hazijafanya vikao vya kamati ya afya ya msingi kufanya mara moja, viongozi wa ngazi zote kusimamia utoaji wa elimu sahihi na huduma ya chanjo katika maneo yao.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa wale wote ambao watabainika kufanya mzaha kuhusiana na chanjo hiyo, wachukuliwe hatua kama wahujumu wa afya za watanzania.

“Nimekuwa nikisisitiza wale wote ambao wamekuwa wakifanya mzaha kuhusiana na chanjo hii, naomba wasifumbiwe macho. Taarifa zitolewe na wachukuliwe kama watu ambao wanataka kuhujumu afya za Watanzania,” amesema.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Credianus Mgimba amesema Mkoa wa Kilimanjaro ulipokea dozi 60,000 ya chanjo za Uviko-19 na mpaka kufikia Septemba 29 tayari zimetumika chanjo 38,785.

Awali akizungumza meneja mradi Kanda ya Kaskazini shirika la EGPAF Dk Alphaxad Lwitakubi amesema juhudi za kutoa elimu juu ya chanjo ya Uviko 19 ni muhimu likawekewa nguvu kama ilivyo kwa magonjwa mengine sugu.


Mwananchi
 
msisahau kupeleka na kwenye kanisa la ufufuo na uzima 😂😂😂
 
Back
Top Bottom