Kilimanjaro: Kutokana na umuhimu wake wananchi waanza kulima kilimo cha Alovera

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,847
15,252
Wakulima wengi mkoani Kilimanjaro kwa sasa wameanza kuangalia fursa mbalimbali katika sekta inayohusiana na kilimo cha mazao ya biashara pamoja na masoko yake.

Baadhi ya wakulima wachache mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Hai wameamua kulima kilimo cha zao la alovera kama zao la biashara baada ya kugundua kuwa kuna masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.

aloe-plantation-most-species-have-rosette-large-thick-fleshy-leaves-46845123.jpg

Kutokana na faida zitokanazo na jani la alovera duniani kote hasa katika kutibu magonjwa mbalimbali kama vile ya Kinywa na ngozi basi zao hili limejipatia soko katika viwanda maalumu kwa ajili ya kulichakata na kutoa bidhaa mbalimbali kwa matumizi binadamu kama vile sabuni za kuogea, dawa za meno, mafuta ya kujipaka na. Pia kama dawa za kutibu magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu.

Zao hili ambalo linaonekana kustahimili hali ya hewa zote ni zao geni la kibiashara mkoani Kilimanjaro na wengi wa wananchi wameonekana kufuatilia kwa ukaribu aina hiyo ya kilimo pamoja na Masoko yake kwa ajili kuangalia namna ya kuanza aina hiyo ya kilimo chenye tija ndani na nje ya
nchi.

Wengi wa wakulima wa zao hilo wanadai kuwa zao hilo sio gharama kubwa kulima kama ilivyo mazao mengine ambayo huitaji mbolea, dawa za kuuwa wadudu nk. Hivyo wameshauri wakulima wenye nia ya kulima zao hilo kutohofia bali walime kwa wingi kwani ndio utakuwa mwanzo wa kuanzishwa kwa Kiwanda kitakacho chakata malighafi hizo na Kuzalisha kitu kingine
large-aloe-plant-orange-flowers-vera-grows-other-desert-plants-trees-garden-setting-175178555.jpg

Hii ni fursa kwa wakulima na vijana ambao hawana ajira kulima zao hili la biashara.

Hii ni aina mpya ya Kilimo cha biashara mkoani Kilimanjaro
 
Cha muhimu vijana waangalie fursa hiyo waingie shambani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom