Kilimanjaro: Mhujumu Uchumi ahukumiwa kulipa faini Tsh. Mil 333 au kwenda jela miaka 20

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
MSHITAKIWA katika shauri namba 11/2018 ya uhujumu uchumi na makosa ya kupanga Omari Bokoi amehukumiwa kulipa faini ya Sh Mil 333 au kwenda jela miaka 20 baada ya mahakama ya wilaya ya Same ,mkoani Kilimanjaro kumkuta na hatia ya kupatikana na vipande vya nyama ya Twiga.

Hai.png

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Helen Hoza alitoa hukumu hiyo, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi sita na vielelezo tisa vilivyowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka.

Mahakama iliwaachia huru washitakiwa wawili, Omari Mnoa na Peter Charles baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani.

Katika mashitaka ilidaiwa mahakamani kuwa Oktoba 15 mwaka 2018 katika eneo la Muheza karibu na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wilayani Same washitakiwa walikutwa na vipande vya nyama ya Twiga vyenye thamani ya Sh milioni 33.3 sawa na Dola 15,000 za Marekani.

Ilidaiwa pia kuwa Bokoi alikutwa na gunia moja likiwa na vipande hivyo ambavyo ni sawa na kuua twiga mmoja, akiwa amevibeba kwenye pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usajili Mc 661 ATV, bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Samuel Magoka, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kufanya vitendo vya ujangili.

Alieleza kuwa, wanyama jamii ya twiga wameendelea kutoweka na serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kuwalinda.

Magoka alisema, twiga ni nembo ya taifa na kivutio cha watalii kinachoiingizia serikali fedha.

Kabla ya hukumu mshitakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu ana mke na mtoto ambao wanamtegemea na pia amekaa rumande kwa miaka miwili wakati wa usikilizwaji wa kesi yake.
 
Kwa wajuvi, inawezekana kufanya makubaliano na mahakama ya kulipa kwa mfano hiyo milioni 333 kidogo kidogo ukiwa nje au ni lazima ilipwe kwa mkupuo?
Na je kichwa cha habari kiko sawa kuwa alipe milioni 333 ilhali Twiga ana thamani ya milioni 33.3 tu?
 
MSHITAKIWA katika shauri namba 11/2018 ya uhujumu uchumi na makosa ya kupanga Omari Bokoi amehukumiwa kulipa faini ya Sh Mil 333 au kwenda jela miaka 20 baada ya mahakama ya wilaya ya Same ,mkoani Kilimanjaro kumkuta na hatia ya kupatikana na vipande vya nyama ya Twiga.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Helen Hoza alitoa hukumu hiyo, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi sita na vielelezo tisa vilivyowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka.

Mahakama iliwaachia huru washitakiwa wawili, Omari Mnoa na Peter Charles baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani.

Katika mashitaka ilidaiwa mahakamani kuwa Oktoba 15 mwaka 2018 katika eneo la Muheza karibu na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wilayani Same washitakiwa walikutwa na vipande vya nyama ya Twiga vyenye thamani ya Sh milioni 33.3 sawa na Dola 15,000 za Marekani.

Ilidaiwa pia kuwa Bokoi alikutwa na gunia moja likiwa na vipande hivyo ambavyo ni sawa na kuua twiga mmoja, akiwa amevibeba kwenye pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usajili Mc 661 ATV, bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Samuel Magoka, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kufanya vitendo vya ujangili.

Alieleza kuwa, wanyama jamii ya twiga wameendelea kutoweka na serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kuwalinda.

Magoka alisema, twiga ni nembo ya taifa na kivutio cha watalii kinachoiingizia serikali fedha.

Kabla ya hukumu mshitakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa sababu ana mke na mtoto ambao wanamtegemea na pia amekaa rumande kwa miaka miwili wakati wa usikilizwaji wa kesi yake.
Nyama ya TWIGA alipe faini million 333? Hapana naenda jela miaka 20 najua nitakaa si zaidi ya miaka 10
 
Masikini ndio hufungwa. Wale wa Epa na Escrow wengi wapo mitaani wanakula maisha
 
Back
Top Bottom