Kilimanjaro: Madiwani waliounga mkono juhudi na kuangushwa na wajumbe warudishwa kwa wingi. Wapo walioshika mkia lakini jina limerudi

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Hatimaye sasa imejulikana kwanini CCM walichelewesha kutangaza majina. Waliounga juhudi na kuangushwa vibaya na wajumbe wa CCM wamerudishwa kwa wingi ili wakawe wagombea.

Mfano zipo kata unakuta muunga mkono juhudi alipata kura 12 na akawa wa mwisho na mshindi ana kura za wajumbe 50 lakini mwenye kura 12 amerudishwa kisa tu aliunga juhudi mkono.

Hali hii italeta vurugu sana na huenda ikatokea hata kwa nafasi za ubunge. Upo uwezekano wa yale ya kulazimisha ushindi ya serikali za mtaa kujirudia.

Inawezekana kabisa ni maelekezo kutoka juu!
 
Huyo aliyepata kura 50 sijui utambembeleza na nini ili uchaguzi mkuu yeye pamoja na wafuasi wake wasipigie kura upinzani! Hii Ni furaha kwa wapinzani.

Alipoondoka upinzani wapiga kura wake walichukia lakini ccm wakafurahi, leo amerudi kugombea ccm wamechukia lakini bado wale wapinzani wanamwona msaliti.

CCM msitegemee kushinda hayo maeneo.
 
Ndiyo maana nikakwambia ni dalili kuwa CCM watalazimisha ushindi
 
Hata
Hatimaye sasa imejulikana kwanini CCM walichelewesha kutangaza majina. Waliounga juhudi na kuangushwa vibaya na wajumbe wa CCM wamerudishwa kwa wingi ili wakawe wagombea...
Hata Diwani aliyemtishia maisha DC wa wilaya ya Hai, jina limerudishwa ni mgombea halali kupitia CCM. Huko musoma mambo ni hayo hayo,wa mwisho kawa wa kwanza.
 
Huyo aliyepata kura 50 sijui utambembeleza na nini ili uchaguzi mkuu yeye pamoja na wafuasi wake wasipigie kura upinzani! Hii Ni furaha kwa wapinzani...

Wananchi Ni wengi kuliko yeye na wajumbe wake, Kura nyingi zitatoka kwa wananchi. Wajumbe ki ukweli huwa Wana mitazamo tofauti na wananchi na ndo maana Kama membe angegombea na Magufuli ndani ya CCM membe angeshinda kwakuwa wajumbe hawaeleweki, lakini nje ya wajumbe magufuli akigombea na membe magufuli atashinda coz Kura nyingi zipo kwa wananchi na sio wajumbe
 
Ukweli ni kwamba hakuna Mwananchi anayemtaka msaliti aliyeuza haki yao. Hayupo!
 
Huyo aliyepata kura 50 sijui utambembeleza na nini ili uchaguzi mkuu yeye pamoja na wafuasi wake wasipigie kura upinzani! Hii Ni furaha kwa wapinzani.

Alipoondoka upinzani wapiga kura wake walichukia lakini ccm wakafurahi, leo amerudi kugombea ccm wamechukia lakini bado wale wapinzani wanamwona msaliti.

CCM msitegemee kushinda hayo maeneo.

Hii ni dalili tosha kuwa CCM haitashinda uchaguzi 2020 lakini Jiwe atatumia Dola kutangaza ushindi. Ndiyo maana kawarudisha Waunga Juhudi wake ambao hawapendwi na wananchi hata chama chake kwa ngazi zote. UDIKTETA wa Jiwe utatamalaki uchaguzi 2020.
 
Wananchi Ni wengi kuliko yeye na wajumbe wake, Kura nyingi zitatoka kwa wananchi. Wajumbe ki ukweli huwa Wana mitazamo tofauti na wananchi na ndo maana Kama membe angegombea na Magufuli ndani ya CCM membe angeshinda kwakuwa wajumbe hawaeleweki, lakini nje ya wajumbe magufuli akigombea na membe magufuli atashinda coz Kura nyingi zipo kwa wananchi na sio wajumbe
Lakini usisahau kuwa hao wajumbe pia ni wananchi-
 
Huyo aliyepata kura 50 sijui utambembeleza na nini ili uchaguzi mkuu yeye pamoja na wafuasi wake wasipigie kura upinzani! Hii Ni furaha kwa wapinzani.

Alipoondoka upinzani wapiga kura wake walichukia lakini ccm wakafurahi, leo amerudi kugombea ccm wamechukia lakini bado wale wapinzani wanamwona msaliti.

CCM msitegemee kushinda hayo maeneo.
Anatishiwa tu mambo ya uhujumu Uchumi na kutakatisha Fedha, anatangaza kukubalianaa na kumuunga mkono aliyepitishwa kwa nguvu zote
 
Back
Top Bottom