Kilimanjaro: Basi la Kampuni ya Marangu Coach lapata ajali maeneo ya Kia

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Basi linalomilikiwa na Kampuni ya Marangu Coach, ambalo linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam kwenda Arusha, limepata ajali leo Januari 11, 2019 nje kidogo ya maeneo ya Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (Kia).

Kwa taarifa za awali hakuna vifo isipokuwa kuna abiria kadhaa wamejeruhiwa, huku kukiwa bado chanzo hasa cha ajali hakijafahamika mara moja.

Tutakujuza zaidi baada ya kupata taarifa kutoka kwa mamlaka husikia.!

======

Basi la kampuni ya Marangu Coach limepata ajali maeneo ya KIA mkoani Kilimanjaro

Baadhi ya abiria wamejeruhiwa huku chanzo kikiwa ni utelezi uliosababisha gari hilo kupoteza uelekeo na kupata ajali kutokana na mvua ilionyesha maeneo hayo

IMG_20190111_175422_685.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Doh.. angalau hamna vifo..pole kwa majeruhi wote.
Bado chanzo hakijajulikana?
 
Nawapongeza sana jeshi la polisi kitengo cha barabarani kwa kudhibiti mwendo kasi WA magari ya abiria. Hapo Hakuna vifo kwasababu speed haikuwa kubwa, sipati picha speed ingekuwa kubwa Kama zamani, sijui ingekuwaje :(

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upumbavu wa dereva. Unaona kabisa barabara sio salama why don't you drive max 20km/hr? Badala yake anakomaa na 80KPH tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom