Kilimanjaro m' awards.je? MPOTO na MPOKI nani alistahili.

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Wana JF,naomba maoni yenu kuhusu hili. wote wameimba na ku-ghani,aina ya beat ni moja.huyu kaimba "mjomba" mwingine kaimba "shangazi"
*muanzilishi wa tungo alikuwa MPOTO.
*akafuatia MPOKI aka-paste.
Je maamuzi ni sahihi? au ndio ujumbe wa mpoto kwa mjomba umefika na kumponza NAWAKILISHA..........
 
Kwani Mpoki kashnda kwenye category gani?

Ndio mambo ya demokrasia hayo! Hata mimi cjui ni kwa nini CCM inaendelea kutawala Tz:lol:!
 
ni usanii tu!wimbo wa mpoki hauna ujumbe wowote zaidi ucheshi,hakustahili hata kuwa nominee!Hii inadhihirisha kuwa hata waandaaji hawako serious!
 
kosa lilianzia kwa kumchagua kushindana, maana mjue mashindano haya yamepigiwa kura na wapenzi, sasa kama Mpoki ana watu wengi huwa anawapasua mbavu kwenye Comedy unategemea Mjomba Mpoto atapata nini? Tena hili nakumbuka hata Masanja alikuwa akimpigia upatu sana kwenye kile kipindi chao cha ze comedy, lakini mshindi wa ukweli ni Mjomba Mpoto, pole sana Mjomba endelea kutafuta nauli utafika tu.
 
Makosa yalifanyika kumpitisha Mpoki kuwa mshiriki, wakati wimbo wake hauna ujumbe wowote. Waandaaji waangalie sana mambo kama hayo yanaweza poteza maana ya Mashindano.
 
Makosa yalifanyika kumpitisha Mpoki kuwa mshiriki, wakati wimbo wake hauna ujumbe wowote. Waandaaji waangalie sana mambo kama hayo yanaweza poteza maana ya Mashindano.

Maana ya mashindano ipotee mara ngapi?
 
  • Sikiliza mistari ya msanii huyu
  • GAMESIS
  • Wasanii wa Bongo Flava wameshanunuliwa na mafisadi
 
Last edited by a moderator:
kwani haya mashindano ni ya kitaifa na nani aliyapitisha?Mimi nikitoa tuzo zangu je itakuwaje?
 
WaDanganyika kwa kuchakachua hata music hamuachi kitu.

Pale lazima alikuwa apate Off side trick na wimbo wao wa Ahmada au Mpoto na adela. lakini sio Mpoki.

Nahisi ndugu yetu Ruge Mutahaba alifanya mambo pale.

Ingawa inakatisha tamaa wasanii wengine
 
naaam kosa lipo kwa waliopitisha majina kupigiwa kura... Wapiga kura wenyewe ndo walewale waangalia komedi mnategemea nini?

Offcourse mpoto deserved that award
 
Wana JF,naomba maoni yenu kuhusu hili. wote wameimba na ku-ghani,aina ya beat ni moja.huyu kaimba "mjomba" mwingine kaimba "shangazi"
*muanzilishi wa tungo alikuwa MPOTO.
*akafuatia MPOKI aka-paste.
Je maamuzi ni sahihi? au ndio ujumbe wa mpoto kwa mjomba umefika na kumponza NAWAKILISHA..........

Watanzami waliambiwa wampigie kura yule wanayeona ni bora....hawakupewa vigezo. Wakapiga kura kwa utashi wao. Utashi wao uliaminiwa ndio maana wakapewa dhamana ya kuchagua wanayemuona ni bora. Nao hawakufanya ajizi, Mpoki ni bora kuliko Mpoto n.k.

Washindi wasilaumiwe, wapiga kura wasilaumiwe.
 
Wana JF,naomba maoni yenu kuhusu hili. wote wameimba na ku-ghani,aina ya beat ni moja.huyu kaimba "mjomba" mwingine kaimba "shangazi"
*muanzilishi wa tungo alikuwa MPOTO.
*akafuatia MPOKI aka-paste.
Je maamuzi ni sahihi? au ndio ujumbe wa mpoto kwa mjomba umefika na kumponza NAWAKILISHA..........

Mimi naliona tatizo lipo kwa waandaaji wa tuzo kwa kuupitisha wimbo wa MPOKI kuingia kwenye mashindano. Unaweza kuu-nominate uchafu ule watu wakaupigia kura ya kushinda? Ni nani huyo ambaye alipata hata wazo la kuupendekeza huo wimbo wa MPOKI kwa jambo lolote lenye akiri? Kilimanjaro Music award wamefanya mengi makubwa lakini kwa hili WAMEFANYA UTUMBO, UTUMBO TENA UTUMBO ULIOOZA! Acheni mzaha kwenye mambo ya msingi katika maisha.
 
Ndivyo washindi wa Tanzania mara nyingi wamekua wakipatikana: msishangae, hata viongozi wa nchi walioko madarakani wengi tulishangaa walivyo ibuka washindi katika nafasi walizopo.

Hakuna cha Mpoto: Mpoki anafaa kwa zawadi aliyopata kwani ndivyo wapira kura walivyoamua.
 
Kimsingi watanzania wengi hawako makini kwenye mambo ya msingi..................ukimpa mtu aliye kwenye nchi ambayo wako makini na mambo ya msingi asikilize wimbo wa Adela wa Mjomba Mpoto na Shangazi wa Mpoki hawezi amini kilichotokea pale kwenye hizi awards...Nadhani wakati mwingine akili ya kawaida lazima itumike......
 
ndo mambo ya kijinga jinga yanayofanywa na watu wazima ,... ni aibu. na mwingine ataiga ataimba mam dogo afu anapewa tuzo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom