Kilimanjaro: Amuua nduguye kwa kukataa kuchangia nyama ya 1,500 waliyokula

Umasikini mbaya sana ........
umasikini ni laana.........
ukiambiwa hivi elewa
Suala sio umasikini, suala ni kukiuka makubaliano. Inaudhi sana. Ni afadhali ukatae mapema au hata unidanganye kwamba, "isee yaani mfukoni sina kitu kabisa", nilipe kwa ridhaa yangu, roho inakuwa radhi kabisa, kuliko kukubaliana na baada ya mlo kukataa, tena kijeuri!!
Kwani watu wanashindwa kulipa jero ya TARURA? Ni kwa sababu ya utaratibu mbovu!
 
Hapo issue ni malezi tu,watoto waliolelewa kwenye maadili mema hawawezi kuuana bali wataheshimiana na kusaidiana,

Tuwe makini sana katika malezi ya watoto wetu ili wapendane na kusaidiana toka wakiwa wadogo.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Ndungi katika Wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua ndugu yake, William Shoo kwa madai ya kukataa kuchangia nyama ya Sh1, 500 waliyonunua.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 11, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema mauaji hayo yalitokea Oktoba 10, 2021 asubuhi baada ya marehemu kugoma kuchangia nyama hiyo waliyonunua.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, kabla ya mauaji hayo mtuhumiwa alinunua nyama kwa kushirikiana na marehemu ambapo walikula pamoja na walipomaliza kula marehemu alikataa kuchangia chochote ndipo ugomvi ukaanza.

Amesema katika ugomvi huo, mtuhumiwa alimkata ndugu yake na kitu chenye ncha kali kichwani na kusababisha kifo chake.

"Awali kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa alinunua nyama kwa kushirikiana na mwenzake, ambayo ina thamani ya Sh1, 500 walipokula pamoja ndugu yake huyo alikataa kulipia, ndipo ugomvi ukaanza ambapo ilipelekea kuchukua maamuzi hayo ya kumkata na kitu chenye ncha kali"

Katika tukio lingine, Jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumuua John Nyaki kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, wakimtuhumu kuiba mizani.

Kamanda Maigwa, amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 6, 2021, asubuhi katika eneo la Kibosho Dakau Wilaya ya Moshi.
Tulishawazoea watu wa huko. Mmea wa Arusha katika ubora wake. Halafu oohh, Kilimanjaro tumestaarabika. Huo ndio ustaarabu ?
 
Hizi nyakati ni mgumu Sana haya matukio ha ajabu ajabu yamekuwa mengi watu Wana misingi ya mawazo sana
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom